Biashara ya Madini ya Dhahabu: Fahamu Uwekezaji Wake, Changamoto na Faida

Kuna sehemu umeeleza kuuziwa madini feki. Kwetu wanapima kwa viroba (mifuko ya 25k) labda unauzwa kwa 200k@ halafu linakuja tajiri moja feki (wakikuona mgeni na una wenge wanakuchezea) huyu tajiri feki atajifanya anataka kununua mawe yote. Tuseme kuna viroba 100x200000=20,000,000. Mara nyingi kama mawe yana sample sana wtu hugombania (kota wenye mitaji midogo). Hapo bei aidha itapanda au mtanunua kwa kukomoana. Unanunua viroba 10. Kimbembe ni kwenye kuosha. Umetoa 2m halafu unapata 100000 (iliwahi kunitokea mara mbili sitakaa nisahau na ndio ilikuwa mwisho kununua mawe). Utabaki na 3m kuna siku utapata ila faida haiwi kubwa. Niambie itachukua muda gani kukuweka chini

Sent using Jamii Forums mobile ap

Mie naonaga kununua mawe then unapgia kupata faida ndo risk kubwa zaidi! Nunua mawe kasagie kwa jirani osha kwa mwalo wako ukuze kifusi hata km utachukua miez 6! kifusi ndo kinakubeba!

Au unganeni mnunue kalasha msagie kwwnu na kuosha kwenu, ila migodini kupoteza hizo millions kugusa tu! Ila kama unakuza kfusi hela yako utaikuta huko
 
Mie naonaga kununua mawe then unapgia kupata faida ndo risk kubwa zaidi!..nunua mawe kasagie kwa jirani osha kwa mwalo wako ukuze kifusi hata km utachukua miez 6!.kifusi ndo kinakubeba! Au unganeni mnunue kalasha msagie kwwnu na kuosha kwenu!...ila migodini kupoteza hizo millions kugusa tu! Ila kama unakuza kfusi hela yako utaikuta huko
Kabisa. Na hapa pia inabidi uwe na ujuzi wa kujua shimo lipi lina dhahabu nzuri. Mimi kilichonikost ni ubora wa dhahabu. Hilo eneo lilikuwa na dhahabu ya ajabu.

Unaosha na kukamua dhahabu kubwa mno (siku ya kwanza nilitaka kujilaumu kwamn nimenunua mawe kidogo) ukiichoma inapungua uzito mno. Kesho yake tulikutana wote tulionunua na stori ikawa the same.
 
Dah uzi mzuri huu hapo na kauzoefu kanahitajika hapa naona kwenye hii sekta aisee

Sent using Jamii Forums mobile app
Afadhali huyu ameomba ushauri hapa jukwaani. Mwaka 2016 nilifuatwa inbox na jamaa mmoja baada ya kuchangia kwenye uzi humu jf. Yule jamaa mpaka leo nashindwa kuelewa lengo lake. Alinisumbua sana mpaka nikaanza kumpa ushirikiano.

Mara nina mtaji wa 20m USD nahitaji kuwekeza, tafuta eneo tununue, fuatilia vibali na mambo meeeeengi. Na wakati huo nilikuwa hovyo nikawa nahangaika nikijua hapa mambo si muda yatajipa.

Baada ya kuhangaika nae mwisho nilianza kuwa na mashaka naye. Mpaka leo siwezi kumsaidia mtu inbox mpaka nione kuna umuhimu. Kwanza nimejifunza ukitoa elimu jukwaani unawasaidia wengi.

Shukurani sana kwa Wangari Maathai kwa elimu unayoitoa hapa.
 
Wadau Naomba kujua. Napenda sana kujifunza hasa Kule wanakochimba na jinsi hii biashara invyofanyika kuanzia uchimbaji hadi inapofika kwa mnunuzi.

Kwa siye ambaye hatuna connection ya kufahamu watu waliopo kwenye madini Tunafanyajee angalau ufike Ayo maeneo na kuweza kuungana na watu wanakochimba na kuanza kujifunza.

Naombeni maujuzi wadau nifanyajee Ili niwezee jitupaaa ayo maeneo.

Nafahamu migodi mingi kwa majina

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Afadhali huyu ameomba ushauri hapa jukwaani. Mwaka 2016 nilifuatwa inbox na jamaa mmoja baada ya kuchangia kwenye uzi humu jf. Yule jamaa mpaka leo nashindwa kuelewa lengo lake. Alinisumbua sana mpaka nikaanza kumpa ushirikiano.

Mara nina mtaji wa 20m USD nahitaji kuwekeza, tafuta eneo tununue, fuatilia vibali na mambo meeeeengi. Na wakati huo nilikuwa hovyo nikawa nahangaika nikijua hapa mambo si muda yatajipa.

Baada ya kuhangaika nae mwisho nilianza kuwa na mashaka naye. Mpaka leo siwezi kumsaidia mtu inbox mpaka nione kuna umuhimu. Kwanza nimejifunza ukitoa elimu jukwaani unawasaidia wengi.

Shukurani sana kwa Wangari Maathai kwa elimu unayoitoa hapa.

20mil usd unajua lkn ni zaidi ya Tsh. Bil 45 mzee baba?
 
Kiukweli kule ujitoe tu ufahamu kama huna mtaji! Kazi zipo ila za kutumia nguvu..esp kuosha unga...kuchenjua dhahabu(hapa lazima ujifunze kwwli kweli) na ni ngumu mtu kukupa tope lake umchenjulie..wanaiba sana hapa kwa kuchenjua .
Kazi nazoona wanafanya zaidi kina kaka wasio na .mtaji ni kupiga moko(kuzamaa huko chini kupiga mwamba) ni kazk ngumu kiukweli...ila ukibahatika ukatoka na kajiwe uongo! Mistake za kule ni zile zile .kwasababu kazi ni ngumu bas mtu akipata hela anatumia hovyo sana!

Kuosha unga ni 2000@ mzunguko mmoja...mzunguko mmoja unaweza chukua ndoo zile ndogo 5-8!inategemeana na ukubwa wa ile machine(crusher )na inaweza zidi pia kidg..so unga ni mwingi kiukwel..sasa vibarua ni hela ya kula tu..mayb uombe uoperator na mkubaliane mlipane mkishauza kifusi...hapo makubaliano ni yenu wewe na mwajiri wako! Bt haizid 500k had kaz kufunga!

Mie nachoamini pia ni bahati!.kuna dogo ndugu yangu alifika kule mwaka 2017! Akitokea chuo ...alifika hana kitu..akaomba kwa mzee 200k! Leo hii kila miezi miwili ana faida ya kuanzia 6-8m!so alianza na , 200k akinunua mawe ya bei ya chini(fello)..akapanda had kumiliki crusher! Means akianza leo 14th kazi anafunga 14july anauza kifusi yy hana mpango na plant kbs.faida ndo hizo 6-8m! Ikigoma sana 4m.. Kule naona wasomi kama wanatoka mapema eti!...mradi uwe serious na usmart fulani!

Na ukitaka kufanikiwa mapema nenda kwenye mgodi ulolipuka ...sio mgodi uliodormant!..!
Wewe jamaa mzoefu sana.

Umetufumbua macho kwenye hiyo biashara ya madini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee baba niliona kimya humu Jukwaani nikajua Mai Mai walishafanya yao,so itabidi tuji-organise tutume kikosi kije kukukomboa arifu hahah.
Hahahaha, Mai Mai watoto wadogo wale uchawi unawadanganya , ila huku bana dah kuna bro kazingua juzi, karudisha mpira kwa kipa uanze upya, nilidhani imefika JF humu.

Kule mashariki ni kichapo tu, ADF na FARDC

Mahakamani ni VK anapambana na kesi yake.
 
Hahahaha, Mai Mai watoto wadogo wale uchawi unawadanganya , ila huku bana dah kuna bro kazingua juzi, karudisha mpira kwa kipa uanze upya , nilidhani imefika JF humu

Kule mashariki ni kichapo tu ,ADF na FARDC

Mahakamani ni VK anapambana na kesi yake

Aisee huyo mwana sijamsikia aisee, ilikua ni misala hii hii ya dizaini za kina mai mai au ni kwa msala mwingine?

