Bei ya ufuta mwaka huu ni majanga

Bei ya ufuta mwaka huu ni majanga

Nilishalima Ufuta, Nilitumia gharama kubwa, Bei yake ya 2500 per kilo iliniuzi sana, Mwaka huu sijalima.
Mazao Mazuri sasa ni Tikiti, Mihogo na Mengineyo.
 
Hali zenu wanajamvi?

Anaandika steka toka kusini, wadau zao la ufuta ni nguzo muhimu kwa uchumi wa mikoa ya kusini hasa mkoa wa Lindi, tulizoea kuuza zao hili kwa bei ya sh 2000-2500/ cha ajabu mwaka huu limeshuka kati ya sh 1500-1700/ kila mtu analaani mfumo na pia wanajaribu kuhamasishana wasiuze kwa hiyo bei ila watu wana dhiki zao hivyo hulazimika kuuza tu huku nyuso na mioyo yao ikiwa imekunja na leo ukijaribu kwenda kule na kale kawimbo ketu cha mbele kwa mbele utarudi jina, karibuni sana kusini mje kula ming'oko.
Ni wilaya gani unapatikana huo ufuta nije kukusanya kidogo?
 
" karibuni sana kusini mje kula ming'oko"
hiki kimekuwa chakula cha wageni? bora ungetukaribisha chipweng'e!
 
Yaani kule dodoma kwa mfano mwaka jana kilo iliuzwa hadi 3500 ila kwasasa wakulima wanalia ovyo na bei ya ufuta.

Sio kweli, ufuta wa dodoma haujawahi kuuzwa sio tu 3500 hata 2500 haujawahi kufika....
 
Kilimo ndio fursa yenye tija kubwa kwa sasa na siku za usoni! Ila usilime kwa kujaribu au kwa mkupuo mmoja utarajie kupata faida ya kusimulia miaka yote!
 
Back
Top Bottom