Bendera ya CCM yachomwa na Wamachinga

ccm ni Chama kimoja kati ya vingi hapa Nchini japokuwa ni tawala.
Kuchoma bendera yake tena mbele ya vyombo vya dola ni utovu wa hali ya juu wa nidhamu, na ni kinyume kabisa na maadili ya Mtanzania. Nina hakika tukio hili halifahamiki na Watanzania walio wengi kwani lingelaaniwa hadharani. Ila hii ni changamoto kwamba kuna pengo la elimu sahihi kwa kundi hili. Ni jukumu la Watanzania wote bila kujali itikadi zao kulikemea hili kwa hali na mali tusije tukajikuta katika dimbwi la utawala usio wa sheria na wa kutovumiliana. Hakuna ubabe katika siasa unaoleta maendeleo bali nguvu ya hoja pekee.
 
Hao wamachinga wamekosa elimu gani?

kati yako wewe unayejiita unaelimu na waliochoma bendera kwa kukosa elimu yupi bora katika kutetea maslahi ya wanyonge?

Watu wengi hujidanganya eti wao wanaelimu hivyo ni wastaalabu huku wakilambishwa makombo elimu yenyewe ndiyo hiyo ya kufundishwa kusema ndiyo na kusaini mikataba mibovu.

Jambo lolote la uonevu halihitaji elimu ya shuleni ili ujue kama unaonewa siku hizi hata TV zinafundisha mambo mengi sana ya haki za binadamu

Tusifikiri wale wamachinga hawana elimu yawezekana kabisa wakazidi hata hao mnaojiita mna elimu. Kama nyiyi mna elimu na tatizo mnalifahamu toeni jawabu la tatizo hilo wao wameona hilo ni jawabu kwao no matter how

Wasomi wa nchi hii hamna msaada kwa taifa hili maana mashuleni mmefundishwa wizi mtupu

Tunaposema tatizo la nchi hii halijafikia lile la ungonvi wa waarabu na Marekani/israel tunakosea sisi liko zaidi ya hapo tena mbali sana angalieni madhara ya rushwa yanavyoua watu wengi kila leo na kuwaathili zaidi ya 80 percent ya watanzania ambao hata chai hawaijui lakini waarabu wanchoma bendera huku nymbani kwao kuna misosi tele, umeme, sofa nyumba safi nk
sisi tena tulitakiwa kuchoma zote nchi nzima
Chama ni watu unapotenganisha chama na watu unakosea kwamba sera za ccm nzuri lakini viongozi/waumini ni wabovu si kweli it must be either of the two kama sera ni mbovu na watu ni wazuri chama hicho ni kibovu au kama sera ni nzuri na watu ni wabovu chama hicho ni kibovu

Mungu ibariki Tanzania
 
swali la msingi, je wananchi katika kuonesha kuudhiwa na chama chochote cha siasa, wanayo haki ya Kikatiba ya kutoa maoni yao kwa kuchoma bendera ya chama, Katiba ya Chama n.k?

Mwanakijiji, katiba yetu inatoa haki kwa raia kufanya jambo lolote ambalo halisababishi uvunjifu wa amani! Kama wananchi walichoma bendera bila kumdhuru mtu mi naona sawa tu. Kama walichoma katiba (ya chama cha siasa) bila kupigana napo sawa, ila wakichoma katiba ya nchi watashatakiwa, ni kosa.
Watanzania wamefikia hatua hii baada ya kuna haki haitendeki. Tunajua kuwa maandamano yameruhusiwa ktk katiba ya nchi, lakini hawa vijana wakiandamana wanapigwa na polisi, sasa wakasemee wapi shida zao?
Ukiona wananchi wanavunja vituo vya polisi na kuwatoa watuhumiwa ujue kuna mushkeli mahali, ujue kuna haki potevu wanayoitafuta. Labda swali la kujiuliza ni kwamba, "Kwa nini tumefikia hatua hii?"
 
hili suali mnalizungumzia kwa kuangalia katiba ya nchi na ilani za vyama tu.na pia mnaonekana kujali amani ya nchi, ni vyema sana na niko pamoja na nyinyi.kuna walioangalia upande mmoja wa shilingi katika huu mjadala na kuna walioangalia upande wa pili. mimi acha niisimamishe shilingi sawasawa na acha mwenye kuhukumu aihukumu hii kesi. upande wa shilingi mliouangalia ni kuikubali katiba na kuamua kuwaita hawa vijana wahuni. masuali.
je mmejaribu kuzijadili hisia za hawa vijana?
je mmefatilia walifanywa nini hata wakaamua kuchoma bendera?
je alieanzisha huo mtafaruku wa kutaka kuvuruga hiyo amani tulionayo ni hawa wachoma bendera au ni hao wenye bendera?.

hao watu mie sijawaona kama ni wahuni ila picha yao inaniambia kwamba ni watu waliokatiliwa kuishi maisha waliostahili na zaidi ya yote wamepandishwa jazba na kitu fulani ambacho kiko dhahiri ndani ya nyuso zao.ni kipi? ----------
kumbukeni bendera ni tambara tu ambalo likichomwa litanunuliwa jipya hata siku ya pili.pia kumbukeni kwamba kuna vijana wengi ambao sehemu zao za kutafutia riziki wanafukuzwa na kukatiwa riziki zao za halali ambazo huwa wanawapatia familia zao na hatimae hubaki kunanga nanga mitaani. je hisia ya mtu kama huyu umeikisia itakuwa vipi?
alochoma tambara moto na alomzuilia mwenziwe riziki ni yupi anataka kuchafua amani?
au ndo tunafuata agano kwamba tukipigwa shavu la kulia tumgeuzie adui na la kushoto?
siwezi kuwahukumu hawa vijana kwa kuchoma tambara moto kwani najua hao wenye hilo tambara wana mengi ya udhalimu wanawafanyia wananchi, mengine yanaingia akilini na mengine ni ya kinyama.
naomba amani idumu kwa watanzania lakini pia tuzingatie kwamba kila anaeonewa ana hisia na kila mmoja ana njia yake ya kuzitawala hisia zake.kama wewe una subira alokosa subira usimwite "muhuni".
 
Madilu.
Mimi nadhani si kweli. Kuchoma Bendera ya SISIEMU ni majibu ya wanachama wa SISIEMU juu ya uadui uliotangazwa na chama chao wenyewe.Bendera imechomwa kama ishara ya Fukuto lililozidi ndani ya nyumba.
Bendera kuchomwa ni matokeo ya Siasa zao za kuwafanya watu wajinga kwa kuwapa ahadi hewa, zenye kuvunja sheria kwa makusudi na zisizo tekelezeka.
Haya ni mawazo yako lakini hayana ukweli ama hayakubaliki kifikra. Ni sawa na kumtesa mkeo kwa sababu tu ulitoa mahali na sasa yupo chini ya himaya yako, tena basi kwa kosa lilofanywa na wazazi wake. Pamoja na kwamba mfano huu ni mzito kuliko kuchoma bendera lakini muhimu kuitazama Bendera kama sio mali yako kwa thamani ya fedha uliyotoa.
Huwezi kupima thamani ya Bendera kwa kutumia fedha hata kidogo, mjomba hata kama umekosana na mamaa nyumbani unapochoma nguo zake hiyo haiwezi kuwa majibu ya uadui wa aina yeyote ila ni kuchanganyikiwa kwako kimawazo kiasi kwamba umeshindwa kufikiria zaidi. Na wala haiwezi kuwa ponya ya maradhi na frustration ila nafuu ya muda mfupi itakayokuponza baadaye.
Mara nyingi hali kama hii huwakuta watu ktk hali ya insanity na kuyafanya haya ghafla bila kutegemea yaani sii wao kifikra kwa muda wa tukio la hizo ahadi hewa. Lakini hawa vijana wameweza kwenda nunua kitambaa ama bendera wakarudi nayo na kuipiga kiberiti hadharani ni makusudi kabisa tena kwa ukosefu wa nidhani wa chama tawala na mfumo mzima wa vyama vingi.
Unapochoma kitu chochote ni kusema kwamba unakiondoa kitu kile ktk historia na mahusiano yako. Hata ukichoma picha za rafiki, familia ama ndugu ni kutuma message yenye ishara mbaya sana ktk mahusiano yako na hao watu.
Bendera ya CCM ipo juu zaidi ya mifano hii kwa hiyo unaweza pima mwenyewe kuwa kuchanganyikiwa kwako kutokana na ahadi hewa za baadhi viongozi hakuwezi kupata suluhu kwa kuichoma bendera hata kidogo...
Ugonvi kati yako na mkeo hakuwezi kupata suluhu kwa kuchoma chupi zake..hata kama alifanya ukahaba - Chupi zake hazikumfanya awe mzinifu.
 
