Waziri Mchengerwa Kuhusu Udart kuwa hata na aibu

themagnificient

JF-Expert Member
Dec 13, 2016
988
3,318
Moderator naomba msiuunganishe huu uzi nna ujumbe wake Binafsi

Mheshimiwa Waziri kuwa hata na aibu maana nimeskia unawaambia wananchi kuwa hadi Septemba shida ya mwendokasi haitakuwepo,kitu ambacho wewe mwenyewe unajua ni uwongo

Umesema mabasi 170 yatashushwa ili kuondoa huo usumbufu, ila nikwambie ukweli tu Mwendokasi Shida kuu ya kwanza ni Management mbovu na wezi waliojazana pale, Shirika hata mlete mabasi 1000, kwa ile management ambayo ilitupa mitambo ya kulipia kwa kadi wakaleta mfumo wa upigaji wa kuchana tiketi kwa mikono,sahau mabadiliko pale short and clear huuu mradi atakaeuweza ni sekta Binafsi tu.


Mradi kuanzia Sekta ya uongozi hadi ufundi kumeoza, mabasi bado mapya yameshatupwa yamekufa hadi yana matope ,maana yake hakuna kitengo cha kuyatengeneza kilichomakini maana gari huwa halifi ni kubadili spare tu

Pia zipo tetesi kipindi cha magu waliajiriwa Baka baka ambao wengi ni Madereva ambao wengi wanajiamini kufanya lolote sababu wana mshahara mara mbili, nikuombe tu shirika liendeshwe na sekta binafsi ili kuwe na heshima ya kazi la sivyo wale hata uwaletee magari 10,000, ndani ya mwaka 1 swala litakuwa lile lile, na Mbagala ndio inaenda kuwaaibisha
 
Mimi nikishaona mradi unasimamiwa na hii serikali najua tu utafeli sababu ya upigaji yan
 
Waziri amesema serikali inajitoa kwenye kuendesha mwendokasi. inampa muwekezaji kwa masharti ya kuleta ma bus mengi.

na pia inakuwa rahisi kumpa adhabu akikosea. tofauti na sasa
 
Hadi hiyo Sept sijui October,2024 bado ni MBALI,wananchi wanateseka,tafuteni suluhu za muda mfupi na wa kati ili kupunguza ADHA hizi kwa wananchi
 
Back
Top Bottom