Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,064
- 22,757
Na Asha Bani - Tanzania Daima
Akizungumza na waandishi wa habari jana katika makao makuu ya chama hicho, Mkurugenzi wa Uenezi na Propaganda, Hizza Tambwe, alisema vikundi hivyo ambavyo vimechaguliwa ni vile vilivyotunga nyimbo za chama kwa ajili ya kuhamasisha watu kukichagua kwa kishindo.
Tumeamua kutumia wasanii na sanaa katika vikundi vingi katika uchaguzi huu kwa kuwa nyimbo za wasanii mara nyingi zimekuwa zikiwavutia jamii na kuelezea hali halisi ya mafanikio ya chama na si vinginevyo, alisema Tambwe.
Mwanasiasa huyo alivitaja vikundi hivyo ambavyo tayari vimeshawasilisha nyimbo zao ni pamoja na Dar es Salaam Modern Taarab, Bwagamoyo Sound, Abdul Salvador na Hisia Bendi, Msondo Ngoma, Sikinde Ngoma ya Ukae, Hussein Jumbe, New Zanzibar Stars Modern Taarab, Super Shine Modern Taarab na kundi la Mapambano.
Vikundi vingine ni pamoja na Five Stars Morden Taarab, Katavi Musica Band, Rashid Kalala, FM Academia, Twanga Pepeta, msanii wa kundi la kuigiza ambaye kwa sasa ni mwimbaji Dokii, Inspector Haroun (Babu), Danny na David, Wahdatul, Mwendapole, TMK Wanaume, Swax Family, Tumsifu na kundi la sanaa la Nimujo.
Vikundi vingine ni kundi la mchiriku, Tandare Modern Taarab, Skills, Five Stars, Omary Tego, Cost Modern Taarab na Hadija Omary Kopa.
Wakati huo huo, chama hicho kimejitangazia ushindi wa kishindo katika nafasi ya urais na kudai kuwa Rais Jakaya Kikwete anasubiri kuapishwa kutokana na kukosa mpinzani ndani ya chama na nje ya chama.
Uchaguzi kwa upande wetu umekwisha, kwa sasa tunasubiri rais wetu kuapishwa na hata hivyo hakuna nguvu za kutoka katika vyama vingine vya upinzani ila tunachojua rais anaumiza kichwa kumchagua atakayerithi mikoba mwaka 2015, na si vinginevyo, alisema Tambwe.
My take - Kama hili dai ni kweli kampeni yote hiyo ya nini ? Tunajua chema huwa chajiuza asubuhi sasa kwa nini CCM inajitembeza kiasi hiki hadi usiku? Je ni kweli Jakaya Mrisho Kikwete anaumiza au anaumizwa ? Piki piki, mipasho ya vikundi vya taarabu, rushwa ya pilau na fulana, kupakatwa na vyombo vya dola - vyote hivi ni dalili ya kutambua kutouzika na hivyo kutafuta ushindi kwa mbinde. Kwa mbaaali naona kuna mtu ataumia, yangu macho.