Biashara ya Michezo ya Video (Video Games): Jifunze Uendeshaji, Changamoto na Faida Zake

Mkuu sitatumia ps 4, nitatumia ps 3 2 na tv inch 32, 2.....hiyo kwa bei ya laki 3 vyote ni mil 1 laki 2.....laki 150 padi za akiba laki 150 kodi miezi 3....

nitachezesha mechi 2 za dakika 10 kwa 500.....

kwa mwanzo wa hii hiashara ni heri ps3, ili ujifunze biashara inaendaje na changamoto za machine na pad na wateja wako unawasoma....maana PS4 padi zake zinafika hadi 100 sasa ukipata changamoto ya pad kama hujajipanga unaona hailipi
Ushauri wangu chukua ps4 moja na ps3 moja. Na tv 2 za inch 32.
Gamers wengi wanapenda fifa 20 na kuendelea ambayo haipo kwenye ps3. Utakosa wateja wa fifa wengi.
 
Sikia.
*Ps4 chukua moja ni 650k. Chukua iliyochipiwa ndo inafaa kwa biashara.

*ps3 chukua 2 kwa 320k kwa kila moja.
*ps2 chukua 2 kwa 130k kwa kila moja.

* tv chukua 2 za inch 32 kwajili ya ps3 na moja ya inch 42 kwaajili ya ps4. Nenda kwa wapemba mbweni utapata inch 32 kwa 300k na inch 42 kwa 450k za mtumba. Za mtumba zitadumu muda mrefu sana. Nasisitiza usinunue za dukani ni hasara.
*chukua inch 22 kwaajili ya ps2. Vilevile za mtumba.

* nunua gaming pc used kwa 350k. Tafuta hawa jamaa wanaitwa camara huwa wanazo. Chukua na monitor ya inch 22 au tv yenye hdmi au vga port. Hii itakusaidia kuweka games zenye kuharibu pad mf. Mortal kombat x au xl au 11. Pad za pc ni ngumu na gharama yake ni 8k pad moja k.koo.

*ps4 na ps3 weka games za mpira na mission ambazo haziharibu pad. Pc tia game za ngumi na zenye kuharibu pad.

BEI

*Ps3 na ps4 mpira ni 500 kwa dakika 10
Ps2 mpira mechi 2 500 na ni dakika 10

*games zingn za mission ni dakika 15 kwa 500 kwa ps3 na ps4 na dakika 30 kwa ps2.

LOCATION*

tafuta sehemu yenye watu wengi hasa vijana na yenye usalama. Fremu ni kati ya 50k hadi 70k. Usiogope itakulipa tu.

* dumisha usafi na kama unamweka mtu basi mlipe kwa siku elf 5 mpaka elf 7 kwa siku kutegemea na mahesabu anayokuletea.

* fanya mwenyewe kama mwezi hivi ndo umpe kijana. Na uwe muda mwingi unapiga jicho maana wakizoea huwa wana tabia ya udokozi.

* biashara ikikubali weka cctv camera ni kama 450k kila kitu. Itasaidia usalama na pia kum monitor kijana.

*VIFAA VINGINE

*stabilizor ni muhimu sana kwaajili ya kulinda vifaa vyako.
*pads ni za kuchunga hasa za ps4 maana ndo kikwazo kikubwa cha biashara hii.
*kibali toka serikali za mtaa ni 20k tu na hakuna kenge atakaye kusumbua

●muda wa kufungua ni saa 3 asubuhi hadi saa 5 usiku. Ila siku za shule hakikisha madogo hawaingii chini ya saa 7 mchana.

● kwenye ps4 jaribu kuweka hata kijisofa itaongeza hadhi.

****** FAIDA ********

* ukifikia hayo juu jiandae kula kuanzia 20k hadi 30k kwa siku za kawaida na 40k kwa siku za weekend.

KUNA WATU WANAPENDA KUONGEA VITU WASIVYO VIJUA. KAMA HUJUI KITU NI BORA KUKAA KIMYA
Mungu akubariki
 
Wakumbushe pia, kutengeneza controller kwenye hitilafu ndogo kabisa ni kuanzia elfu5... Na inaenda hadi elfu 30.

Lerner hawajui kuwa analogue haihitaji nguvu, ikimeguka tu, kuibadili ni kipengele.

Ku-update game eg FIFA au GTA ni GB10 mpaka 20 inategemea na signal ya network.

Mwisho wa yote niwatakie mafanikio mema.
 
Wakumbushe pia, kutengeneza controller kwenye hitilafu ndogo kabisa ni kuanzia elfu5... Na inaenda hadi elfu 30.

