Biashara ya mabasi ya mwendokasi (UDART) ikadhibiwe Sekta Binafsi kabla haijafia mikononi mwa Serikali na kuitia aibu kubwa

Toka tupate uhuru ndio PM wa hovyo kuwahi kutokea,yupo tuko kazi yake kuvaa suti na kuzurura.
 
Nilikuwa siamini kwamba kwenye kila analogusa Magufuli huwa ana haribu Ila kwenye Mwendokasi ndo sehemu niliyokuja kuamini kwa Mara ya kwanza!

Kwanza inabidi wote tujiulize mwendokasi ilianzia wapi?

Mradi wa mabasi ya mwendokasi ukianzishwa na kuasisiwa na Rais wa Awamu ya nne. Kwa Jinsi mradi ulivyokuwa umeandaliwa ulitakiwa kusimamiwa na kampuni binafsi na tangu mwanzo ulisimamiwa kwenye mfumo huo. Mradi huu ulikuwa chini ya Kampuni na Kisena na wakati unaanza kila kitu kilikuwa kinaendeshwa katika dunia ya kisasa. Ticket zilikatwa kielectronic na watu waliweka hadi kuwa na kadi ya kutumia mwezi mzima.

Alipokuja Magufuli kwanza alianza ku deal na kisena kwa sababu kisena hakuwa kwenye kundi la watu waliomuunga mkono kwenye uchaguzi wa mwaka 2015. Alimtesa kisena kumpa kesi za uhujumu uchumi na mkewe na baadae kumnyang’anya mradi na hatimaye akaondoa utaratibu wote mzuri uliokuwa umewekwa kwa ajiri ya kuendesha mradi.

Matokeo yake akawapa wanajeshi, na hapo ndo Tatizo lilipoanza. Mradi ulianza kuendeshwa kwa tabia za kiswahili na watu wakaanza kukata ticket kama daladala.

Mradi huu hadi kufikia sasa ulitakiwa uwe umeshaanza kujiendesha kwa faida Ila kwa roho mbaya ya magufuli na tabia zake za kuchukia matajiri ndo amefanya mradi ule uwe kituko na usifike popote.

Polee kisena. Buriani Mwendokasi.
Kisena mwenyewe huo mradi alikuwa anauendesha ovyo tu

Ova
 
Kuna vibanda vya kukatia tiketi kule Kimara - Mbezi vimefunikwa na majani mwaka sasa. Havina Dirisha, AC system na havikaliki badala yake Maafisa wa tiketi wanatumia vibanda vya mbao na nyasi kuanzia asubuhi hadi 12 noon.

Baada ya hapo hakuna tena tiketi hadi kesho yake. Waliacha kutumia e-cards miaka minne iliyopita sasa ni tiketi za kuprinti na sijui zinaprintiwa wapi na nani. Acha PM ashangae tu, huenda akachukua hatua. MAAJABU YA MWENDO KASI!
Hio miaka miwili toka wameacha kutumia tiketi za electronic PM hakuwa na taarifa?!!!

Hii nchi maigizo ni mengi,viongozi wanajua kucheza movies kuzidi hadi wahindi!! Serikali ina taarifa zote za kila siku kuhusu mwenendo wa huo mradi,hayo mengine ya kufanya ziara za kustukiza ni janja tu ya nyani!!
Tuachane na huo mradi ni mradi gani wa huduma unao simamiwa na serikali hizi za CCM unao onyesha ufanisi!!
 
Tuache siasa za changa lamacho, Serikali ya JPM ndiyo imeua utendaji wa UDART.

Barabara za UDART kweli ni mali ya serikali lakini mradi wa mabasi mwendo kasi ulikuwa toka mwanzo ni mradi binafsi(private investment) uliowekezwa na mnganzania, Nd Kisenha.

Serikali ilifanya kila njia kumnyima pumzi mwekezaji huyu wa UDART. Alipoagiza mabasi alinyimwa katakata kuyatoa bandarini mpaka hela yote ipatikane Kulipa Kodi. Huku ni kukosa ushirikiano kwa muwekezaji, ambapo wale wa kigeni hupewa Tax Holiday au Mkataba maalum kwa malipo ya kodi kubwa.

Hii ingewezesha huduma iendelee, biashara iendelee na kodi ilipwe. Hili ni kosa, maana serikali haikuwa na msaada wowote kwa muwekezaji.

Pili, tunasikia tetesi kuwa sasa UDART ni mali ya Serikali maana baada ya Nd Kusenha kufunguliwa madai ya Uhujumu uchumi, kwawaida ya modus operadi ya Awamu ya 5kwa wafanyabiashara, serikali imejimilikisha uendeshaji.

Serikali zote toka Awamu ya kwanza hadi nafikiri Mwinyi (miaka zaidi ya33) mfupa wa DMT (Da es salaam Motor Transport) na UDA(Usafiri Dar es Salaam), ziliwashinda. Sasa sijui Awamu ya 5 ndio wangeweza Kuendesha UDART?

Mbaya zaidi serikali inaua moyo wa wazalendo kuingia miradi mikubwa kiuwekezaji, kinyume cha wanachoongea majukwaani.

Ziara ya Waziri Mkuu Majaliwa kwa UDART kweli sioni mantiki yake zaidi ya kusema Serikali imachukua na kuanza mradi huu on a false start.

Sana sana ni kujikosha kwa wananchi kwa failures za serikali yenyewe, kusaidia wazalendo kuwekeza nchini mwao.
Kisena nae ni mbabaishaji tu,huwezi kuleta mabasi utegemee tax holiday!!

Mabenki yako chungu mzima,alishindwa kwenda benki kwa dhamana ya hayo mabasi,achukue mkopo alipe kodi ya serikali!!

Lengo lake alitaka aingize mabasi hayo kinyemela kwa makubaliano na serikali kuwa atalipa pindi yakianza kufanya kazi!!ili baadae aje na sound za kwamba hapati faida na vieelelezo uchwara!!ili asilipe kodi!! Kisena ni aina ya wawekezaji uchwara.
 
Kitu usichokijua ni kuwa huo mradi unaendeshwa na sekta binafsi.

Tatizo ni jinsi hiyo sekta binafsi ilivyopatikana.

Simon group ni scam
Halafu sekta binafsi yenyewe ikapewa na mpaka mtaji na serikali,ikapewa route ambazo gari zingine aziendi na bado wameshindwa,kuna kampuni nyingi zinaendesha miradi kama ule nje ya africa,wawape ule mradi kwani washakua na uzoefu wa biashara ya usafiri,lakini sio hao wezi kina kisena na riz moko
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom