Biashara ya Kununua na Kuuza Mazao (nafaka): Jifunze Mbinu za Kuanzisha na Kusimamia

Mkuu katika Dunia ya sasa yenye ushindani mkubwa sana ni Bora ukafanya kitu inaitwa AD VALUE. Hayo mahindi yaongezee thamani kabla ya kuyauza, make bila hivyo kwa kweli biashara inakuwa ngumu kwa sababu itabidi uwe unafanya Ujanja ujanja ili uweze kupata angalau cha juu na ujanja ujanja huo ni pamoja na kutumia vipimo fake wakati wa kununua.

Na some time kuchanganya mahindi mazuri na ambayo kidogo si mazuri, na huu ujanja huwa ni wa muda tu so kikubwa ni kuyaongezea thamani.
Ubarikiwe sana kwa mchango wako mzuri!
 
Biashara ya nafaka inalipa sana, endapo kama unausafiri wa kusafirisha hizo bidhaa. Mchele, nafaka kama maharage, mbaazi, kunde, choroko, Dengu nzima pamoja na njugu mawe. Zinalipa sana kwa utapata wateja wa mashuleni hasa hiz private school
 
Biashara ya nafaka inalipa sana, endapo kama unausafiri wa kusafirisha hizo bidhaa. Mchele, nafaka kama maharage, mbaazi, kunde, choroko, Dengu nzima pamoja na njugu mawe. Zinalipa sana kwa utapata wateja wa mashuleni hasa hiz private school
kama vipi hii biashara bado inalipa hapa dar
 
Ujanja wa kuhifadhi mazao ili usubiri Bei ipande umepitwa na wakati. Kinacholeta faida kubwa ni kadi ya mzunguko wa mtaji na si kusubiri uuze kwa bei kubwa Mara moja baada ya kuhifadhi kwa miezi mingi.

Mfano umenunua Michele Tani 10 kwa sh 1000/= kwa kilo. Bei ya kuuza kwa jumla kwa Sasa ni sh 1300/= kwa kilo. Lakini ukisubiri kwa miezi mitano ijayo bei itakuwa sh 1,800/= kwa kilo.

Ukiuza Sasa utapata faida ya sh. 300/= x 10,000 = unapata 3,000,000/=. Halafu ndani ya mwezi mmoja unaweza kuzungusha mtaji Mara mbili hivyo kupata faida ya sh 6,000,000/= kwa mwezi. Kwa miezi minne unapata faida ya sh 24,000,000/=.

Ukiuza baada ya miezi mitano utapata faida ya sh 800/= x 10,000 hapo unapata faida ya sh 8,000,000/=.

Sasa aliyekuwa anazungusha mtaji muda wote Ana 24,000,000/= wakati aliyesubiri Bei ipande atapata 8,000,000/=. Hapo nani mjanja? Zaidi ya hayo ukifika mwezi wa tano aliyekuwa anazungusha mtaji wake unakuwa mkubwa na anaweza kuongeza mtaji kwa sh milioni kumi ili aongeze kiwango Cha manunuzi Bei ya kununulia itakapopanda. Hivyo huo mwezi wa tano bado atafanya biashara kubwa tu!

Wajanja walishaachana na ushamba wa kuweka stock kwa biashara ya nafaka!
Japo hii comment ni ya miaka miwili iliyopita, sio mbaya niikijibu kwakua member bado yupo active.

Mkuu ulizungumza kirahisi sana, kuuza tani 10 mara nne ndani ya mwezi mmoja inahitaji soko kubwa sana, vinginevyo utakaa na hizo tani zako mida mrefu kabla haijafata mzigo mwingine.
 
Jenga maize/storage tank la chuma au anything kama la tani 50 au 100 au zaidi ( yapo Alibaba au mafundi wanaweza kukutengenezea), mahindi wakati wa mavuno yanakuwa bei rahisi sana karibu na bure nunua yahifadhi then kiangazi kikifika au mahindi yakipanda bei uanaachia mzigo sokoni, utatengeneza pesa kirahisi sana ila inahitaji mtaji mkubwa kidogo

Mtaji ina range kiasi gani mkuu
 
HHay
Utafiti bubu niliofanya ni kwamba, mahindi mazuri kwa sembe kwa soko la Dar ni yale yanayotoka Kiteto, Dom, Singida na Tanga. Sijui kwa nini wenye milling machines wengi wanayapenda zaidi ukilinganisha na ya nyanda za juu kusini.

Halafu siku hizi hata mikoani kuna milling machines pia, kwa hiyo utaona hoja ya kuongeza thamani bidhaa zako inapata mashiko zaidi kwa karne hii.
Hiyo mikoa tajwa mahindi yake ni mazito!
 
