TANZIA Benjamin William Mkapa, Rais wa Tanzania wa Awamu ya Tatu afariki dunia

Status
Not open for further replies.
Hakuna atakaye dumu milele, Duniani tunapita tu,
Bwana alitoa na Bwana ametwaa, Jina lake libarikiwe
 
Nimesikia radio Tumaini nikahisi mtangazaji amekosea! Hiki ni kishindo kwa nchi. Tunaomba Mungu nchi yetu ibakie moja kama tulivyopita salama baada ya kuondoka Baba wa Taifa. Pumzika kwa amani mzee wetu, kiongozi wetu, mtu mwenye msimamo ....Mzee Benjamini William Mkapa ...
 
May his soul rest in eternal peace🙏 Alikua kiongozi mwema kwa nchi yetu.
 
Ni vizuri sana kuwa na busara ya kuacha kutumia vifo vya watu wengine kwa malengo ya kijenga hoja za kisiasa bila uthibitisho wake. Wote tunatembea na vifo vyetu viganjani mwetu. Tusubiri facts kwanza halafu ndipo tuzichambue
Mkubwa , huwezi kumtenga Mkapa na Siasa. Mshtuko ulioikumba jamii ni kutokana na haiba yake kisiasa. Leo kuna mamia ya watu wametangulia mbele ya haki, kwanini haiujulikani! si wanasiasa kama Mkapa.

2. Bendera zitapepea nusu mlingoti kwasababu mwanasiasa kafariki, si wananchi wengi waliofariki jana na leo.

3. Kwaviletumevunja utamaduni wa facts, zipi unataka watu wasubiri? Watu watasema kwavile tumevunja trust inayotoa facts. Watu hawaamini tena kinachosemwa!
 
Nimesikia radio Tumaini nikahisi mtangazaji amekosea! Hiki ni kishindo kwa nchi. Tunaomba Mungu nchi yetu ibakie moja kama tulivyopita salama baada ya kuondoka Baba wa Taifa. Pumzika kwa amani mzee wetu, kiongozi wetu, mtu mwenye msimamo ....Mzee Benjamini William Mkapa ...
Wee jamaa kishindo kipi kwa nchi? Mnatakiwa mujue kuwa siasa za uongo uongo na kufunika uhalisia zinapoteza uhai wa watanzania kizembe zembe sana na ni aibu kwa nchi. Naendelea kusimama na ubalozi wa Marekani ili nibakie salama tena!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom