Tauceti Rigel
JF-Expert Member
- Mar 6, 2025
- 201
- 555
Habari za wakati huu wakuu.
Naomba ushauri kutoka kwa wenye uzoefu na biashara ya nyama choma hapa jijini Dar es Salaam.
Nina mpango wa kuanzisha biashara ya nyama choma, lakini sitaki kabisa kuifanya sehemu ya baa. Nia yangu ni kuifikisha huduma hii kwa watu wa kawaida – wale wanaotafuta chakula kizuri kwa bei halali, bila kelele za pombe wala mazingira ya ulevi.
Maeneo ninayoyafikiria kwa sasa ni:
Sababu kubwa ya kuchagua maeneo haya ni kwamba watu wa maeneo hayo wanahangaika mchana kutwa kwenye kazi ngumu – mafundi, waendesha bodaboda, wapita njia, nk – na wangependa nyama choma ya ukweli bila kwenda baa.
Changamoto yangu ni mtaji mdogo. Natafuta namna ya kuanza kwa mazingira ya kawaida kabisa – hata kama ni kujibanza kwenye mradi wa mtu mwingine kwa kuchangia pango, mradi tu nianze.
Swali langu kuu ni hili:
Ninawezaje kupata faida hata kama nitakuwa nauza portion kubwa kwa bei ya kawaida?
Binafsi ninaumia sana kuona mtu analipa elfu tano kwa ugali nyama, lakini anawekewa nyama kama ya buku. Mimi natamani niwe tofauti – niuze ukweli wa nyama, lakini bado niwe na faida ya kujiendeleza.
Naomba ushauri wenu:
Nawakaribisha kwa moyo wote – mawazo, uzoefu, hata kunielekeza kwa mtu anayetoa nafasi ya kushirikiana ni msaada mkubwa.
Asanteni sana kwa muda wenu 🙏🏾
Nakaribisha hata inbox kama kuna mtu anaweza kunifungulia milango zaidi.

- Kitunda
- Karibu na Chuo cha Kampala – Gongo la Mboto
- Tabata Dampo (eneo lenye maspare mengi ya magari na gereji)
Sababu kubwa ya kuchagua maeneo haya ni kwamba watu wa maeneo hayo wanahangaika mchana kutwa kwenye kazi ngumu – mafundi, waendesha bodaboda, wapita njia, nk – na wangependa nyama choma ya ukweli bila kwenda baa.
Changamoto yangu ni mtaji mdogo. Natafuta namna ya kuanza kwa mazingira ya kawaida kabisa – hata kama ni kujibanza kwenye mradi wa mtu mwingine kwa kuchangia pango, mradi tu nianze.
Swali langu kuu ni hili:
Ninawezaje kupata faida hata kama nitakuwa nauza portion kubwa kwa bei ya kawaida?
Binafsi ninaumia sana kuona mtu analipa elfu tano kwa ugali nyama, lakini anawekewa nyama kama ya buku. Mimi natamani niwe tofauti – niuze ukweli wa nyama, lakini bado niwe na faida ya kujiendeleza.
Naomba ushauri wenu:
- Nianzie vipi kama nataka kujibanza kwa mtu mwingine?
- Wapi napata nyama kwa bei nzuri ya jumla (labda machinjioni?)
- Nidhibiti vipi ubora, wingi wa nyama, na faida kwa pamoja?
- Kuna changamoto gani za kufanya biashara hii nje ya baa?