Ben Pol aomba Talaka Mahakamani dhidi ya Mke wake Anerlisa

Slowly

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
5,821
2,000
Anaandika Millard Ayo
"Mwimbaji Staa wa Bongofleva Ben Pol amefungua shauri la talaka Mahakamani dhidi ya Mke wake Anerlisa ambae ni Raia wa Kenya ambapo kwa mujibu wa taarifa kutoka chanzo cha kuaminika kilichoongea na millardayo.com shauri hilo limefunguliwa na Benard Paul Mnyang’anga katika Mahakama moja ya Mwanzo Jijini Dar es salaam, hata hivyo bado haijafahamika sababu za Mwimbaji huyu kuamua kuivunja ndoa hiyo.

Ben Pol na Anerlisa walifunga ndoa mwishoni mwa mwezi May mwaka 2020 katika Kanisa Katoliki la St. Gaspar Mbezi Beach, Dar es salaam na kuhudhuriwa na Watu wachache kutoka upande wa familia zote mbili pamoja na Marafiki wachache wa karibu wa familia."


Ni nini kimemkumba mwamba , au anataka mabillion ya Anerlisa , au kachapiwa ?? Ikumbukwe penzi hili ni kama lilimtoa mwamba kwenye ramani ya mziki....

"Usifanye makosa kumwacha mwanamke aliyekamilika sababu ya mwanamke mzuri " by Billnas
 

Asprin

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
63,954
2,000
Walifunga kanisani? Mbn sielewi au Mimi ndy nipo nyuma ya wakati

Si nilisikia benpol kabadili Dini kawa muislamu na na huyo mkewe wamefunga ndoa ya kiislamu

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
Labda alibadili dini baada ya kuoa...

Bibie akawa anampakulia kitimoto kwa siri mpaka aliposhtuka kuona pua ya kitimoto kwenye mchuzi...
 

Watu8

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
56,353
2,000
Walifunga kanisani? Mbn sielewi au Mimi ndy nipo nyuma ya wakati

Si nilisikia benpol kabadili Dini kawa muislamu na na huyo mkewe wamefunga ndoa ya kiislamu

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
Mkuu hawa wasanii ukianza fuatilia ishu zao unaweza dhani ni aliens walioshushwa toka sayari za mbali...

Jamaa alifunga ndoa kanisani, fews months later akatosana na mkewe, then akabadili dini na jina, then akapatana na mkewe na sasa mambo ya talaka...Haya yote yametokea maybe in a year or less
 

Watu8

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
56,353
2,000
Wajuvi watufungue kati ya Ben pol na huyu mkenya ni nani atapoteza zaidi baada ya mgawanyo wa mali ?
Kila mtu atakula hamsini zake...

Labda kama kuna walichochuma pamoja ndani ya huo muda waliokuwa wanandoa, mahakama ndio ya kuamua nani apate nini baada ya kusikiza pande zote...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom