Kwa uzoefu wangu na Biashara hii. Maeneo yote yote unaweza tega na yanalipa vizuri. Ila ukitega uswahilini ndani ndani wekeza kwenye Mitungi midogo sana na ukikaa road weka na mitungi mikubwa kwa kiasi chake (sio kwamba mingi sana) inaweza ikawa mitungi mikubwa 3 au 2 kila Brand.Kaka naomba ushauri ni mazingira yapi mazuri kwa kufanyia hii biashara yaani barabarani au uswahilini??pili je kuna upinzani wowote kutoka kwenye aya maduka ya vitu vidogodogo wanaouza gas pia kwa wewe ambaye unauza gas tu?
Hao wenye viduka vidogo vya mangi halafu wameweka Mitungi wasikuumize kichwa:
1. Fanya delivery
2. Uza Complete kwa bei za offer (mteja aliyenunua Complete kwako ni lazima arudi kubadilisha, hawezi kukuhama)
3. Usipungukiwe na kitu, weka Burner, regulator, Pipe, Clamp, kila kitu na toa ushauri kama mtu mwenye experience (wengi wa watuamiaji gesi ni waoga)
4. Uwe na brand tofauti tofauti
5. Wengi wanaochanganya biashara ya Gesi na duka la Mangi huwa maisha yao si marefu, either wakate/wafilisi mtaji wa gesi au mtaji wa duka sababu ya bei za gesi zipo juu kufananisha na vitu vya dukan kwahyo akicheza vibaya tu mitungi miwili lazima imyumbishe. Mwisho wa siku huwa wanakuja kuacha kuuza gesi wanabaki na mitung kama mapambo