Biashara ya Night Club Dar imekufa?

Mfufua Nyuzi

Senior Member
Mar 11, 2024
193
240
Habari wakuu,

Naona siku hizi zile Night Clubs ndani ya jiji la Dar es salaam hazipo tena zimefunikwa/replaced na Bar kubwa kubwa.

Mfano hapo nyuma palikuwa na club za mziki mbalimbali mfano Billcanas, Maisha basement, Ambiance n.k Lakini siku hizi zile Nights club zimevunjwa na kugeuzwa Lounge,Casinos au bar.

Siku hizi hata ukitaka kuingia club kwa ajili ya kucheza mziki, utahangaika sana tofauti za hapo nyuma kidogo badala yake utaishia kukaa kwenye bar, lounge kubwa kubwa kama vibez lounge, BM Lounge n.k ambazo si club bali ni bar zenye open space kwa ajili ya kukaa na kunywa pekee mziki upo lakini hauna privacy kama club.
 
Habari wakuu
Naona siku hizi zile Night Clubs ndani ya jiji la Dar es salaam hazipo tena zimefunikwa/replaced na Bar kubwa kubwa. Mfano hapo nyuma palikuwa na club za mziki mbalimbali mfano Billcanas, Maisha basement, Ambiance n.k Lakini siku hizi zile Nights club zimevunjwa na kugeuzwa Lounge.Siku hizi hata ukitaka kuingia club kwa ajili ya kucheza mziki, utahangaika sana tofauti za hapo nyuma kidogo badala yake utaishia kukaa kwenye bar,lounge kubwa kubwa kama vibez lounge,BM Lounge n.k ambazo si club bali ni bar zenye open space kwa ajili ya kukaa na kunywa pekee mziki upo lakini hauna privacy kama club.
Hazijafungwa. Subiri mwezi mtukufu uishe ndo utajua bado zipo au hazipo.
 
Habari wakuu
Naona siku hizi zile Night Clubs ndani ya jiji la Dar es salaam hazipo tena zimefunikwa/replaced na Bar kubwa kubwa. Mfano hapo nyuma palikuwa na club za mziki mbalimbali mfano Billcanas, Maisha basement, Ambiance n.k Lakini siku hizi zile Nights club zimevunjwa na kugeuzwa Lounge,Casinos au bar.Siku hizi hata ukitaka kuingia club kwa ajili ya kucheza mziki, utahangaika sana tofauti za hapo nyuma kidogo badala yake utaishia kukaa kwenye bar,lounge kubwa kubwa kama vibez lounge,BM Lounge n.k ambazo si club bali ni bar zenye open space kwa ajili ya kukaa na kunywa pekee mziki upo lakini hauna privacy kama club.
Matokeo ya bendi za muziki kufa, watanzania hawaishi maisha ya raha tunaishi kiupweke kama watoto yatima hatuna furaha.
 
Uholela wa biashara bila vibali. Bar na pubs zinatakiwa kufungwa saa sita usiku. Then club zinakesha. Watu wakitoka bar wanaingia club mpaka asubuhi.
Sasa bar,pub,liquor stores zote zinakesha nani ataenda club?
Hata ndio matokeo ya kutosimamia sheria ndio maana hata mitaani watu hawalali kisa bar inapiga muziki hadi asubuhi.
 
Kuna siku nimeamka asubuhi saa 12 nina mzuka wa kula bata, nikaenda las carinyo sikupaelewa. Nikachukua boda hadi chimbo lingine sikupaelewa pia, boda akasema nikupeleke kuna chimbo lingine wanasema kwa mchina karibu na makaburini kinondoni.

Kufika naingia ndani japo ni padogo lakini watu shazi wamekesha wanakunywa.
Sikukaa sana kwa vile niliona hatuendani.
Siku hizi hizo nights club zipo kwenye frame tu kwa uwekezaji kidogo.
 
Mkuu kila mtaa kuna mabaa makubwa tu, halafu unakuta labda kila jumatano au weekend kuna bendi,open space,mziki upo,na karibu na kwako au mtaani kwako.

Mtu unakaa karibu na maskani ,kufahamiana na usalama wa kutosha .
 
Tembea mkubwa night club choice dar tu ziko nyingi saaaana. Yaani night club ni biashara ya pesa kuliko hizo open bar zenu za kitambaa.
Sasa sijajua umeangalia wingi kwa level ipi. Maana bar hizo ni chache sana zinazo perform kushinda night clubs.
Pitia masaki ujifunze.
 
Kuna siku nimeamka asubuhi saa 12 nina mzuka wa kula bata, nikaenda las carinyo sikupaelewa. Nikachukua boda hadi chimbo lingine sikupaelewa pia, boda akasema nikupeleke kuna chimbo lingine wanasema kwa mchina karibu na makaburini kinondoni.

Kufika naingia ndani japo ni padogo lakini watu shazi wamekesha wanakunywa.
Sikukaa sana kwa vile niliona hatuendani.
Siku hizi hizo nights club zipo kwenye frame tu kwa uwekezaji kidogo.
Hapo kwa mchina panatazamana na kituo cha mafuta?
 
Back
Top Bottom