Kuonyesha hasira kwa kuchoma moto kwangu mimi haionyeshi chochote zaidi ya ushabiki usiokuwa na maana. Kwanza wamesababibsha usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa barabara hiyo, pili usumbufu kwa wanafunzi waliokuwa wanasoma pamoja na hayo pia wamesababisha woga kwa wananchi wa eneo husika. Ingekuwa ni vyema na busara kwa HASIRA hiyo kuielekeza kwenye UPIGAJI KURA
MAPINDUZI YA KWELI hayaletwi kwenye kufanya fujo zisizo za msingi bali kwenye uwezo wa kupima wagombea wetu na kuchagua watu sahihi.
 
Hao wamachinga wamekosa elimu gani?

kati yako wewe unayejiita unaelimu na waliochoma bendera kwa kukosa elimu yupi bora katika kutetea maslahi ya wanyonge?

Watu wengi hujidanganya eti wao wanaelimu hivyo ni wastaalabu huku wakilambishwa makombo elimu yenyewe ndiyo hiyo ya kufundishwa kusema ndiyo na kusaini mikataba mibovu.

Jambo lolote la uonevu halihitaji elimu ya shuleni ili ujue kama unaonewa siku hizi hata TV zinafundisha mambo mengi sana ya haki za binadamu

Tusifikiri wale wamachinga hawana elimu yawezekana kabisa wakazidi hata hao mnaojiita mna elimu. Kama nyiyi mna elimu na tatizo mnalifahamu toeni jawabu la tatizo hilo wao wameona hilo ni jawabu kwao no matter how

Wasomi wa nchi hii hamna msaada kwa taifa hili maana mashuleni mmefundishwa wizi mtupu

Tunaposema tatizo la nchi hii halijafikia lile la ungonvi wa waarabu na Marekani/israel tunakosea sisi liko zaidi ya hapo tena mbali sana angalieni madhara ya rushwa yanavyoua watu wengi kila leo na kuwaathili zaidi ya 80 percent ya watanzania ambao hata chai hawaijui lakini waarabu wanchoma bendera huku nymbani kwao kuna misosi tele, umeme, sofa nyumba safi nk
sisi tena tulitakiwa kuchoma zote nchi nzima
Chama ni watu unapotenganisha chama na watu unakosea kwamba sera za ccm nzuri lakini viongozi/waumini ni wabovu si kweli it must be either of the two kama sera ni mbovu na watu ni wazuri chama hicho ni kibovu au kama sera ni nzuri na watu ni wabovu chama hicho ni kibovu

Mungu ibariki Tanzania

naanza kuona wapiganiaji wa kweli hapa jf. kijana umeongea kweli kuliko ukweli wenyewe .tukipata wenye mawazo kama yako basi nchi itakomboka .kwani hatujali elimu ,tunajali uadilifu.elimu ni muhimu kama mwenye elimu atatujali,kama hakutujali sisi hiyo elimu yake hatuna haja nayo.keep it up .ufunuo
 
Mkandara,

umesema ukweli lakini hukumalizia ukweli wote.

Ningekuwa na uwezo na thubutu ya kuchoma chupi za mke wangu, tena zile za bei mbaya kutoka Victoria Secret, jambo ambalo sina uwezo nalo kwa sababu yeye ndo Bread Winner wa familia ningezichoma nikiwa na nia ya kuhujumu mali.

Tendo hilo la kuchoma chupi za mke wangu nia na madhumuni yake yangekuwa ni kutaka mke wangu akienda kugawa uroda huko aendako asiwakoge waume wenzangu kwa chupi kali( Hasa zile za mtindo wa kaptula ya Bushmen katika Movie ya Gods Must be Crazy).
Nia ya kuchoma chupi au nguo za mke wangu ingekuwa ni kumfanya asiulambe.

Baada ya kuchoma chupi zake za bei mbaya ningemnunulia za kitambaa cha kijani au Bluu ambazo hangethubutu kuwaonyesha hawala zake tena.

Kuchoma Bendera ni Symbol ya resisatnce na ni kupeleka ujumbe mkali usio na utani ndani yake kwa chama husika bila kujali matokeo.

Kuchoma bendera kwao hawa vijana hakukua na nia ya kuhujumu mali za SISIEMU kam nia yangu ya kuchoma chupi za mke wangu, kwani wangetaka kuhujumu mali zao wanajua bendera si chochote na wala hazina thamani.

