Biashara ni ngumu jamani!

Biashara ni ngumu jamani!

Ngoja nikupe ushauri general watu wanaofanikiwa kwenye biashara wanakuwa na sifa zipi au wanafanyaje kwenye biashara zao hadi unawaona wanafanikiwa,nina imani biashara yako ni mpya na ndio maana umekuja kuomba ushauri.
1.Kitu cha kwanza kabisa unatakiwa ujue watu wa katika eneo lako wanahitaji nini au wana tatizo gani linalowasumbua halafu wewe ndio ulete utatuzi wa jambo hilo usiuze biashara ya vitu ambavyo umeviwaza wewe tu kichwani kwako.
Kwa mfano kama unaishi kwenye eneo ambalo watu wana shida ya maji wewe anzisha mradi wa kuuza maji utapata wateja.
2.Kitu kingine wakati unaanza biashara ukishatenga pesa ya mtaji na kodi zote hakikisha una pesa nyingine ya ziada kwa ajili ya kuendesha maisha yako kwa muda hata wa mwaka mmoja bila ya kutegemea biashara ndio ihudumie familia utakwama maana kwa kipindi cha mwanzo faida itakuwa ni ndogo na itaishia tu kwenye kuhudumia biashara tu ili isife.
3.Hakikisha umejipangia malengo yako ya muda mrefu,kwa mfano umeanza na biashara ya mgahawa lakini malengo yako ni kuja kumiliki hotel so usibweteke hadi lengo lako la kumiliki hotel litimie.
4.Jitangaze/fanya marketing usingoje hadi mteja aje mwenyewe hii staili imepitwa na wakati siku hizi biashara yoyote inahitaji utengeneze connection kuanzia kwa marafiki,ndugu,majirani ukiwaalika kuja kupata huduma na huduma yako ikiwa nzuri watakuletea na wateja wengine.
Ongea na watu vizuri,usidharau mtu wa aina yoyote ongea hata na bodaboda wawe wanakuletea wateja au unawapa vipeperushi wanavisambaza kisha unawalipa hela ndogondogo.
Tangaza na mitandaoni pia facebook,Instagram,Tiktok weka mawasiliano yako.
5.Hakikisha bidhaa zako ziwe zina upekee fulani ukilinganisha na wapinzani wako lakini bei pia iwe na unafuu kidogo kulinganisha na wapinzani wako hapo utawavutia wateja na wataanza kusimuliana kuhusu bidhaa zako.
6.Uvumilivu-Hapa ndipo pagumu na wafanyabiashara wengi wanaoanza biashara huishia kati na kunyoosha mikono juu.
Mtu anafanya kwa miezi 3 akishaona hapati hela alizotarajia anaachana nayo anarukia kitu kingine hakikisha unakuwa king'ang'anizi hadi utengeneze jina faida zitakuja mbeleni.
Hasa kama mtu unasimamia biashara Mwenyewe dukani hela ya kula na matumizi binafsi utatoa Wapi me hela imenikata vibaya nina mwaka faida ndogo ns nategemea Duks tu
 
Mkuu pesa ya matumizi yangu binafsi wala haitegemei biashara yangu hata shilingi mia moja.
Pesa ya matumizi yangu najitosheleza nayo mwenyewe kwa sasa,labda kwa baadaye
Wekeza zaidi huko kunakokupatia "pesa ya matumizi yako binafsi" kwa sababu inaonekana ndo pako vizuri. Kimsingi wewe tayari umeshafeli kwa kufakamia hizo bia wakati biashara yako ni ngumu. Pombe itakuongezea matatizo zaidi.
 
Ngoja nikupe ushauri general watu wanaofanikiwa kwenye biashara wanakuwa na sifa zipi au wanafanyaje kwenye biashara zao hadi unawaona wanafanikiwa,nina imani biashara yako ni mpya na ndio maana umekuja kuomba ushauri.
1.Kitu cha kwanza kabisa unatakiwa ujue watu wa katika eneo lako wanahitaji nini au wana tatizo gani linalowasumbua halafu wewe ndio ulete utatuzi wa jambo hilo usiuze biashara ya vitu ambavyo umeviwaza wewe tu kichwani kwako.
Kwa mfano kama unaishi kwenye eneo ambalo watu wana shida ya maji wewe anzisha mradi wa kuuza maji utapata wateja.
2.Kitu kingine wakati unaanza biashara ukishatenga pesa ya mtaji na kodi zote hakikisha una pesa nyingine ya ziada kwa ajili ya kuendesha maisha yako kwa muda hata wa mwaka mmoja bila ya kutegemea biashara ndio ihudumie familia utakwama maana kwa kipindi cha mwanzo faida itakuwa ni ndogo na itaishia tu kwenye kuhudumia biashara tu ili isife.
3.Hakikisha umejipangia malengo yako ya muda mrefu,kwa mfano umeanza na biashara ya mgahawa lakini malengo yako ni kuja kumiliki hotel so usibweteke hadi lengo lako la kumiliki hotel litimie.
4.Jitangaze/fanya marketing usingoje hadi mteja aje mwenyewe hii staili imepitwa na wakati siku hizi biashara yoyote inahitaji utengeneze connection kuanzia kwa marafiki,ndugu,majirani ukiwaalika kuja kupata huduma na huduma yako ikiwa nzuri watakuletea na wateja wengine.
Ongea na watu vizuri,usidharau mtu wa aina yoyote ongea hata na bodaboda wawe wanakuletea wateja au unawapa vipeperushi wanavisambaza kisha unawalipa hela ndogondogo.
Tangaza na mitandaoni pia facebook,Instagram,Tiktok weka mawasiliano yako.
5.Hakikisha bidhaa zako ziwe zina upekee fulani ukilinganisha na wapinzani wako lakini bei pia iwe na unafuu kidogo kulinganisha na wapinzani wako hapo utawavutia wateja na wataanza kusimuliana kuhusu bidhaa zako.
6.Uvumilivu-Hapa ndipo pagumu na wafanyabiashara wengi wanaoanza biashara huishia kati na kunyoosha mikono juu.
Mtu anafanya kwa miezi 3 akishaona hapati hela alizotarajia anaachana nayo anarukia kitu kingine hakikisha unakuwa king'ang'anizi hadi utengeneze jina faida zitakuja mbeleni.
Hii namba 4 sasa ndugu na majirani kutegemea kukopwa no kuchelewa kulipwa,
 
