Biashara ya Michezo ya Video (Video Games): Jifunze Uendeshaji, Changamoto na Faida Zake

Wakuu msaada kidogo ninahitaji kununua Playstation 4...Nimefanya survey kwa sellers wengi kidogo(kwenye page za Instagram) na nimegundua kuna tofauti kubwa ya bei kati ya sellers wa Kenya na TZ kitu amnacho kinanipa wasiwasi kidogo...mfano; playstation 4 Pro sellers wengi wa tanzania wanauza kuanzia laki 8 na 50 na kuendelea ila kuna sellers wa kenya wawili mmoja laki 5 na 40 na mwingine laki 6: Sasa je hizi bei za wakenya ziko real kweli kwa PS 4 Pro tena unapewa 2 Pads na Parcel yako isafirishwe kwa DHL kwa gharama zao?? Hakuna utapeli kweli hapa? Maana this offer is too good to be true..Mwenye experience ya haya masoko ya Instagram hasa Kenya anisaidie
 
Usithubutu. Nenda gerezani kariakoo utapata ps4 nzuri tu. Hao kenya ni matapeli
 

Kama unarafiki yupo kenya mwmabie akachukue akuagizie.
 
Wadau mtupe mrejesho...Ata mimi napenda sana magem na huwa nataman nije kufungua hii biashara
 
Tuma hela tu ili upate uhakika😂
 
Page za Instagram kenya zote ni za matapeli.... Tafuta mtu aliyepo nairobi akutafutie.
Ila bei halisi ninazojua kenya ni ps4 30,000 kesh, ps3 16,000 ksh
 
Naomba kujua km nikiamua kuanza na pc 3 vip wateja wanaweza kupatikana na vip bei ya kucheza game moja
 
Unaweza tuwekea namba zao hao wapemba mheshimiwa Ili kupata TV hizo...... Natanguliza shukrani 🙏🙏
 

 
Ps 4 pro hata iwe 500 GB upati kwa laki 5,tena wamekutangulizia na chambo ya controllers 2,unaenda kupigwa mkuu,hiyo bei hata ps 4 slim upati
 
Nashukuru nimeingia rasmi kwenye hii biashara.

Kiukweli ukipata sehemu za uswahilini, kwa kuanza, unatoboa kiurahisi sana.

Kama ukiwa vizuri zaidi na mtaji wa kutosha, ukipata sehemu za mjini hasa maeneo ya chuo - ni vizuri zaidi, japo sijui exactly wananufaika vipi.

Malengo yangu ni kupiga hii mishe vizuri uswahilini, niingize mzigo wa kutosha then nikapambane huko town.
 

Mawazo yako ni mawazo yangu.. nimenunua TVs na PS 4 nne.. hapa nakusanya mzigo wa furniture na rent huku nikifanya survey ya location nzuri..
 
Mkuu inaonyesha unajua hii biashara vizuri vp kuhusu wanachosema juu ya mapato?natamani kuifanya ila juu ya changamoto zake na je znakabilika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…