Wamechoma Symbol ya chama ili kuonyesha kupinga chama kiujumla. Tendo la kucham Bendera ya SISIEMU ni sawa na kumwandikia Bosi barua ya kumkashifu kwa kutumia Toilet Paper, ni matusi mara mbili

Inawezekana sheria haiko upande wao katika kuchoma bendera, Pengine kwa kukwepa sheria hiyo Wangeweza kuchambia bendera hizo na kuzitupa barabarani kuonyesha hasira zao.

Nia na madhumuni yao ni kupeleka ujumbe mkali wa Kisiasa ambao mimi wewe na wengine wengi inaoneka wazi tumeupata kisawa sawa.

Kama ni sawa au siyo sawa,kama ni utovu wa nidhamu au ni uvunjaji mkuu wa sheria na uvurugaji mkubwa wa AMANI NA UTULIVU.
Wao wamekwisha peleka ujumbe.

Kitendo cha kuchoma Bendera za SISIEMU kama ilivyo kuzomea viongozi wa SISIEMU kitasambaa hata hivyo msambazaji sitakuwa mimi.

Tendo walilolifanya hawa vijana la kuchoma Bendera litaingia kwenye historia ya mapambano ya kupinga Kudharauliwa kunyanyaswa na kupuuzwa na kundi la Watanzania wenzetu wenye kushika mpini.
 
Madilu,
Umenimaliza mzee wangu lakini bado hujafunika kabisa!
kinachomfanya mke huyu kugawa sio chupi na pili kinachokuuma zaidi bado kakibeba mwenyewe, mal;i sii yako mjomba!. Na kile kinachotakiwa na huyo mzinifu wa mkeo sio chupi yake hata akiwa uchi wa nyama mzee bado atafurahia ushindi...hiki ndicho chanzo na utatuzi wa zengwe hili unaanzia hapo sio ktk chupi.
Ndio hao viongozi wa CCM wanavyozidi kufurahia ushindi hadi huko Dodoma kwa sababu tumeshindwa ku attack the real issue...Mzee wangu ukisha fumania mkeo, nguo zake haziwezi kuwa suluhisho kwani fedha zimekwisha teketea, pili wewe kama machinga huwezi kumwambia kitu kuhusu Victoria secret ya mtumba hali mjomba pembeni huagiza toka Ulaya na zikaletwa tena kwa dozen kutokana na kodi yako.
Leo kila mmoja wetu hapa kaganda ktk TV, radio, JF kufahamu nani kaingia na nani nje tena wengine tunaomba jamaa zetu wawe ktk kundi hilo la Chukua Chako Mapema...

Kuchoma bendera ya CCM hakuwezi kubadilisha maamuzi ama maonezi ya hawa viongozi wa manispaa ila unazidi kuwapa sababu ya kuendeleza yale wanayoyafanya. Tumeyaona Kenya na South Afrika (Soweto) miezi michache tu iliyopita.
Kuna wale waliosema tujiulize kuhusu hawa machinga kilichosibu hasa kufikia wao kuchoma bendera hiyo. Kwanza
Kuhusu elimu zao, nadhani tutakubaliana kuwa elimu sio kukaa darasani ila ni matumizi yake ktk fani mbalimbali. Tunapata elimu ili kuweza kuitumia na sio elimu kwa sababu ya kujua kusoma na kuandika. Maamuzi kama haya ni dhahiri yanaonyesha upeo mdogo wa kielimu kifahamu chanzo na tiba ya gonjwa hili la viongozi wetu kutoa kutoa hadi za Uongo.
Maandamano hado ofisi za manispaa na kutinga ktk geti lao, kuwazomea na hata kusababisha wao wasiweze kufanya kazi siku hiyo ni somo kubwa sana kwa viongozi hao.
Mjomba Madilu dawa ya mke anayezini nje ni kumtafutia mkeo mwingne. CUF wapo Chadema wapo na wote hawa wanasubiri kura zenu kuwafanya wake zenu. Ama kama mapenzi yamezidi sana basi fumanizi linaweza kusaidia.. vishindo, mikwara na pengine hata makofi ya haraka haraka...(hilo kuvamia ofisi zao) pamoja na kwamba sio ustaarabu. Kama mkeo hataogopa basi jamaa mme mwenzako anaweza kuogopa na pengine kukomesha mawasiliano.
 