Bhbm,

Mkuu mimi c pingani na wewe but nataka kukushauri jambo moja,

- katika swala zima la biashara ya nafaka ni bora ukajikita katika ku ad value au kuongeza thamani ya hizo nafaka.

1. Ni bora ukawa na ofisi yako mjini na jaribu kuyaongezea thamani hayo mazo kama vile kugred na kupark kabisa. Hapo utakuwa umeongeza thamani na utauza kwa bei ya juu, na unaweza tafuta hata supermaket tano tu za kuwa sambazia.

2. Hili la kununua mchele kutoka mbeya na kuja kuuza dar kama ulivyo hakuna cha maana sana mtu nacho pata zaidi ya ujanja ujanja wa kuchanganya. Mtu anachukua mchele wa mbeya na kuchanganya na mchele wa morogoro
- hii biashara ya nafaka c kwa mba inalipa sana ila ni ujanja ujanja unao fanywa na wauzaji kwa kuchanganya changanya. Anaweza chukua gunia la maharage safi akachanganya na nusu gunia la maharage mabovu ndo business inaenda.

- ila hili la ujanja ujanja ni la muda sana na si endelevu.

So jitajidi upate hata mashine ya kupaki kwenye mifuko, mfano ukipata mashine moja inayo itwa heavy duty sealing machine ni nzuri sana unaweza ukawa na vibarua wako wa kugred na wewe ukawa unapaki na kuuzia watu wa supermarket.

Hiyo mashine niliyo kuambia ni ambayo ina silidi kama vile totopark zinavyo kuwa zimefungwa kwenye vile viroba.

Kuna kampuni moja ya Kenya ina tengeneza vifungashio vizuri sana unweza cheki huko.
Tupe mawasiliano Yako tafadhali
 
Habari za jioni ndugu , naomba mtu ambae ni mzoefu na hii biashara ya kununua na kuuza nafaka hasa mchele (kutoa mikoani) ambae anaifanya hapa Dar es salaam. nahitaji anipatie muongozo na utaratibu mzima wa kuanza lkn itapendeza zaidi tukawasilian 0673117224
 
Hii biashara ya nafaka asikudanganye mtu kuwa inalipa halafu ukaingia kichwakichwa sitosahau kilichokanikuta tandika, nilileta sampo ya choroko madalali wakaniambia choroko safi sana wewe zilete tu basi nikajichanganya nikakusanya tani 30 Kilwa vijijinii nikasafirisha kwa mbwembwe kupeleka Dar wale madalali nilipowapa taarifa kuwa niko njiani wakaniambia wewe zilete tu.

Tumeingia Dar asubuh ya Jumamos dalali ananiambia muhindi kasafiri ila Jumatatu anarudi na atazichukua zote hizi kwa 1200 kwa kilo na wakati huo mimi nilinunua kwa 600 nikajiona nishakuwa tajiri,nilikuwa na laki 3 nikaamua kuponda raha na watoto wazuri kwakuamini jumatatu naikunja hela yangu aiseee laiti ningejua.

Kiukweli Jumatatu ikafika nikamstua dalali twende basi kwa Muhindi akaniambia Muhindi hanunui tena kiukweli nilipagawa sana nikamuuliza nani sasa ananunua akaniambia hamna anayenunua kama vipi nichukue sampuli nipite natembeza kwenye masoko. Aisee nilitembeza masoko yote Dar kwa wiki mzima hata mmoja aliechukua nikaenda sehemu fulani nikakaa nikaanza kulia kilio cha chinichini na mfukoni nina kama elfu 20 tu ghafla napokea simu mwenye store anaitaka store yake kuna mzigo anataka kuuweka, baadae mtu fulani akanihurumia akaniunganisha na tajiri yupo dodoma yule jamaa alinunua zote kwa bei ya 1270.
 
Hii biashara ya nafaka asikudanganye mtu kuwa inalipa halafu ukaingia kichwakichwa sitosahau kilichokanikuta tandika,nilileta sampo ya choroko madalali wakaniambia choroko safi sana wewe zilete tu basi nikajichanganya nikakusanya tani 30 kilwa vijijinii nikasafirisha kwa mbwembwe kupeleka dar wale madalali nilipowapa taarifa kuwa niko njiani wakaniambia wewe zilete tu,,tumeingia dar asubuh ya jumamos dalali ananiambia muhindi kasafiri ila jumatatu anarudi na atazichukua zote hizi kwa 1200 kwa kilo na wakati huo mimi nilinunua kwa 600 nikajiona nishakuwa tajiri,nilikuwa na laki 3 nikaamua kuponda raha na watoto wazuri kwakuamini jumatatu naikunja hela yangu aiseee laiti ningejua...kiukweli jumatatu ikafika nikamstua dalali twende basi kwa muhindi akaniambia muhindi hanunui tena kiukweli nilipagawa sana nikamuuliza nani sasa ananunua akaniambia hamna anayenunua kama vipi nichukue sampu nipite natembeza kwenye masoko aisee nilitembeza masoko yote dar kwa wiki mzima hata mmoja aliechukua nikaenda sehemu fulani nikakaa nikaanza kulia kilio cha chinichini na mfukoni nina kama elfu 20 tu ghafla napokea simu mwenye store anaitaka store yake kuna mzigo anataka kuuweka...baadae mtu fulani akanihurumia akaniunganisha na tajiri yupo dodoma yule jamaa alinunua zote kwa bei ya 1270
Ukianza sasa hutaanzia chini bali utaanzia kwenye elimu na uzoefu ulipota kutokana na tukio hilo.

