Biashara ya Madini ya Dhahabu: Fahamu Uwekezaji Wake, Changamoto na Faida

Vilipuzi na compressor mara nyingi huwa vinaenda sambamba. Mfano kuchoronga mwamba tundu moja bei yake average ni tsh 10,000. Ukimuwekea mtu na mlipuko ni 15,000. Hvyo kuchoronga na kulipua tundu moja inakuwa 25,000. Ila kumbuka mtu wako anayelipua lazma awe na certificate. Thats y sikushauri kuuza milipuko kama milipuko usije ukashikana mashati na mamlaka.

Hii kuchoronga mwamba kwa kutumia compressor kwa siku unaweza choronga tundu ngapi wastani?
 
Hii kuchoronga mwamba kwa kutumia compressor kwa siku unaweza choronga tundu ngapi wastani?
Inategemea na urefu wa shimo ie ng'anda ngapi au ft ngapi
Pia inategemea na compressor inatoa upepo kiasi gani

Inategemea na ubukwa wa digger Y24 iko kawaida, Y 18 iko vizuri ila wengi hawaipendi sababu ni nzito

Inategemea uzoefu wa driller

Inategemea na ugumu wa mwamba pia


Ila sehemu nyingi Tundu 400 inaweza chukua masaa 12 au zaidi

Hapo ni mafuta, BIT, Oil, Drillers

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi ukiwa mnunuzi tu unaeza peleka kuuza sokoni bila certificate?
 
Kuna sehemu umeeleza kuuziwa madini feki. Kwetu wanapima kwa viroba (mifuko ya 25k) labda unauzwa kwa 200k@ halafu linakuja tajiri moja feki (wakikuona mgeni na una wenge wanakuchezea) huyu tajiri feki atajifanya anataka kununua mawe yote.

Tuseme kuna viroba 100x200000=20,000,000. Mara nyingi kama mawe yana sample sana wtu hugombania (kota wenye mitaji midogo). Hapo bei aidha itapanda au mtanunua kwa kukomoana. Unanunua viroba 10.

Kimbembe ni kwenye kuosha. Umetoa 2m halafu unapata 100000 (iliwahi kunitokea mara mbili sitakaa nisahau na ndio ilikuwa mwisho kununua mawe) Utabaki na 3m kuna siku utapata ila faida haiwi kubwa. Niambie itachukua muda gani kukuweka chini

Sent using Jamii Forums mobile app
,,, Mkuu nahitaji shule zaidi kutoka kwako
 
Back
Top Bottom