Nilitaka kutoa maoni, but then I changed my mind... nilikuwa nafikiria habari za mke wangu na chupi yake.. na hamu ya kutoa maoni ikanitoka kwani hakuna ambacho ningesema ambacho kingekuwa na sense hata kidogo.. carry on friends..! can you go a little deeper katika mafano yenu ili tuelewe as long as tusije tukapofuka macho with your use of vivid imagery!
 
Mwanakijiji,
Mzee wangu haya mambo tumeumbwa nayo hayana aibu wala hayakimbiwi...hayajakufika bado lakini pia nihoja ndani ya kutafuta suluhu kwani mbali na Utanzania tumeumbwa waume na wanawake...Longa tu mzee wangu kijiwe kipate nuru kidogo tumeganda sana hadi sura zinakomaa kwa matatizo... tunahitaji kucheka kidogo.
 
Hii ! Hii! Hii!

Ningependa kumwolea mke mwingine lakini ubavu huo sina, kwani mke wangu ndo mvaa pens humu ndani.
Hata leo hii tukiongeza kinda mie ndo wakuacha kibarua changu nikae kulea mtoto.
Ndiyo ni Dume, tena la mbegu lakini kwenye ubavu wa kiuchumi natoa mlio wa kubwekabweka kaa kale kajibwa aina ya Chihuahua kutoka Mexico.

Hili la kuchoma bendera hata Magwiji wa Modern Democracy, USA, bado haliwaingii akilini na hawajalijatolewa ufumbuzi.

Kuna Debate inaendelea hapa USA watu wanajiuliza ili uhesabike umechoma Bendera , bendera ni lazima iwe ya ukubwa gani.

Nikichoma bendera ya 1x1 sq inchi na nikichoma ya 36x60 sq in uzito ni mmoja?
Bendera karatasi, ubao au bati jepesi?
Benera ya Nylon au palstic Je?
Nikidesign software ikaonyesha nachoma bendera on line je?
Nikichoma bendera ilo tundikwa ofisini na ile niiwekayo sebuleni kwangu uzito bado ni mmoja?

Tuache kuchoma mambo ya kuchoma bendera.

Nikishona Chupi za Beendera ya Chama changu kwa sababu ya mapenzi juu ya chama changu nitakuwa nimevunja sheria?

Chupi hizo nikiziuza na kutoa sehemu ya mapato kwa cham changu?

Taulo la Bendera ya chama au taifa ni Ruksa? Pazia Je?

Nijuavyo mimi Chupi za Bendera ya Marekani ziko nyingi sana hata wakati mwingine Uncle Sam mwenyewe anatoka hadharani akiwa kavunja Chupi ya Bendera ya Marekani na nyota zake zote 50.

Walau wanngeruhusu kushona chupi zenye nembo ya Jembe na nyundo na maneno yasemayo Nambari One, wananchi tunaahidi tukizinunua hatutavaa hadharani.
 
Madilu Madilu Madilu !!
Mwenzio nitafukuzwa kazi leo kwa kucheka hapa ofisini!hiyo sentensi ya mwisho ni mwisho. tehe tehe !
 
Nilichojifunza katika taifa hili la Tanzania nio kuwa wataokuja kubadilisha historia ya nchi hii kutoka ktk hali mbaya tuliyonayo hadi ktk hali nzuri ni wale vijana ambao kila leo mnawasema hawana upeo/elimu/maarifa/ustaarabu/busara/ nk

Sisi tunaojidai tunaupeo/tumeelimika/tunabusara hatutaweza kwa kuwa tumeshagajigawa makundi mawili makuu

kundi la kwanza ni hilo la watu tunaowaita wahuni wasiokuwa na upeo ambao ndiyo hasa wanayaona madhara ya kuwa maskini, rushwa, ufisadi na ndiyo hao wanakula mlo mmoja kwa siku. Kundi hili hapo mwanzo lilikuwa linawaamini sana kundi la pili ambalo ni watu wanajiita wameelimika na kuwa na upeo kwamba wangeweza kuongoza mapambano zidi ya rushwa, ufisadi na klioogoza taifa ktk neema. lakini sasa hivi mtazamo huo haupo tena kwa kuwa wamebaini watu wanaosema wamesoma wanaupeo na wanabusara ndiyo hao wameungana na hao mafisai kuwaganadamiza wao maskini na walalaho manano yao yakiutetezi wanayoyadai hawa watu ni yanaishia ktk vinywa vyao tu lakini hakuna aliyeonyesha kwa vitendo kwamba kweli amechukizwa.

ndiyo kundi hili la wasomi ni la kwanza kubeza maamuzi yaliyochukuliwa na kindi la walalahoi wakati wao hawajawai kuchukua hatua yoyote ile kuonyesha kuwa kweli wmechukizwa na ufuska, ufisadi, rushwa ni mafundi wa kuongea tu na kufanya analysis zisizo na misingi/jawabu ya kutatua tatizo lenyewe.
Ukisema kuwa hawa watu wasubiri wakati wa kupiga kura wawanyime ccm ni sawa lakini kama ingekuwa ni suala tu la kusubiri kusingekuwa na chama chochote kupiga kampeni kwani ikumbukwe kwenye taarifa wamesema wao walikuwa ccm ni kuutangazia umma kuawa wao si ccm tena it is something else. Na watu wajue kuwa kunahaja ya kubadili mtazamo juu ya ccm ktk haya inayofanya kifupi maamuzi kama hayo in kampeni na kutoa taarifa kwa umma kuwa ccm wamefanya haya huku na Tz kupitia habari wajue.
Watu hawa walioelimika wakijiita ndiyo wanaongoza kutapeli bila hata huruma hawa maskini hata kama leo wanasema na kutetea maslahi ya wanyonge; hawa wengi wao wamebahatika kuwa na kazi wamepanga nyumba ina umeme,tv,sofa na wengine wamebahatika hata kujenga vibanda vyao na pengine kuwa hata na ka mark 2 amepack na hawa wliokuwa wanategemewa kuwa wanamapinduzi wameridhika wamestaarabika wameungana na mafisadi kazi kupiga domo pekee lakini kimsingi wanahofia tujumba twao

lakini mimi nasema Tz sasa inaelekea kutamu kwani waliogundua kuwa wanaonewa ni wale hasa wanaoonewa si pale mwanzo kuwa wliokuwa wanafahamu kuwa wanaonewa ni wale wasomi ambao kimsingi hawakuwa wanaoonewa;

Mungu akishasema ndiyo hakuna kiumbe chini ya mbingu kitasema hapana

Mungu ibariki Tanzania
 
CCM tunasafisha chama, haya yatapungua tu soon. Subirini matokeo ya KIZOTA

..i hope huo usafi unausema unafanyika kwa nia nzuri na si kupanga timu pekee[ni lazima timu ipangwe ili kabumbu lipigwe!]

..maana,inafahamika kuna watenda kadhaa hawataguswa na hii detergent!...sasa,hii italeta malalamiko na makundi!hilo unalifahamu!

..anyways,yetu macho!ila,nitafurahi nikiona ccm inasafishwa na kuwa proactive!isingoje isemwe mpaka iwe aibu!hata watoto wadogo wafahamu!hii ita-set standard hata kwa wapinzani siku[inshaallah!]watakapopata nao nafasi. kwasababu kwa mtindo wa sasa,hata wao wakipata leo mambo yao yatakuwa kama ya ccm and even worse!
 
mimi nadhani hata wale wanaojifanya kuangalia mambao kwa upande wa pili wa shilingi nao wanaangalia kwa macho ya makengeza

hawa vijana mnaowaita wahuni hapo walipoondolewa walipewa na viongozi wa CCM na viongozi hao kuwatumia kwa kutundika bendera za CCM wakati wa mikutano ya wapinzani

kwa wale msioijua Iringa hapo ni karibu kabisa na ofisi ya CCM mkoa wa Iringa na ni kwenye uwanja wa Mwenbetogwa ambao ndiyo "jangwani" ya Iringa
uhuni wa hawa vijana unakujaje wakati mwaka 2005 walikuwepo hapo na walitumiwa kuwazomea wapinzani? ina maana wakati huo hawakuwa wahuni?

pamoja na utetezi unaotolewa kwa kitendo cha kuchoma bendera(Hata mimi sikikubali)lakini hawa vijana walitakiwa wafanye nini wakati elimu waliyo nayo ni ya darasa la saba?

uhuni wao umekuwa uhuni kwa sababu tu wamechoma bendera ya CCM, mbona vijana hao walipotaka kulilipua gari la Mrema mwaka 2000 kwa kuziba kwa matambara kwenye bomba la kutolea moshi hawakuitwa wahuni?
 
Kidogo kidogo mambo yanaanza kupamba moto. Sijui CCM watawafunga wangapi.
 
Back
Top Bottom