Hongera sana mkuu
 
Mkuu "Chasha Poultry Farm" nimekuwa nikifatilia comments zako nyingi kwenye threads tofauti kwa kweli una mitazamo ya tofauti, kisomi na kimapinduzi zaidi kwenye tasnia nzima ya ujasiriamili na biashara Tanzania, binafsi nimekuwa insipired sana na miongozo yako mbalimbali, Mungu akubariki.

Value addition is very important in every things we do as entrepreneur and business men, watanzania umefika wakati tutoke kwenye mbinu za ujima za kibiashara. Mkuu big up sana.

Nipo kwenye ajira kwa sasa, ila for sure I'm not happy being employed, this two years of employment are more than enough, anytime soon naenda kujiajiri coz I can see and feel niko na spirit ya ajabu in entrepreneurship and business, my business idea ni kuwa supplier wa food staffs kwenye big hotels and supemarkets in town ndio maana point yako ya value addition imenigusa sana na malengo makuu ni oneday kumiliki viwanda vya kuchakata na kusindika mazao mbalimbali ya majini na nchi kavu for export purpose.

I do believe oneday nitaleta mrejesho wa mafanikio makubwa kwenye hili, mungu awabariki wana JF wote.

AMEN
Vipi mkuu samahani!,, ulifanikiwa kuanza hii biashara??
 
Hii biashara ya nafaka asikudanganye mtu kuwa inalipa halafu ukaingia kichwakichwa sitosahau kilichokanikuta tandika,nilileta sampo ya choroko madalali wakaniambia choroko safi sana wewe zilete tu basi nikajichanganya nikakusanya tani 30 kilwa vijijinii nikasafirisha kwa mbwembwe kupeleka dar wale madalali nilipowapa taarifa kuwa niko njiani wakaniambia wewe zilete tu,,tumeingia dar asubuh ya jumamos dalali ananiambia muhindi kasafiri ila jumatatu anarudi na atazichukua zote hizi kwa 1200 kwa kilo na wakati huo mimi nilinunua kwa 600 nikajiona nishakuwa tajiri,nilikuwa na laki 3 nikaamua kuponda raha na watoto wazuri kwakuamini jumatatu naikunja hela yangu aiseee laiti ningejua...kiukweli jumatatu ikafika nikamstua dalali twende basi kwa muhindi akaniambia muhindi hanunui tena kiukweli nilipagawa sana nikamuuliza nani sasa ananunua akaniambia hamna anayenunua kama vipi nichukue sampu nipite natembeza kwenye masoko aisee nilitembeza masoko yote dar kwa wiki mzima hata mmoja aliechukua nikaenda sehemu fulani nikakaa nikaanza kulia kilio cha chinichini na mfukoni nina kama elfu 20 tu ghafla napokea simu mwenye store anaitaka store yake kuna mzigo anataka kuuweka...baadae mtu fulani akanihurumia akaniunganisha na tajiri yupo dodoma yule jamaa alinunua zote kwa bei ya 1270
Ukajiona ushakuwa tajiri bonge la Businessman na ukaanza kutafuta watoto warembo,ogopa sana madalali
 
Ukajiona ushakuwa tajiri bonge la Businessman na ukaanza kutafuta watoto warembo,ogopa sana madalali
Yeye alikosea mzigo kama choroko hakuna haja ya dalali maana wateja wanafahamika ni wahindi,,angetakiwa kutembelea magodown wa wahindi kama kina Afrisian achukue namba anakua anapiga tu akihitaji kuleta mzigo,,,
 
Nimekuelewa sana ndg yangu wa choroko kisa kama hiki kilinikuta solo la mmbande dalali kaniambia nipeleke pilipili mwendo Kasi idadi yeyote ndoo kubwa sh 40,000 nikakopa mpaka nauli kufika na ndoo 10 dalali anasema hazijaiva vizuri hakuna biashara nikaanzq kuzunguka kila genge kuuza kidogokidogo kumbe wote wamoja,mwisho nikamwangukia dalali yuleyule akachukua kwa 10,000 kwa ndoo nikaapa kutorudia makosa madalali ni pasua bichwa
 
Back
Top Bottom