Beeb
JF-Expert Member
- Aug 18, 2018
- 29,402
- 58,951
Nimekielewa ulichokiandiaka mkuu.nimesoma nacheka huu uzi. Wewe dada nikiacha mengine yote ya kupata waliokupa namba za simu, mara sijui pm muwasiliane mara mkutane mwanza mie nakushauri kama ifuatavyo.
Kuna Uzi humu ukiutafuta unaelezea sana habari za Uganda na Wengine tumetoa uzoefu wetu wa kwenda mara ya kwanza.
Nakusisitiza nenda peke yako. (Sijui umenielewa)?
Siku ya kwanza nilienda peke yangu, sikutaka kupelekwa na mtu nisiyemfahamu. Sasa ukiona yafaa wewe pelekwa na mnaokutana humu uone. (Utaliwa mpk ushangae) we si mwanamke wewe
Sikwambii ufanye nn, ila soma nilivo safiri itakusaidia. Nilienda kukata uhamiaji hati ya dharula ya kusafiria. Kama sikosei ilikuwa 15000/=
Nikapanda gari ubungo, safari ikaanza, nikalala kahama, hapo nimevaa soksi ndefuuu mpk mapajani za mpira humo nimepanga maburungutu ya millions zangu, alafu nikavaa suruali pana tu.
Kesho yake asbh tulitoka kahama nikaingia kampala saa 9 au 10 hivi. Safarini tayari kwenye gari kuna wafanya biashara tulianza kupiga stori njiani (huwakosi) ila sikuwaonesha mie ndio first time
Katika stori tu njiani, nilijua gest ya katikati ya mji, majengo ya bidhaa, lakini pamoja na yote nilitoka na ramani ya hivyo vyote hapa jamii forum (uzi upo) unaeleza mpaka gesti.
Tuliposhuka stand nikachukua boda nikamwambia nipeleke gest flan, alipojua mie Mtanzania akabadili lugha akaanza kugonga kiswahili (kibovu lakini). Prrrrrrrrri tuk tuk mpaka gesti nikalipia elfu 25 ya Uganda ilikuwa kama elfu 15/16 ya Tanzania. Nikalala
Hii gesti niliolala ingekuwa Tanzania basi nimelala karikakoo kabisaa, ukitoka nje ni maduka. Basi asbh mzee nikaanza kukata mitaa mwenyewe napita jengo mpk jengo na study. Lakin nilipolala hapo walilala pia watanzania wawili waanya biashara wazoefu, na mkongo mmoja ambao jioni ile kulikuwa na match chini sehemu ya chakula tukakaa tunapiga stori kabla ya kulala
Aisee katika story walinipa madini sana ya biashara, zinavofanyika, kupita mpakani, na kuongeza kipato kwa kubeba mzigo unapokuja uganda na unabeba unaporudi. So hakuna kusafiri kiboya.
Aisee ni mengi, siwezi eleza yote. Kesho yake kama nilivoeleza hapo juu nikafanya kuzunguka mwenyewe nikajua mengi, nikarud kulala kuwa sasa kesho naenda kununua. Usiku huo pia wakaja watanzania watatu wanawake pale lodge. Wawili toka dar, mmoja kigoma.
Aisee wale wadada tulikaa tujapiga story wakanipa ramani hadi nikahsi naamka tajiri leo. Kesho yake nikaingia nao madukani japo tuliachana, kila mtu akawa bize kufunga mzigo, ukishafungwa moja kwa moja kwenye gari. Kesho yake alfajiri safari
Hapo mnarudi njiani mko wengi, na stori kama zote (naimani ushanisoma eeh?) Utapewa mbinu na kila ujanja.
Dada imetosha. Ondoka nenda, mpk unafika ushakuwa mwenyeji. Kila la kheri.
Dumelang