Bendi za muziki 30 kumpigia kampeni Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bendi za muziki 30 kumpigia kampeni Kikwete

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mag3, Jul 1, 2010.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  Jul 1, 2010
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Na Asha Bani - Tanzania Daima

  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kinatarajia kutumia vikundi mbalimbali vya sanaa na bendi 30 ambavyo vimetunga nyimbo za kuhamasisha wananchi kumpigia kura Rais Jakaya Kikwete wakati wa Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana katika makao makuu ya chama hicho, Mkurugenzi wa Uenezi na Propaganda, Hizza Tambwe, alisema vikundi hivyo ambavyo vimechaguliwa ni vile vilivyotunga nyimbo za chama kwa ajili ya kuhamasisha watu kukichagua kwa kishindo.

  “Tumeamua kutumia wasanii na sanaa katika vikundi vingi katika uchaguzi huu kwa kuwa nyimbo za wasanii mara nyingi zimekuwa zikiwavutia jamii na kuelezea hali halisi ya mafanikio ya chama na si vinginevyo,” alisema Tambwe.

  Mwanasiasa huyo alivitaja vikundi hivyo ambavyo tayari vimeshawasilisha nyimbo zao ni pamoja na Dar es Salaam Modern Taarab, Bwagamoyo Sound, Abdul Salvador na Hisia Bendi, Msondo Ngoma, Sikinde Ngoma ya Ukae, Hussein Jumbe, New Zanzibar Stars Modern Taarab, Super Shine Modern Taarab na kundi la Mapambano.

  Vikundi vingine ni pamoja na Five Stars Morden Taarab, Katavi Musica Band, Rashid Kalala, FM Academia, Twanga Pepeta, msanii wa kundi la kuigiza ambaye kwa sasa ni mwimbaji Dokii, Inspector Haroun (Babu), Danny na David, Wahdatul, Mwendapole, TMK Wanaume, Swax Family, Tumsifu na kundi la sanaa la Nimujo.

  Vikundi vingine ni kundi la mchiriku, Tandare Modern Taarab, Skills, Five Stars, Omary Tego, Cost Modern Taarab na Hadija Omary Kopa.

  Wakati huo huo, chama hicho kimejitangazia ushindi wa kishindo katika nafasi ya urais na kudai kuwa Rais Jakaya Kikwete anasubiri kuapishwa kutokana na kukosa mpinzani ndani ya chama na nje ya chama.


  “Uchaguzi kwa upande wetu umekwisha, kwa sasa tunasubiri rais wetu kuapishwa na hata hivyo hakuna nguvu za kutoka katika vyama vingine vya upinzani ila tunachojua rais anaumiza kichwa kumchagua atakayerithi mikoba mwaka 2015, na si vinginevyo,” alisema Tambwe.  My take - Kama hili dai ni kweli kampeni yote hiyo ya nini ? Tunajua chema huwa chajiuza asubuhi sasa kwa nini CCM inajitembeza kiasi hiki hadi usiku? Je ni kweli Jakaya Mrisho Kikwete anaumiza au anaumizwa ? Piki piki, mipasho ya vikundi vya taarabu, rushwa ya pilau na fulana, kupakatwa na vyombo vya dola - vyote hivi ni dalili ya kutambua kutouzika na hivyo kutafuta ushindi kwa mbinde. Kwa mbaaali naona kuna mtu ataumia, yangu macho.
   
 2. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #2
  Jul 1, 2010
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Si mkwere tule bwana...anafikiri Tz nzima wote ni wapenda muziki.....I dont see kama haya yote yanahiyajika
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Jul 1, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Kama mmechangia billion 5 kwa simu, si lazima afanye retirement ya hizo fedha zenu?..sasa hayo ndiyo matumizi yake..asomaye na afahamu!
   
 4. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #4
  Jul 1, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,947
  Likes Received: 2,093
  Trophy Points: 280
  Mtoto akiwa na afya mbaya hata ukimvisha nguo mpya na nzuri kiasi gani hawezi kupendeza!
   
 5. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #5
  Jul 1, 2010
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  kazi za waswahili wa pwani ndo kama hivyo, kwa watu serious tulitegemea muda huu wa kampeni kufanyike midahalo ya kitaifa kuona ni namna gani tunaweza kuivusha hii Nchi katika lindi hili la umasikini lakini badala yake kampeni na hasa za ccm ni ushenzi mtupu wa kucheza ngoma na kushabikia pilau ikisindikizwa na bendi za muziki ama kweli watanzania tuendelee kudanganywa , leo julai mosi utaona mbwembwe za mkwere dodoma atakavyokata mauno akirudisha fomu za kugombea .
   
 6. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #6
  Jul 1, 2010
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160


  Duu Uongozi wa kisanii unatumia wasanii kuingia ikulu kisanii. Wanasubiri kuapishwa tu maana ushindi wameshaupata!!!! what a hell is this?
  TAMBWE, haya ni matusi kwa watanzania! Tunahitaji maendeleo na maisha bora ya wananchi siyo mchiriku na taarab. Hivyo vikundi ulivyovitaja vipo mitaani siku zote na wanaopenda kuburudishwa navyo wanavifuata kwenye maonyesho yao na hawaburudiki kwa kusikiliza nyimbo za ccm? Ndiyo maana uliondolewa CUF nini?
   
 7. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #7
  Jul 1, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Kicheckesho ni kwamba eti huyu mtu anaweza kuwaletea maisha bora watanzania!!!!!!!!! Better Idd Amin Dada than him
   
 8. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #8
  Jul 1, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  kweli mkwere ni mkwere tu.....
   
 9. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #9
  Jul 1, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135


  Yaani siasa za CCM mpaka kichefchef, yaani rais ajaye anachaguliwa na aliyepita. Kama walivyosema wachangiaji wengine taratibu za chama ni za nini kama inaeleweka ajaye atachaguliwa na huyu??????
   
 10. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #10
  Jul 1, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Mkuu hongera sana!

  Utaona hata kule kliniki mama anamficha hataki aonekane kwa wenzie! lol..............................Wazazi tunalifahamu hili!
   
 11. bona

  bona JF-Expert Member

  #11
  Jul 1, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  ukitaka mambo yako yakunyokee jiunge ccm - mkapa
   
 12. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #12
  Jul 1, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280

  Kwa hiyo ndo yananyooka kama hivi?
   
 13. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #13
  Jul 1, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Mungu tuhurumie, utuepushe na zimwi hili.

  Hivi hawa watu wamefika hatua ya kuongea rubbish in public this much?

  Tambwe Hiza bana!!! Lakini wakuu sishangai, angekuwa katibu mkuu ndo ingekuwa balaa.....

  Chama kimeja vijembe tu.... kazi wameshindwa.
   
 14. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #14
  Jul 1, 2010
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  I think there is a negative relationship between his age and this thinking capacity. The more he gets older the less his thinking capacity becomes
   
 15. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #15
  Jul 1, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  kazi ipo na tutashuhudia upuuzi mwingi tu zamu hii
   
 16. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #16
  Jul 1, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...Et tu, TMK Wanaume? CCM wanatumia umasikini na njaa za wasanii wetu kurudi madarakani. Nilidhani kuwa TMK Wanaume kwa ungangari wanaouonyesha jukwaani wa 'mapanga saa' wasingekubali upuuzi huu lakini ndio hivyo tena....:twitch: !
   
 17. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #17
  Jul 1, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  hakuna jinsi hapo inabidi vijana wetu wapiga ngoma wakubali tu,ndio njia ya kupata chakula.

  nawashauri wachukue hela zao na wamuimbe lakini wasimpigie kura.
   
 18. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #18
  Jul 5, 2010
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kama ccm ilifanya mazuri katika kipindi kilchopita ya nini haya yoto kwa mwenye akili timamu atagundua kua kunachofichwa CHEMA CHAJIUZA KIBAYA CHAJITEMBEZA Ningewashauri ccm katika kampeni zao wangechagua kikundi kimoja MJOMBA MRISHO MPWITO hiki kingelikua kioo kwa viongozi wa ccm na kujitizama nini waliahaidi na nini walifanya Vikundi vilivyotajwa hapo juu ni wazi wanafanya hivyo sio kwa ridhaa yao ni NJAA au WOGA ambapo ktt bongo kuipinga ccm ni kujichimbia kaburi.cccm UZURI SIO UREMBO WA KUNADI HADHARANI,KATIKA MAKAPU UZURI WA MTU NI TABIA NA HESHIMA YAKE MUNGU IBARIKI TANZANIA
   
 19. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #19
  Jul 5, 2010
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Wasaanii msikubali kutumiwa kama toilet PAPER au kwa tamaa kwani vitendo vyenu vya kuunga mkono CCM ambayo katika kipindi cha mwisho haijareta chochote kwa wanamziki mbali na KOMBA TOT ambacho ni kitengo cha ufisadi najua mnafanya biahashara lakini bihashara hiyo inaweza kuwatokea puani MNAPASHWA KUA KIO CHA JAMII NA SI VINGINEVYO MUNGU IBARIKI TANZANIA
   
Loading...