carbohydates
Member
- Oct 13, 2026
- 18
- 35
Benki ya Dunia imeweka msisitizo katika kuhamasisha mitaji ya sekta binafsi ili kuchochea uwekezaji na kupanua fursa za ajira kwa vijana barani Afrika, kupitia biashara ndogo na za kati, madini na maendeleo ya viwanda.
Mkazo huo umejadiliwa katika Mkutano wa Magavana wa Nchi Wanachama wa Benki ya Dunia barani Afrika (African Governors’ Caucus Meeting), uliofanyika Bangkok, Thailand, ukiwa sehemu ya Mikutano ya Mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Kundi la Benki ya Dunia.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, ambaye pia ni Gavana Mbadala anayewakilisha Tanzania katika Benki ya Dunia, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, alishiriki mkutano huo na Rais wa Benki ya Dunia, Ajay Banga, kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar.
Majadiliano hayo yalilenga mipango ya Benki ya Dunia barani Afrika, pamoja na namna ya kuhamasisha mitaji ya sekta binafsi ili kuimarisha uwekezaji, kukuza ujuzi na kuongeza uwezo wa biashara ndogo na za kati katika kuzalisha ajira.
Ushiriki wa Tanzania katika majadiliano hayo unakuja wakati suala la upanuzi wa shughuli za kiuchumi, uendelezaji wa viwanda na kuongeza thamani ya rasilimali likiwa muhimu katika kujenga uchumi unaozalisha ajira na fursa za biashara.
Kupitia uwekezaji katika madini na viwanda, nchi za Afrika zina nafasi ya kuongeza thamani ya malighafi kabla ya kuziuza, badala ya kutegemea mauzo ya bidhaa ambazo hazijachakatwa. Hatua hiyo inaweza kuchochea shughuli za uzalishaji, kuongeza mahitaji ya wataalamu na kupanua fursa kwa wajasiriamali.
Vilevile, kuimarishwa kwa biashara ndogo na za kati kunaweza kuongeza nafasi ya vijana kushiriki katika shughuli za kiuchumi, hususan pale wanapopata mitaji, ujuzi na masoko ya uhakika.
Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Mipango na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dkt. Tausi Mbaga Kida, pamoja na Kamishna Msaidizi wa Idara ya Fedha za Nje katika Wizara ya Fedha, Robert Mtengule.
Chanzo : Radio saut fm