Ben Saanane anavyoteseka na kivuli cha unafiki...

Ben Saanane anavyoteseka na kivuli cha unafiki...

At this point, wanne hawa, yaani zitto, mchange, exaud na ben mmepotoka, hatutaki wanachama kuona upuuzi huu hautusaidii huu huku tena, nendeni mkayamalize huko vikaoni busara hamna kabisa. Kwa nini hamumuigi Mnyika? Ni role model wa siasa zetu
 
At this point, wanne hawa, yaani zitto, mchange, exaud na ben mmepotoka, hatutaki wanachama kuona upuuzi huu hautusaidii huu huku tena, nendeni mkayamalize huko vikaoni busara hamna kabisa. Kwa nini hamumuigi Mnyika? Ni role model wa siasa zetu, acheni kuandika mnajiabisha watu wazima hoyo, nchi kwanza, chama kinafuata , ubinafsi wenu mwishoni
 
Mchezo anaoufanya ben saanane na mamuya naujua sana,ndio maana nipo kolikoli kuwaumbua hapa.Nasubiria jambo moja litamkwe na mm nipigilie king ya mwisho.
Namsapoti zitto hadi tone langu la mwisho kwasababu wamekuwa wakimsakama kuanzia gazeti la mwanahalisi ambalo linamilikiwa na mtu wa chadema na aliyeandika makala zote ni kiongozi wa juu wa chadema,lakini hawakumshinda zitto.
Wamekuwa na tabia ya kumtenga na kumsakama ili hali wao wana akadi za ccm nyuma.

mbona mnapenda kujivua nguo nyie? Au ndo miongoni mwa zile ID 20?
 
Nimesoma yote nimebaki nasikitika.
Ni lazima chama kiwaite wote waliotajwa kwani kuna ukweli kwa zaidi ya asilimia 85.
Swala la kusubiri eti kuletewa madai halisaidii.
Zitto Zuberi, Ben Saanane, Dr kitila mkumbo, habibu mchange, Juliana Shoza, Exaudi Mamuya, majina mengine ni ya badnia sijui ni akina nani ila najua hao wakiitwa watatajana.

Hatuwezi kuendelea kufanya kazi kwenye mazingira kama haya, lazima viongozi wa juu waelewe wazi kuwa chama sio hawa watu wachache inabidi wahojiwe na tupewe maelezo.

Kukaa kimya kwenye mambo kama haya kwa kutegemea natural course does not show leadership. Lazima viongozi wakubali kupamabana na haya mambo leo. Ufa uliopo ni mkubwa na wengine tunajua mengi sana hatutaki tu kuwa madomokaya.

Kuna watu ni wasomi lakini sio viongozi, tusichanganye degree , masters phd na uongozi. Uongozi ni karama, hekima, busara, utulivu , ushauri , uwajibikaji na kuweza kuhakikisha unalinda ulichoapa kukitumikia. Hawa wote waliotajwa wamevunja katiba ya chama na ikithibitika waliotajwa nayo ni ya kweli lazima adhabu stahiki ziwafuate. Nitashangaa sana kama tunaweza kuwahoji na kuwafukuza madiwani chama kikashindwa kutumia kipimo hicho hicho kwa hawa watu. Toxic.

Mwaka 2015 sio mbali tuyamalize haya matatizo leo ili mwenye maumivu yamuume sasa tufike 2015 na team safi yenye nia thabiti ya kumkomboa mtanzania.

Tamaa ya madaraka ya hawa wanaojiita vijana wasomi ndio inawaponza. Hawana shukrani wala hawana vision. Hawajui maana ya chama cha siasa. Mjumuiko huu wa watu wengi wenye fikra, akili, uwezo, nia na malengo tofauti hayahitaji ilmradi kiongozi bali yanahitaji kiongozi wa kweli mwenye record safi.

Nafurahi kwani itabidi wengine wasifike nchi ya ahadi kama Musa.

Chief Mkwawa wa kalenga.
Makundi ya vijana walafi yasiposhughulikiwa leo yatatuponza baadaye.
 
asante sana kamanda mchange kwakuleta huu ufafanuzi,maana haya uliyoyaandika ndiyo nilkiyotaka kuyatolea ufafanuzi japo bado nitatoa ufafanuzi wangu kuhusu hizi shutuma ambazo kwangu mimi nachokiona ni sawa na mtu kuchimba shimo halafu akatumbukia yeye mwenyewe,suala la ben kutumiwa kimkakati katika harakati zakumchafua zitto na sisi ambao wao hutuita masalia wala halijaanza leo,huu ni mkakati unaoratibiwa dhidi ya zitto pamoja na vijana ambao wanamuunga mkono zitto,nazidi kusisitiza kwamba ben saanane anatumia uongo kuuaminisha umma kwamba anamfahamu zitto kitu ambacho hata nafsi yake nina hakika inamsuta.ben acha kukimbia kivuli chako,sio rahisi kumchafua zitto kama unavyoweza kudhani,japo mnajitahidi sana lakini hamtofanikiwa.palipo ukweli uwongo hujitenga .
We ndo sijakuelewa kabisaaa.
Maana naona umeongea juu juu tu.
Kwanin usijibu hoja by hoja bibie??
 