FARDC naona kimedani wanaenda wanaimarika vyema,pongezi kwa legendary Felix.

VK vs FT watatoana roho.
 
Aisee huyo mwana sijamsikia aisee,ilikua ni misala hii hii ya dizaini za kina mai mai au ni kwa msala mwingine?

FARDC naona kimedani wanaenda wanaimarika vyema,pongezi kwa legendary Felix.

VK vs FT watatoana roho.
Hahahaha ,kuna suala moja lishazungumzwa sana humu OK tuache hilo

FARDC sasa wana hali ya kupambana, ili nililijua mapema tu, Felix kule mashariki anajitahidi.

VK kasimama mahakamani anakuambia yote aliyofanya kafanya km kiongozi na maelekezo ya Boss
 
Hahahaha ,kuna suala moja lishazungumzwa sana humu OK tuache hilo

FARDC sasa wana hali ya kupambana ,ili nililijua mapema tu ,Felix kule mashariki anajitahidi

VK kasimama mahakamani anakuambia yote aliyofanya kafanya km kiongozi na maelekezo ya Boss

Hio VK Vs FT ni kama ya Laigwanani vs Msoga, kwenye kikao cha chama Laigwanani alichoka kuitwa fisadi ikabidi apandishe Jazba aulize hivi mwenyekiti ni kitu gani ambacho nilikifanya hukijui au ambacho hukunituma? Ikabidi wazee wa busara wauingilie kati, hahah

Ngoja tuwaachie uzi wadau wasije kutumaindi hapa hahah.
 
Hio VK Vs FT ni kama ya Laigwanani vs Msoga,kwny kikao cha chama Laigwanani alichoka kuitwa fisadi ikabidi apandishe Jazba aulize hivi mwenyekiti ni kitu gani ambacho nilikifanya hukijui au ambacho hukunituma?Ikabidi wazee wa busara wauingilie kati,hahah

Ngoja tuwaachie uzi wadau wasije kutumaindi hapa hahah.
Hahahaha, kweli tuwaachie uzi wao Mkuu.
 
20mil usd unajua lkn ni zaidi ya Tsh. Bil 45 mzee baba?
Ulishawahi kupitiq kipindi kigumu mpaka ukaamua kufanya lolote lenye dalili ya kutoboa? Basi ndio ilikuwa wakati huo. Kwanza jamaa mawasiliano yetu yalikuwa kwa WhatsApp maana muda mwingi ilikuwa "niko England mara niko Marekani hapa, mara ya mwisho aliniambia yuko South Africa" wakati ule wageni wanachinjw na kuchomwa moto, nikahisi jamaa amekufa vile.

Alikuwa anategea siko online (kwa kuangalia last seen) muda mrefu anatuma meseji kuwa yuko bongo anataka tuonane. Kilichonisanua ni siku nimemwambia kuna eneo limepatikana aje na wataalam walifanyie upembuzi yakinifu (tathmini na hii ni wakati usd20m ziko za moto😁😁) akaanza kunichenga.

Akageukia kwenye rubby na green tomalin. Nikajua huyu mzinguaji haswaa. Kuna wengine humu jf walifahamu hii skendo na ndio nikaapa inbox ni kwa watu maalumu tu.
 
MTIRIRIKO WA NAMNA UNAVYOWEZA KUJIHUSISHA NA BIASHARA HII

Hii biashara inakuhitaji sana mwenyewe uwepo eneo la tukio na uwe na akili nzuri kidogo ili kurun show na kutoboa.
Ni biashara nzuri kama kichwa chako ni kizuri na kweli una kiu ya mafanikio.

Kuna namna tofauti tofauti ya kujihusisha na hii biashara kwa mzoefu na kwa ambaye sio mzoefu.

