Choveki,.....Kwa nini usi-type kwenye GOOGLE na utapata habari zote hizi. Acheni uvivu jamani wa utafutiwe hata habari kama hizi......KILIMANJARO AIRPORT UP FOR GRAB FOR JUST 1000 US
Hapana ndugu Sikonge si uvivu bali ni kwamba muda mwingi inabidi nirudie kusoma marudio ya kijana mtanashati na jinsi alivyo na akili finyu ukilinganisha na uncle Ben, wakati miye nataka nisome ya uncle Ben W, ila kutokana na watu kurudia rudia mambo ya kijana mtanashati, inanibidi nitumie muda mrefu zaidi kutafuta ya rais mstaafu ili nielewe mabaya yake pia, kwani mabaya ya kijana wetu yapo nje nje na sihitaji kukumbushwa!
Kinachosikitisha ni kuwa uwanja wa KIA umekodishwa kwa
dola 1000 kwa mwaka na bado huyo aliyekuwa mkuu wa nchi anapewa sifa ya kimungu mungu!, Hapo hujaangalia NBC, Kiwira, Tanesco, akina TANGOLD, Meremeta, Radar, EPA-malipo hewa benki kuu-, ndege ya Raisi nk.
Pia nashangaa kuwa badala ya kujadili ishu tunaleta ushabiki ushabiki tu, je unadhani Tz tutaendelea?, Kitakachotokea ni kuwa tutaendelea kubadilisha na kuchagua maraisi vilaza mmoja baada ya mwingine kila baada ya miaka kumi mpaka tushike adabu zetu!! Unadhani ule msemo wa Wajinga ndiyo waliwao maana yake nini? Maraisi tuwachaguao huwa wanatupaka mafuta kwa migongo ya chupa nasi tunahisi ati wanatupenda kama watanzania wenzao.
Anayeongelewa ni huyu:
Benjamin William Mkapa nimjuaye...(kama kielezavyo kichwa cha habari) kuna mijadala lukuki ya JK, kwanini na huu tuupeleke kwa JK?
mnapenda kulazimisha mambo! haya maoni ya watu, akili zao, muda wao, malengo yao, huwezi kuwapangia watu waseme nini na lini, wala usijione una akili, nionyeshe thread moja tu ya JF ambayo watu waliajadili same thing bila kwenda nje kidogo ya maada! utapata pressure za bure kuhangaika kuwa kiranja humu! sema ulilonalo moyoni usaidiwe! acha kutapatapa!
Hapana Mkuu Waberoya, nilichokumbusha ni kuwa sioni sababu ya kumjadili JK kwenye mjadala wa BWM, kwani huu mjadala siyo wa kuwalinganisha hawa jamaa wawili, bali kujadili BWM na alivyotuingiza mjini. Pia si kwamba nalazimisha mambo, nadhani aliyelazimisha huu mjadala ni Kaniki, kwani ameeleza kinagaubaga kuwa anamsifu BWM kwa mazuri yake ndipo na wengine wakaamua kuandika mabaya yake! Kilichonitatiza ni kuwa badala ya kushusha nondo za huyu muungwana BWM, nondo zinazoshushwa ni za muungwana JK. Mimi nilichokumbusha ni kuwa mijadala ya JK ni mingi mno, na ukisoma mengi yaandikwayo unatamani kulia machozi kuisikitikia Tanzania yetu, na nikawa nakumbusha kuwa huu ni wa BWM siyo JK.
La mwisho ni kuwa pressure itanipata kwa sababu naipenda Tanzania kupita kiasi na kila baada ya miaka kumi tunachagua nunda mpya wa kutuingiza mjini!