Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,710
- 40,777
KATIKA hatua inayoonyesha kuchoshwa na kunyanyaswa kila mara na vyombo vya dola, kikundi cha wafanyabiashara ndogondogo mjini hapa, jana walishusha bendera kadhaa za Chama Cha mapinduzi (CCM) na kuzichoma moto mbele ya askari polisi.
Mbali ya kuzichoma bendera hizo za CCM, machinga hao walisikika wakipiga kelele wakimtaja Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA) Kabwe Zitto, kwa madai kuwa ni mtetezi wa wanyonge na kumwomba aje Iringa kuona uonevui huo.
Machinga hao walichukua hatua hiyo majira ya asubuhi katika eneo la ofisi za CCM mkoa, wakipinga hatua ya uongozi wa Manispaa ya Iringa kuwavunjia vibanda vyao vya biashara.
Inadaiwa kuwa machinga hao ni wanachama wa CCM ambao walikuwa wamepandisha bendera hizo wakati wa ziara ya viongozi wa CCM taifa wakati wa ziara yao mkoani Iringa, waliyoifanya kwa lengo la kuelezea bajeti ya serikali na kukanusha madai ya ufisadi yaliyokuwa yametolewa na ushirika wa vyama vya upinzani dhidi ya viongozi kadhaa wa serikali.
Machinga hao walisema kuwa wameamua kuzichoma moto bendera hizo ili kuonyesha kuwa kuanzia wakati huo wao si wana CCM tena na wapo tayari kujiunga na upinzani kutokana na tabia ya CCM kuwageuka vijana baada ya uchaguzi kwisha.
Machinga hao walisema kuwa wamelazimika kuchoma moto bendera za CCM kutokana na unyanyasaji unaofanywa na viongozi hao wa manispaa.
Alisema yanayofanywa na manispaa hiyo, yanapingana na agizo la Rais Jakaya Kikwete, ambaye mara zote amekuwa akihimiza vijana kujiajiri katika sekta zisizo rasmi kama hizo, ambapo kwa kuwaunga mkono amekuwa akiwapa mikopo.
Walisema biashara hizo wanaziendesha kupitia mikopo kutoka kwa Rais Kikwete na kitendio cha kuvunjiwa mabanda yao wamekihesabu kama njama za kuwatafutia matatizo na serikali, hasa katika urejeshaji wa mikopo hiyo.
Kufuatia machinga hao kufanya fujo hizo kwa kuchoma moto bendera katikati ya barabara, magari yalilazimika kupita njia nyingine ili kukwepa moto huo, ambao ulikuwa umewashwa katikati ya barabara hiyo jirani kabisa na jengo la CCM mkoa na kufanya wanafunzi wanaosoma masomo ya ziada katika jengo la CCM kukatisha masomo na kutoka nje kushuhudia tukio hilo.
Eneo hilo ambalo Manispaa ya Iringa ilianza kuvunja vibanda jana ni lile ambalo viongozi wa vyama vinne vya upinzani wakiongozwa na Zitto walifanyia mkutano wao.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Albano Hokolola, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwa juhudi za kuwasaka waliohusika zinaendelea.
Ofisa Mipango Miji wa Manispaa ya Iringa, Godad Mwakalukwa, alipoulizwa na mwandishi wa habari hizi kuhusiana na zoezi hilo, hakuwa tayari kuzungumzia kwa wakati huo.
My Take:
Sikumbuki wakati wowote ambapo wananchi wamechoma bendera ya CCM au bendera yoyote ile ya chama cha siasa au ya Taifa. Kweli tumefikia hapa? Je, kuchoma bendera wakati Mkutano Mkuu unaendelea ni ujumbe au ni kutukana tu... tena mbele ya Polisi.. ?