Unaweza kufuata huu mtiririko kadiri uonavyoona inafaa.
  • Jipe muda kwa kuzungukia maeneo kadhaa ya uchimbaji ukiangalia nini kinachofanyika na namna gani watu wanaishi.
  • Kwenye mzunguko wako jipe muda sana kwenye machimbo mapya ya dhahabu.
  • Jaribu kuunda urafiki na watu wawili watatu watatu wanaofanya vitu vifuatavyo, mchimbaji, muuzaji, msagaji, mama ntilie, wenye mabaa na grocery ( tembelea hayo maeneo ujifunze kitu.)
  • Kwa wewe unayeanza sio jambo jema kuanza kununua na kuuza dhahabu kabla hujajua abcd za dhahabu - NI HATARI.
  • Ukiwa kwenye harakati za kusoma mazingira jiridhishe na biashara zote zisizo za dhahabu zinazofanyika na ambazo unaweza kuzifanya ili ukaishi mazingira hayo wakati unajifunza game.( kukodisha pump, blower, kuuza miti, mama ntilie, kuuza maji, grocery nk.
  • Ukipata kauzoefu kidogo Tafuta karasha la kusaga mawe used lenye hali nzuri kwa 5mil (jipya size ya kati ni 8.5 - 9 Mil).
  • Ukiwa na karasha fungua sehemu ya kusagia na kuosha (Mwalo) unapaswa kuwa na Karasha, mercury, mizani, magunia, maturubai ( roughly uwe na kama 10mil kibisha unaweza kuanza na 3mil nyingine iwe pembeni na total ni 13mil).
  • Wakati wa kusagisha na kuosha huwa unatarget vitu viwili ( Kuwa na rundo la mchanga hakikisha unasaga mawe yanayosoma vizuri na ununuzi wa dhahabu).
  • Hapo sasa ukiwa na mwalo na watu wanaoshea kwako unaweza kununua dhahabu kulingana na mzunguko lakini ukikomaa per day unaweza kulaza faida ya 100K +.
  • Ndani ya miezi sita mpaka mwaka kulingana na speed na usomaji wa rundo(kifusi) unaweza kuuza hela nyingi sana na ukatengeneza faida ambayo sasa ndio itakupa kiburi na kukubatiza kuwa miner sasa.
  • Mtaji ukikua sasa na bila shaka utakuwa unaijua network na dhahabu unaijua unaweza kuamua mwenyewe wakati unaendelea na karasha what is the next round..( Uanze uchimbaji [hii ni kamari na inahitaji ujasiri, hela na uwe mshirikina}, Ujenge plant kama mtaji umekua vizuri.
  • Binafsi sishauri sana kuingia kwenye uchimbaji unless uwe na muscles uchimbe kisasa kwa maana ya exploration na drilling ya kisasa otherwise hapo kuna mitihani sana na uamue kuikabili ( I know it and I'm doing this is reality, African magic is highly working here asikudanye mtu).
  • Kama uko vizuri na una muscles unaweza kujenga plant au ukanunua macompressor ukaanza kufanya drilling and blast kwa kukodisha.
  • Plant unaweza kuozesha mzigo wako mwenyewe unaosaga ukifikia kifusi cha kutosha na kukodisha pia wakati mwingine.
  • Unaweza usifanye shughuli yeyote ukamiliki plant ukawa unakodisha watu wanaozesha (usijiingize kwenye dhambi hapa kwa kuwapiga watu dhahabu plant kiujanja si jambo zuri kwa mpambanaji)
  • Gharama ya plant na kila kitu roughly 40mil to 50 mil.
  • Narudia tena, usifanye biashara ya dhahabu kabla hujaijua dhahabu NI HATARI, Usiwe na tamaa utatamanishwa utaingia king watu watakupiga, Usiwe na haraka jiwekee focus yako mdogomdogo utatoboa.

Karibu mavumbini tulicheze disco, kuwa mvumilivu changamoto hazikwepeki ni kupambana nazo kadili zinavyokuja.
Usisononeke na maisha mazuri ya wenzio, Pambana usiku mchana, jua mvua utafika hizo level.
No easy man, work hard, God will put the bless. Heshimu watu.
 
Back
Top Bottom