UDART Inaingiza Faida Kuliko ATCL na TRC Holdings

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
3,214
3,587
Ukiondoa gharama zote za uendeshaji (operations) njia ya Kimara Gerezani pekee inaingiza faida ya 1bl kwa mwezi kipindi kile cha awamu ya 5.

Bado Morocco na Feri na feeders za Muhimbili, Kibaha, Mbezi Beach na Mloganzila.

Inakisiwa Mbagala na Gongolamboto zikikamilika zitaingiza faida maradufu zaidi ya hiyo 1bl ya Kimara Gerezani.

Abiria ni wengi kuliko uwezo wa mabasi yaliyopo kuwahudumia.

Takriban nusu ya mabasi ya UDART yamepaki kwa ubovu ambao matengenezo yanalazimu yapakiwe kwenye meli kupelekwa Ulaya na kurudishwa kama ndege zinavyofanyiwa matengenezo Ulaya. UDART haina vipuri wala gereji Afrika.

Kama mabasi yote yangefanya kazi kwa uwezo wao na zuio la daladala kuipa UDART ukiritimba wa soko kwa baadhi ya njia, huenda UDART ingeweza kutanua huduma zake kwenye makao makuu ya nchi Dodoma ambako nako tayari kuna idadi kubwa ya watu kuzidi Mwanza hivi sasa ambako nako UDART ingetanua ndoto zake kufika jiji hilo la mawe.

Ukosefu wa uweledi kwenye fedha na biashara kunaigharimu UDART na kufanya kampuni kuingia kwenye orodhanyeusi (Blacklist) ya taasisi zinazokabiliana na udanganyifu (dishonesty).

Hii inafanya wengi waamini kwamba ilikuwa ni mapema sana sana sana kwa JMT kuwa na mradi kama huu pasipo kujiandaa na utaalam wa kuuendesha.

Kadhia hii ishughulikiwe mapema isije kutambuka na kuiathiri miradi ya kimkakati mingine ya SGR na JNHPP.

Itakuwa aibu kuu ya vizazi na vizazi vya Tz duniani kwamba tuna jumla ya megawati 4015 toka vyanzo vyote vya nchi lakini tuna shida ya umeme au tuna umeme ghali unaofukuza wawekezaji, pia tuna SGR, MGR na CGR lakini tunashindwa kusafirisha mizigo ya Maziwa Makuu, SADC na EAC.

Nadhani watendaji wa miradi hii ya SGR na JNHPP wajiandae kisaikolojia. Vinginevyo wabadilishwe kwa maana pia huwezi wewe ukajenga na wewe huyo huyo ukaendesha, lazima utakosa uwazi.

Ukiachia nafasi ukapewa dhamana nyingine tofauti ndipo tutakapoweza kubaini mapungufu yako na kuyarekebisha kwa maslahi mapana ya taifa, lakini uking'ang'ania kubaki lazima utafunika mapungufu yako na huenda kama taifa tukaingia kwenye sintojuwa.

Nchi hii ikisimamia vizuri miradi mikakati ya Reli na Bandari (au hata Ndege na Meli pia (yaani logistics sector)) inaweza kujiendesha bila kugusa madini, wanyama, samaki, miti, utalii nk.
 
Shida kubwa ya hii nchi ni ubovu wa mifumo hasa kwenye miradi ya serikali. Kuna mazingira yanatengenezwa ambayo yanazaa ukiritimba,serikali nyingi za Africa na Tz ikiwemo ukiritimba ni mwingi sana. Jambo la kufanyiwa maamuzi ndani ya lisaa au dakika huku kwetu litachukua vikao vitatu hadi vinne ili watu walipane posho.
Uongozi wa juu ndo kasheshe tupu,kila aliyepo juu anawaza kuiba tu hiyo inawafanya na hawa wachini kuwaza hivyo muda wote.
Unaweza kujiuliza kwanini sisi hatukubali kwenda sambamba na kukua kwa Technolojia?Sababu ni kwamba Tech inaziba mianya ya wizi kwa wakubwa.
 
Bandiko makini sana.
 
Nchi hii ikisimamia vizuri miradi mikakati ya Reli na Bandari (au hata Ndege na Meli pia (yaani logistics sector)) inaweza kujiendesha bila kugusa madini, wanyama, samaki, miti, utalii nk.
 
Back
Top Bottom