Bei ya vyakula "Kilimanjaro Fast Food" pale Mombo si rafiki

NGURI PORI

JF-Expert Member
Oct 29, 2011
3,053
3,259
Ukiwa njiani kuelekea Arusha-Dsm/ Dsm-Arusha .. sasa Magari Mengi yanapita Pale Hotel Mpya Ya Kilimanjaro.

Hakika Bei ya Vyakula waliyoweka Si Rafiki kabisa Kwa msafiri na nnadhani wanakomoa kwa Vile Msafiri anakua hana Option Mbadala.

COUPON YA CHIPS KUKU POTION /NYAMA FINYANGO TANO NI Tsh 7000/=

Kumbuka Kuku wanamgawa mara nne.

MISHKAKI YENYE VINYANGO NNE HAFIFU NI TSH 2000/=.

SAMBUSA/MAANDAZI NI TSH 2000/=
Utaishia kicheka ukiziona.
Imepelekea mpaka wale jamaa wanaouza matunda maeneo yale nao kua na Bei Juu .
Kamfuko ka Machungwa ni Tsh 5000/= . ...
Ipo haja ya Bei hizi kuingiliwa na mamlaka husika , wakiachiwa ipo siku tutauziwa andazi Tsh 5000/=
Na wasipolitizama Hili kwa Haraka , italeta Athari mpaka kwnye magari yanayopita pale.
087cbc8680fe2ac39dd9750bcbd15b69.jpg
 
Naam, bei yapo ipo juu kutokana na ubora pamoja na uhakika wa vyakula vyao.

Mimi huwa nikipita pale nakula huku najiamini kabisa. Nachukua Coupon yangu ya kule kwenye vyakula mchanganyiko, napiga pyuu alafu napanda kwa gari kupumzika. Sina wasiwasi kabisa...

Kama KILIMANJARO MOTORWAY FAST FOOD ni ghali, jaribu kwingine.
 
Watu hatujielewi tu, we usihangaike na mtu muache na vyakula vyake.
Cha kufanya ukijua unasafiri mwambie mama watoto akutayarishie dry food kama halfcakes, maandazi, kuna vidude flani wanaita vikokoto safi sana kwa safari, usisahau kununua soda yako au hata juice ya azam mango hapo mtaani kwenu maana ukinunua hoteli ya njiani bei yake ni balaa.

Tutawanyoosha wauza vyakula njiani tuache kuwalea wanapandisha bei kiholea ili kupata super profit kwa kua wanajua hatuna option.

Tujipange ukienda safarini kula kwenye hotel zao acha.
 
Naam, bei yapo ipo juu kutokana na ubora pamoja na uhakika wa vyakula vyao.

Mimi huwa nikipita pale nakula huku najiamini kabisa. Nachukua Coupon yangu ya kule kwenye vyakula mchanganyiko, napiga pyuu alafu napanda kwa gari kupumzika. Sina wasiwasi kabisa...

Kama KILIMANJARO MOTORWAY FAST FOOD ni ghali, jaribu kwingine.

Hujielewi kakwambia bus linakupeleka kwa lazima we unasema ajaribu kwingine kivipi na hotel ni moja hiyo hiyo.

Hizi hotel zitofautishe chakula cha watalii / wenye pesa zao na watu wa kawaida, kama vipi watenge VIP na kawaida ili kutoumiza watu maana unajikuta tu bus limesimama hapo
 
Watu hatujielewi tu, we usihangaike na mtu muache na vyakula vyake.
Cha kufanya ukijua unasafiri mwambie mama watoto akutayarishie dry food kama halfcakes, maandazi, kuna vidude flani wanaita vikokoto safi sana kwa safari, usisahau kununua soda yako au hata juice ya azam mango hapo mtaani kwenu maana ukinunua hoteli ya njian bei yake ni balaa.

Tutawanyoosha wauza vyakula njiani tuache kuwalea wanapandisha bei kiholea ili kupata super profit kwa kua wanajua hatuna option.

Tujipange ukienda safarini kula kwenye hotel zao acha.
Kabisaaaaa mkuu, binafsi sihangaikagi na vyakula vya njiani najiandaliaga mwenyewe nyumbani, tukifika sehem ya kula nitashuka kunyoosha miguu basi
 
Kilimanjaro, Arusha ni kwa ma fogo (Mabillioner) wanauza bei kulingana na quality ya chakula halafu mbona n bei ya kawaida..... nenda KFC Ukaulize bei ya vyakula kule.......

Au kama bei ni ghali panda magari ya kuelekea Chato bei za hotel za huko ni sawa na bure
 
Kuna comments huwa zinatolewa hapa JF zinaashiria kila mtu ana uchumi wa kati au ni tajiri kabisa cha ajabu ukienda jukwaa la nafasi za kazi unakuta kaanzisha uzi anatafuta kazi yoyote halali.

Ni vema tutambue taifa lina watu wenye uchumi tofauti tofauti sasa tukisema nenda KFC hivi watanzania wangapi wanaweza kwenda? Au wenzetu mliopata pesa mnaona tusio nazo ni uzembe?

Maslahi ya wengi ndio maslahi yanayopaswa kuzungumziwa sio maslahi ya watu wachache wenye pesa nyingi.
 
Kuna comments hua zinatolewa hapa jf zinaashiria kila mtu ana uchumi wa kati au ni tajiri kabisa cha ajabu ukienda jukwaa la nafasi za kazi unakuta kaanzisha uzi anatafuta kazi yoyote halali.

Ni vema tutambue taifa lina watu wenye uchumi tofauti tofauti sasa tukisema nenda KFC hivi watanzania wangapi wanaweza kwenda? Au wenzetu mliopata pesa mnaona tusio nazo ni uzembe?

Maslahi ya wengi ndio maslahi yanayopaswa kuzungumziwa sio maslahi ya watu wachache wenye pesa nyingi.
Hahahahah Ahsante sana Kaka...Ujumbe Umewafikia.
 
Back
Top Bottom