Lerner hawajui kuwa analogue haihitaji nguvu, ikimeguka tu, kuibadili ni kipengele.

Ku-update game eg FIFA au GTA ni GB10 mpaka 20 inategemea na signal ya network.

Mwisho wa yote niwatakie mafanikio mema.
Ku update version ya game iliyo installed tayari au kufanya new installation ndio 10GB +?
 
Hii ya game pc ndo naona iko vizuri ulivyoichanganua sijawahi itumia hii embu nielekeze unaunganisha vipi pc mpka unacheza kwenyeTv.
Simple tu. Tv inakuwa kama monitor. Either uunganishe kwa VGA au hdmi.
Then pads za pc zina waya una connect via usb ports au via bluetooth kama pc yako inayo.

Kwa kuongezea tafuta kijisabufa hata cha 60k unganisha na pc kama source ya audio. Inanoga sana na inaleta bonge la vibe hasa kwenye magame ya ngumi
 
Wakumbushe pia, kutengeneza controller kwenye hitilafu ndogo kabisa ni kuanzia elfu5... Na inaenda hadi elfu 30.

Lerner hawajui kuwa analogue haihitaji nguvu, ikimeguka tu, kuibadili ni kipengele.

Ku-update game eg FIFA au GTA ni GB10 mpaka 20 inategemea na signal ya network.

Mwisho wa yote niwatakie mafanikio mema.
Yah kabisa
 
used inaanzia laki 550 hadi laki 7.....unaweza pata 450 ila chache sana na znakuwa fat.... Jaribu kutembea kupatana na facebook groups za used items utapata (ila umakini unahitajika)
Wakuu pes4 ni bei gan nataka kujaribu hii biashara
 
KUNA HII BIASHARA YA GAMES CENTRE kuna vijana wanapiga hela sana siku izi hasa izi PS4 iko hivi

Ps4 moja complete ni 550K mpk 650k Tv inch 40
Hapo una wastani wa kuingiza elfu 10 mpk elfu 20 kwa siku

Ukiwa nazo Ps4 mbili na Tv 2 una weza piga elfu 20 mpk 30 kwa siku

Je, ukiwa nazo Ps4 na Tv 4?
Hapo sawa sawa na mtaji wa kununua bodaboda 2 yaani m2.5 ambazo kwa siku ni elfu20
Lakini GAMES center mtaji wa m2.5 kwa siku ni elfu elfu 40

Unachotakiwa ni kujua tu eneo zuri la kuweka biashara yako wachezaji wengi na wanachuo vijana wa umri wa Kati
Generator muhimu kama sehemu ulipo kuna shida ya umeme
Kibali cha bodi ya game

Ukipata pata hivyo vitu unapiga hela tu kila siku elfu 40 kwa mtaji wa m2.5 na hakuna mkataba hapo hata miaka 20 unapiga tu hela
Mkuu ni wap ntapata bodaboda mbili kwa 2.5m zikiwa mpya ? Tuanzie hapo
 
Kutengeneza button moja tu ya pad za PS4 sio chini ya elfu 30.
CD ikisizingua tu, moja sio chini ya 120K OG, ku update mashine sio chini ya 30GBs za internet yenye speed kali.

Mkiongea haya mambo ongeeni kwenye uhalisia wake.

Nafanya hii biashara, usipokuwa makini, watu wavuta analogy joyride kama uoinde wa mshale, utajuta.... Zinameguka, spare elfu 60

Waswahili bwana amtaki watu waingie kwenye biashara zenu hakuna biashara isio kuwa na faida na kila biashara pia inachangamoto zake acheni mbwembwe gb 30 kwa voda 20k alafu utakuwa ana update kila siku kwani na cd atakuwa ananunua kila wiki mbona izo changamoto za kawaida je ukija kwenye biashara zetu za kusafirisha vitu vya magendo kutoka nchi jirani kama sukari,mafuta,chumvi,cement,mabati,nondo n.k,si ndo utaona dunia inataka kukushukia maana siku wakikuotea ndo utajua umuhimu wa vya vyama vingi.
 
Kaka Castr ninamaswali mawili kutokana na uzoefu wako......je faida kwa siku inarange ngapi kwa kijiwe chako?

vipi kwa mtu anaeanza na playstation 2, utamshauri achukue ps3 mbili au achukue ps 4 moja na ps 3 moja..?

Je ukilingamisha na biashara ambazo umewahi kufanya je unaona kuchezesha Play stations ni bora? .
 
Back
Top Bottom