Biashara ya Mbao na Miti: Fahamu Uendeshaji, Faida na Changamoto zake

Game Theory

Platinum Member
Sep 5, 2006
8,545
835

Jamani mimi nina chaneli ya high quality mbao (zilizokatwa na ambazo bado hazijakatwa) for export toka nchi jirani. Documents na leseni zote zipo. Nafikiria masoko ya Far East na Middle East. Hivyo UAE, SAUDIA, IRAN na kule Malaysia, Vietnam na kadhalika ndio nakutaka.

Je, kuna mtu anaweza kunipa links au ushauri?


MAULIZO YA WADAU WENGINE
Nasikia Biashara ya mbao au ukataji mbao na inalipa? Au kama mtu yeyote mwenye ufahamu wowote wa hii biashara naomba anisaidie.
Mwenye uelewa juu ya biashara ya mbao anisaidie. Nafikiria kufanya biashara hii, nataka kujua faida na changamoto zake, pia minimum capital ni kiasi gani?
Mie nataka kulima miti ya Mininga kwa ajiri ya mbao. Plz naombeni mwongozo. Je, miti hii itakua tayari kuvunwa baada ya muda gani? Na je, ni mikoa gani inafaa kwa kilimo hiki?


MICHANGO WA WADAU KUHUSU BIASHARA HII
 
@lonestar,

Soft wood au Hard wood

Ushauri: Tafuta market ya semi processed wood
 
Ukiweza kumtafuta tiger itakuwa vizuri, tiger ni member humu JF na amekuwa akihangaikia hiyo biashara. Na yeye anatoa mzigo toka nchi jirani na kuleta Bongo. Yeye ni mbao ngumu. Jaribu kumtafuta kwa pm na kama hapatikani nitakupa namba zake mobile phone.
 
Habari yako bwana, mimi niko China.

Huku kuna soko zuri sana la mbao, zote hardwood au softwood. Hii mimi nimekua nikijaribu kuifanya ila nikawa na matatizo ya supply chain nikashidhwa kuingia mikataba nao. Kama wewe uko serious, na uko tayari kufanya biashara basi wasiliana nami ili tuendelee na mazungumzo.
 
Nipatie majina ya mbao ulizo nazo, quality, quantity, contract duration na bei in US$ FOB Dar.
 
Inalipa aisee kamata hela nenda Iran leta mbao kama una mtaji byee kabisa. Go for it aisee.
 
Nasikia wizarani mpaka wanahonga Tshs 30m na bado hawapati vibali.
 
Mimi nigependa kuwahamasisha wanJF kupanda miti ya mbao hasa mbao nyeupe (pines and cypress). Miti hii inasitawi sana sehemu za nyanda za juu kusini.

Mimi nilianza kupanda miti hii kama miaka kumi iliyopita. Nimepanda miti mingi kila mwaka bila kukosa. Kwa sasa ninazo ekari nyingi za miti hii. Vile vile miaka ya karibuni nimepanda eucalyptus.

Wakati naanza kupanda miti mche mmoja nilikuwa nanunua kwa Shs 50 na kuupanda kwa Shs 20. Kwa vile napanda miti mingi (zaidi ya laki moja kwa mwaka) baadaye niliamua kuotesha miche mimi mwenyewe ili kupunguza gharama.

Gharama zaidi ya miche na upandaji ni barabara za moto kuzunguka msitu. Hata hivyo nilinunua ngómbe na kuwaweka kwenye shamba ili wale majani yanayozunguka msitu. Wamenisaidia sana.

Unaweza kupanda miti kidogo kidogo kila mwaka kutumia mshahara wako kama nilivyofanya mimi. Baada ya miaka kadhaa utakuwa na miti mingi na utaweza kuwa unauza miti au kupasua mbao kila mwaka.
 
Hiyo biashara Mufindi, Njombe na Makete inalipa sana. Kule Njombe vijijini kwa sasa mti mmoja wa kupasua mbao ukiuza jumla unakwenda kwa bei kati 10,000 mpaka 15,000 kutemegea na size yake na wateja wapo sio wakutafuta wanakufuata wenyewe, sasa ukiwa na miti 100,000 tayari milionea. Mwenyewe nimenunua mashamba huko kwaajili ya kupanda Pines .
 
Pia kuna mpango wa kimataifa unakuja. Utakuwa unalipwa hela kutokana na idadi ya miti unayotunza.

This has been started by international organisations, concerning with environment and global warming.

Nia kubwa ni Ku_promote upandaji na utunzaji wa mazingira. So ukiwa na shamba la miti, utakuwa unalipwa kila mwezi hela kadhaa.

Mradi umeanza nchi za ulaya na asia. Kwa africa bado. Sina uhakika kwa nn kwa africa, bado haujaja.
 

Kwa mti unaoweza kutoa angalau mbao tatu ndefu za 2" x6" hiyo bei ni ndogo sana ukilinganisha na atakachopata mnunuzi. Ubao mrefu wa 2x6 na uliopakwa dawa DSM una siyo chini ya Shs 17,000. Bei ya mti moja pale Mafinga (Sao Hill) ni zaidi ya Shs. 50 000. Tatizo kule vijijini watu wananunua vimiti vichanga sana.
 
Ninashukuru sana kwa hii topic, hata mimi nipo interested sana na kupanda miti na ni idea ya muda sasa, issue kwangu ni namna ya kuanza especially kupata shamba kwa ajili ya kupanda. Ningeomba kupata japo idea kama ninaweza kupata eneo huko njombe na kwingineko ukizingatia mimi ninaishi dar. Na price inakuwaje, pia gharama za miche kwa sasa ni kiasi gani na kuotesha plus kutunza.

Please please mwenye data ninaomba.
 

Wasiliana na Malila, ni memba humu, mtafute
All the best mkuu.
 
Kuna miti inaitwa mitiki,hii vipi kupanda mpaka kuvuna inachukua miaka mingapi? Je, hizo pines na eucalyptus nikipanda kwenye heka 10 ninunue miche mingapi? Au unaweza kunisaidia kupanda miche ya hekari kumi?
 
Halafu mkubwa KVM umelete uzi mzuri ila mwaga maujuziyako zaidi kwenye hii habari ya miti ili na wengine tupate nguvu au mwamko,pengine tukatoka kiaina. Mfano miti hiyo uliyoitaja inachukua muda gani kutunzampaka kuvuna. Je, yaweza kutoa mbao ngapi n.k
 

Subiri kidogo nitakupa data/hadithi ya upandaji miti.
 

Kazi ya kupanda miti inachukua muda mrefu kidogo. Hesabia siyo chini ya miaka kumi na mbili hivi toka upande ndiyo unaanza kuvuna. Unatakiwa kwenda nayo taratibu. Kila mwaka panda miti kiasi fulani ili utakapoanza kuvuna uendelee kuvuna kila mwaka na kupanda ulikovuna.

Kuhusu gharama za kupanda zinatofautiana kufuatana na kijiji. Kijijini kwangu kwa sasa nadhani ni aghali kidogo kwani ni watu wengi wanopanda miti. Muamko umekuwa mkubwa sana. Ni mimi niliwastua baada ya kuona kazi niliyokuwa naifanya. Kwa sasa nadhani mche mmoja upo chini ya Sh 100 nakuupanda ni Shs 30. Mimi nilianza kwa kununua mche Shs 30 na kupanda Shs 20. Hiyo ilikuwa miaka kumi iliyopita lakini leo mti huo naweza kuuza siyo chini ya Shs 10,000 mpaka 20,000.

Kiasi cha mbao utakazopata inategemea na aina ya miti, matunzo,umri wa mti, na ulipanda kwa nafasi gani (distance between trees). Mazungumzo yangu hapa yanahusu zaidi miti aina ya Pines. Kwa kawaida tegemea kupata kati ya mbao tano za 2x6 kama ukiharakisha kuvuna lakini mtihuo kama umekomaa (miaka 25 hivi) umetunzwa vizuri na ulipandwa kwa nafasi nzuri unaweza kutoa hadi mbao 30. Wengi wetu ikifika miaka 12 tunavuna, na kinachopatikana siyo haba lakini nadhani ni nzuri zaidi kuvuna kuanzia miaka 15 au 16 hivi kwani utakuwa na uhakika wa kupata pingili siyo chini ya mbili na mbao ndefu za 2x6 angalau 6 nakwenda juu . Ubao mmoja wa 2x6 uliopakwa dawa hapo DSM unauzwa siyo chini ya Shs 17,000 na kule Mafinga kiwandani bila dawa ni Shs 10,000 bila kupungua senti tano.

Maeneo Mazuri za Kupanda Miti

Miti ninayozungumzia hapa ni Pines, Cypress na Eucalyptus. Miti hii inaota na kustawi vizuri sana nyanda za juu kusini. Ukitaka kupanda miti nakushauri uende Njombe halafu kutoka hapo fuata barabara nne: Kwenda Makete, Kwenda Ludewa, Kwenda Songea na Kwenda Lupembe. Utakapopita sehemu hizo zote utaoona maeneo mazuri sana ya kupanda miti. Kupata eneo unaweza kununua kijijini au kwa wananchi.

Nakushauri usikubali kukodishiwa. Bei inategemea na eneo. Kuna sehemu upandaji wa miti umeshika kasi sana kwa hiyo maeneo hayo ardhi itakuwa aghali kidogo japokuwa ndiyo sehemu nzuri kwani wananchi wake watakuwa na uzoefu wa upandaji miti na hutakuwa peke yako kwenye kuhangaika kudhibiti moto.

Matunzo ya Miti

Baada ya kupanda unaweza kufyekelea mara moja au mbili mpaka mti ukomae. Pruning nayo unaweza kufanya mara mbili. Njia za kuzuia moto (Fire Lines) unatakiwa utengeneze kila mwaka bila kukosa. Kwa vile mimi nimepanda eneo kubwa basi niliamua kununua ng'ombe ambao wananisaidia kupunguza majani pembezoni mwa shamba.

Ili uweze kumudu vizuri upandaji wa miti mingi, hasa kama utapanda kila mwaka, na nakushauri upande kila mwaka kwa kweli inabidi uajiri kijana, kama siyo mwanzoni basi baada ya miaka kadhaa kupita. Yeye ndiye atakayekuwa ndiyo wa kwanza kujua shamba linakabiliwa na matatizo gani na namna ya kuyatatua haraka iwezekanavyo. Mimi shamba langu ni kubwa (siyo chini ya ekari 1500) nimeajiri vijana watatu. Mmoja wao anaishi ndani ya shamba na ndiye anayetunza ng'ombe. Pamoja na ukubwa wa shamba lakini nimelipanda polepole kwa miaka kama kumi hivi.

Nimeamua kuambatanisha picha chache za mradi wangu nashindwa kuleta nyingi zaidi kwa vile zinatumia muda mrefu mno kuload.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…