Mchange, kwanza uandishi wako umekosa mtirriko mzuri wa mawazo hata kama kuna ukweli wowote kati ya unayoyazungumza itakuwa ngumu sana ujumbe wako kueleweka. Pili, naona unataka kujisafisha lakini hausafishiki. Ona hapa ulichoandika:

"2. Ni BEN SAA NANE ndiye aliyewashawishi na kuwalazimisha wenzie anaowasema leo ni wasaliti waunde kikundi. Hakuishia hapo, akakitunga mpaka na jina. Kuwa ni ‘’patriotic movement seven’’ na akakifupisha PM7.
3. Ni BEN SAA NANE ndiye aliyegawa majina ya kuitana miongoni mwa wana kikundi hiko, yeye akajipa jina la COBRA, mimi akanipa MDUDE "


Unajua nini Mchange, watu wote wenye akili hawawezi kukuamini kwa haya unayoyaandika. You are being too pretentious, unatungatunga tu vijistori vya kubumba na watu wengi waliojiunga humu JF ni watu wazima wenye akili zao, wanaweza kupembua pumba na mchele. Zako hizi ni pumba.

ninachoamini ktk siasa lolote laweza kutokea tena chini ya mwavuli wa uwajibikaji.
kama umefuatilia vyema mtanage huu utagundua kwaba ndani ya CHADEMA sasa kuna makundi 2 yaani kundi la zitto la kundi la Ben sasa hawa hawapikiki tena chungu kimoja.

acha tusikie mengi kutoka kwao na hapo ndipo watanzania watakapojua kwamba siasa zetu ni za majungu kuliko ukombozi wa taifa.
 
ninachojiuliza hivi viongozi wenu wa ngazi za juu like mwenyekiti na wengine wanajua kwamba ninyi mlitaka kuanzisha kundi la waasi la PM7?

Istoshe mbona kama siasa zenu zinataka kuchafua hata wale watu wachache ambao walikuwa safi kwenu na ambao watu waliweka matumaini kwao?? sasa kama CDM na BAVICHA yake mmeamua hadi kumchafua Dr Kitila Mkumbo mwafikiri mtabaki na nani tena??

nafikiri sasa Chadema inabidi kama chama wawaite na muhojiwe kila mmoja kwa jinsi yake na ukweli ujulikane. mnaharibu chama na kukidhoofisha.

hapa naomba ninukuu maneno ya mwanachadema mmoja maarufu aliyewah kusema 20 yrs to come CHADEMA iwill not be there. sijui aliona nn ila nataka kuamin kwamba aliona haya yatokeayo sasa.
 
Too much sasa, huu ni upuuzi. Mwanzisha thread hujui kujieleza,au sijui upo emotional. Ni udhaifu mkubwa kutokujibu hoja unakimbilia kuwachafua viongozi wa juu wa chama,unatapatapa viongozi wa juu wana muda wa kupambana na CCM sio kupambana na mwanachama wao. Mambo ya aibu sana haya, toa hoja, kama kumtetea Zito mtetee kwa hoja achana na maneno ya kumtafutia Zitto apate public sympathy hatutatui tatizo, by the way nasikitishwa na mahusiano yako na Ndg yngu Zitto (usifikiri kusema ZZK ni rafiki yako inatatua jambo, inaacha maswali mazito sana).. Kumbukeni, kila mtu ana nafasi na mchango wake chadema ila wenye mchango mkubwa ni wanachama, viongozi wanawakilisha wanachama na mawzo ya viongozi lazma yareflct mawazo ya wanachama.. Vijana acheni kutumika, kwenye historia hakuna msaliti aliefanikiwa katu. Dhambi ya usaliti itawatafuna vijana CHADEMA badala ya kupambana na CCM mnapambana na mwenyekiti na katibu, mmewahi kushauriww hapa ila humkusikia la muadhin wala la mnadi swala wengi mmeingiwa na roho ya Yuda Escariotte, Angalieni msije mkafika uchaguzi 2015 mkiwa majeruhi sababu mnagombania fito ilihali mnajenga nyumba moja!
 