Habarini wana jukwaa,najua ni usiku wengine tupo tunakunywa mbili tatu na huku kukiwa na hali ya hewa murua sana nyanda za juu kusini kama mjuavyo.

Siyo kila anayekesha bar anasherekea m, wengine tunatumia muda kuwaza jinsi mambo yanavyokuwa magumu kwenye mitikasi yetu.

Biashara ngumu jamani!, au hapa nlipo mzunguko wa hela ndiyo mdogo,mbona watu wanapesa sana huku lakini.. Watu mkitoka Chunya kwani hela mnazipeleka wapi mpaka zipitize huu mji wetu?🙂

Anyway,point yangu imekuwa mbali,lakini naomba unipe moyo wewe uliyefanikiwa kwenye biashara yako,ilikuchukua muda gani mpaka ikaanza kukuingizia faida? Naona yangu hii inaenda kumaliza zaidi ya miezi mi4 nikipiga operational costs bado sioni faida. Nliifungua kwenye eneo ambalo linahitaji promosion sana watu kupafahamu,lakini naamini watu huwa wanafuata huduma na kwangu watapafahamu,lakini itachukua muda gani?😐😐😐

Watu wa Mbeya tumieni hela jamani mnaweza nilenga namimi bila kujua.
NOTE: sitaongelea ni biashara ya aina gani,wewe toa ushauri wako kwa general experience yako tu ita cross-cut pote.

Haya ngoja nirudi kwa wife kama ntafunguliwa mlango🏃🏃🏃🏃
Biashara ni ngumu kila kona saivi, naona walalamikaj ni wengi sana!
 
Kwa mkoa kama dar ushindani Sasa hivi kila mtu anafanya biashara mpka waha wanakopesha bidhaa zako tena wanachukua kkoo wanapitia buku buku tu
Hii sio dar tu, nafkiri tu hali tu imekaza sijui ni kwanini
 
Ni balaa.. na hivi huku mvua inajinyea tu mi ndo hata sitoki nje! Unaenda pigwa baridi na hela haip

Ni balaa.. na hivi huku mvua inajinyea tu mi ndo hata sitoki nje! Unaenda pigwa baridi na hela haipo😁
Mikoani peleka bidhaa hasa minadani Dar wafanyabiashara Tupo wengi na kkoo hapo tu
 
Hii sio dar tu, nafkiri tu hali tu imekaza sijui ni kwanini
Sema wafanyabiashara tunapapenda dar uchukuaji bidhaa simple tofauti uwe chemba kwa mtoro bidhaa utauza ila kufuata dar gharama
 
Huu mwezi ndo umekaza sana wiki ya pili from September biashara hesabu inakataa kabisaaa sijui kwann lakini lazma niishi
 
Mikoani peleka bidhaa hasa minadani Dar wafanyabiashara Tupo wengi na kkoo hapo tu
Kama mikoa ipi? Kumbukeni miji inakuwa kwa kasi pia sio kama zamani! Na mikoani pia kuna watu na biashara zao sasa mlete mikoani afu wa mikoani wapeleke wapi? Au vijijini zaidi😂
 
Sema wafanyabiashara tunapapenda dar uchukuaji bidhaa simple tofauti uwe chemba kwa mtoro bidhaa utauza ila kufuata dar gharama
Kuna biashara nyingine saiz zipo mikoani ata kwa jumla watu hawafuati dar, mf. Mzuri mwanza! Yani sio kama zamani.. baadhi ya biashara tu ndio watu wataagiza lkn nyingi watu wanafanya bila kutegemea dar
 
Kama mikoa ipi? Kumbukeni miji inakuwa kwa kasi pia sio kama zamani! Na mikoani pia kuna watu na biashara zao sasa mlete mikoani afu wa mikoani wapeleke wapi? Au vijijini zaidi😂
😛😛😛 ndiyo kama minadani vijijini Dar viatu maduka mtaa mzima mnavyo
 
Huu mwezi ndo umekaza sana wiki ya pili from September biashara hesabu inakataa kabisaaa sijui kwann lakini lazma niishi
Same! Hakuna nachofanya hapa kuishi ni lazima ila cha moto!
 
Back
Top Bottom