Sintamkumbuka Mkapa kwa lolote jema zaidi ya kumkumbuka kwa wizi na unafiki wake dhidi ya Mwalimu..Hata hizi figure za Inflation hazimsaidii mwananchi hata kidogo kwa sababu mimi nakumbuka vizuri nilikuwa Bongo mwaka 1995 alipoingia madarakani nyumba Kariakoo zilikuwa zikiuzwa kwa Tsh millioni 20 kwa exchange rate ya 500, na niliporudi mwaka 2005 zilifikia dollar 800,000 kwa exchange rate ya 1100. Kila kitu kilipanda bei asilimia 100 ya bei niliyoiacha mwaka 1995 isipokuwa usafiri wa daladala. Umeme wa mgao na maji hakuna, reli ya kati imesimama ktk utawala wake, ATC inakufa na kutemwa na South, mvua zimegoma hadi watu wamekufa njaa kwa mara ya kwanza ktk historia ya Tanzania..
Maisha magumu kwa Mtanzania yalianza wakati wa Mkapa, na hata hizo sifa za ukusanyaji wa kodi haziwezi kusifika kiasi hicho ikiwa kabla ya hapo, nchi nzima ilikuwa ya Kijamaa na serikali ndio ina control njia zote za uchumi, sasa mlitegemea kodi ikusanywe vipi tofauti na serikali ya Mkapa iliyokusanya fedha toka soko huru ambalo halikuwepo awali?..
Definitely, kutakuwepo na tofauti ya makusanyo hata kama njia alizotumia ni mbaya sawa na nyumba za kariakoo zilizokuwa wakiishi familia bure mara wakaanza kupangisha na kukusanya kodi kisha unahesabu tofauti ya fedha toka kuishi wenyewe bure na ile ya kupangisha bila kutazama ubora wa pangisho kulingana na market rate ya kupangisha kama wanavyopangisha wengine..
sasa kwa msomi yeyote anaejua Ukusanyaji kodi na taratibu zake atakubaliana nami kwamba kilichofanyika ni kuwabana tu wananchi walipe kodi ya pango badala ya kuishi bure lakini utaratibu wenyewe haukuzingatia thamani ya vitu hivyo wala njia bora za kudhibiti urasimu na ukiritimba ndani ya vyombo vya ukusanyaji.. Matokeo yake wafanyakazi wa TRA wametajirika tokana na wizi wa kodi pia mafisadi wameiba matrillioni ya kodi, uuzaji wa mashirika na nyumba za nyumba za serikali ktk bei ya kutupa ili mradi mfuko wa serikali uonekane umetuna..
Guyz, huwezi kusifia mtu wa Kariakoo aliyeuza nyumba ya urithi kwa dollar millioni akaenda kuishi Mabibo, asiwekeze ila kaoa wake wanne kuwa ni wazo zuri zaidi kwa sababu kauza nyumba ambayo mzee wake hakuona thamani ya nyumba hiyo alipokuwa akiishi yeye. Kwa nini asisifiwe mzee alojenga Kariakoo kuwa ndio kiini cha utajiri wa huyu bwana kama mnavyomponda mwalimu kila siku bila kujua kwamba pasipo ujenzi wa mwalimu, Mkapa had nothing to sale..Na pasipo utandawazi na soko huria Mkapa had nothing to correct from...Kwa hiyo kama kuna sifa mnayotaka kumpa Mpaka ni kuthaminisha alichokifanya baada ya kukusanya fedha hizo za urithi - Kiuchumi Mkapa kenda kuoa wake wanne!