NingeshangAa sana kutokuwaona masalia wakijitokeza kujaribu kupotosha ukwelu alosema kamanda Ben! Bwana Mchange we Zitto amekufanya kama kimada wake! Ni lazima uongee pumba hizi kujaribu kukinusuru kitumbua ambacho tayari kimeingia mchanga! Kama mnaona mnachafuliwa milango iko wazi kufikisha malalamiko kwa uongozi wa chama!
 
Mods ebu mwngalieni uyu TASWIRA ana utoto mwingi sidhani kama kasoma JF rules
 
Watu
wanafiki kama Ben
hawafai kushirikiana nao kwa jambo lolote,ni hatari kwa afya ya kikundi
chochote,viongozi wa siasa wasiwaendekeze wauza maneno kama
hawa,watawapoteza na kuleta migogoro isiyokuwepo,watu kama hawa ni
wakuwapuuza tu.



Lakini hii pia ni changamoto kuwa Chadema bado haijakomaa,kuwa na
makundi ndani ya chama chenye watu wenye akili timamu ni jambo
lisilozuilika,haiwezekani wote mkafikiri sawa,uongozi ni kuweza
kuwaunganisha wote hawa kwenye lengo la pamoja,ukishindwa hili na
kuegemea upande ni udhaifu kwa uongozi.

Huyu Ben Saanane matendo yake yanathibitisha kwamba ni mshirika mkubwa
wa Rama wa Ikulu, amekucha CDM kuhakikisha chama kinavurugika. Hivi kwa nini anakuwa active kupropagate migogoro? ivi ana cheo gani CDM? Kwa hili siwatetei wakina TUNTEMEKE lakini wao migogoro yao ni kuhusu uongozi.
 
What the f$##@#!!

Mzee Mwanakijiji alipokuwa akionya juu ya Viajana wanasiasa mimi nikawa nang'ang'ana kwamba vija wapewe nafasi waongoze nchi hasa ndani ya CHADEMA. Sikuwa najua kwamba vijana ndani ya CHADEMA ni wa hovyo kiasi hiki: Uchawi, Uongo, Unafiki, Usalaiti, Uasi, Majungu, Uzandiki, kutaka kuuana, nk. Hizi ndizo sifa za vijana wa leo! Kwisha habari yenu
 
kwenye thread kama hizi huwa na baki msomaji lakini niseme wazi Mchange umeshikwa..
 
Hivi kwa nini ni ZITTO+Mchange+Shonza+Tumteneke na si kina Lissu,Mnyika,Nyerere,Mbilinyi,Mdee e.t.c?kuna nini kimejificha juu ya ZITTO?mwenye akili hapati shida kugundua pumba na mchele,hizi thread mnazoleta humu haziweza wasafisha wale walio wachafu na wanafiki!bora hata yule aliyekiri wazi na kugundua kua alipotoka na kutubu hivyo hadharani kuliko wanafiki wanaotaka kulazimisha vichwa vya watu viamini uongo na unafiki wao ulio wazi!uzuri wa mnafiki ulipwa hapa hapa duniani!mtu alitaka uongozi kwa rushwa na ushaidi ukawa wazi nae atajitokeza na kusema yeye ni MSAFI?ebu waheshimuni Watanzania nyie,Watanzania sio wazito wa kufikiri na wajinga kiasi hiko!wenye uelewa wataendelea kuelewa,na washadadiaji watabaki kushadadia!
 
zitto hasafiki ni sawa na kusafisha kanzu na MKAA
Mwanahalisi walimshamchunguza wakamweka wazi kwa uongo wake dhidi ya mwanahalisi tukamjua ashukuru ujinga wa tz ukampumbaza akajiona bado anaaminiwa
Kakutuma uje umsafishe na mkaa nawe umekubali
Ben, Mamuya Mwanahalisi atajuta kuwafahamu
Nawashauri na kundi lenu muache kutujazia server kwa kutetea usaliti, unafiki dhidi ya chama ambacho ni TUMAINI LA WATANZANIA
Mmedanganya sana ila msidhani mnaweza danganya watu wote kwa wakati mmoja na njia ya mwongo fupi
 
Hii thread haina hoja zaidi ni masalia kukurupuana na ID kibao kumtusi Ben!

mnapewa hadi majina nyie mpo tu! viapo?

Thread ya jana ina nyama hii ni matusi kwa Ben tu hamna hoja!
 
Siasa za CHADEMA ni za gombania goli,ni swali la kujiuliza watanzania kuna maslahi gani katika kuanzisha makundi kama M4C,CHALEMA,PM7,TUNTEMEKE CO LTD na mengineyo mengi.Sisiti kusema kuwa uongozi wa juu ni dhaifu kwani wanamchango mkubwa katika kuukuza huu mgogoro.
 
Back
Top Bottom