George786
Member
- Feb 8, 2019
- 53
- 95
WEKEZA KWENYE HAYA KAMA UNATAKA KUFANIKIWA KATIKA BIASHARA YA MADINI
Kuna vimigodi vidogo vidogo lakini changamoto yake unapata mzigo mchache. Kwa mfano, kwa siku ukikusanya 4gm-10! Ni hasara.
Huko Geita mie machocho niliyopita atleast Kanegele hakukua na msongamano sana na purity kule iko juu, plus ntambalale.
Ukweli kama unataka kutoka wekeza kwenye
1. Plant (hapa kama unaaminiana na mtu ingia naye share) weka mkemia mzuri na mzoefu..hapa utapata kipato cha maana..hakikisha na wewe unakuwepo, sio unakaa Dar plant iko Mwambomba utapigwa had ushangae!
2. Nunua Crusher fukuzia kifusi kuza kifusi uza au peleka plant
3. Kuwa na sonara yako .means uwe na jiko lako la kuchomea dhahabu
4. Nunua vifusi (sasa hapa itakubid kuwa na urafiki na mwenye plant naye unamgea %..ukinunua vifusi vizuri una hakika wakuwa na faida ya 5-7m every month ukikatika sana ni 3-5m (sasa ukiwa na plant yako next year tutakuita don bila wewe kupenda)
All in all itakupasa kukaa migodini kusoma Michezo kwanza! Kujua magumashi yanatokeaje!
La mwisho haya mamigodi yana uccm sana walotoka sana kifedha lazima CCM iwahusu ia sivyo utasumbuliwa sana na TRA, polisi Weka urafiki na polisi wa migodini, usijioneshe mpinzani in any means!
Kifupi sina hakika kama kuna hela tamu kama ya dhahabu😄😄! Ukiingia ukapata hutoki! So ni kuwa smart uje utafute mtaji!
Na kuwa na pant yako na kila kitu ulichoelezea hapa ili baada ya muda mfupi utoke inahitaji uwe na mtaji wa bei gani mkuu?
Sent from my iPad using JamiiForums