Shusha BEI ya bidhaa zako kabla hujalazimishwa kushusha na Mpinzani wako

CONTROLA

JF-Expert Member
Sep 15, 2019
6,939
22,955
Katika biashara kila mfanyabiashara anafanya biashara yake kwa namna alivyowekeza pesa zake,muda na akili yake eneo hilo.

Baada ya kujua pesa aliyowekeza,muda aliotumia,gharama zote mpaka bidhaa inamfikia mteja ndipo mfanyabiashara hupanga bei ya bidhaa zake.

Wafanyabiashara wengi 80% sio waaminifu kwenye upangaji wa bei zao,wengi katika kundi hili hupanga bei kwa tamaaa na namna uhitaji wa kile kitu ulivyo na wala hawaaangaliii mteja anafaidikaje (wengi hujiangalia wao tu,kwenye bei).

Leo naomba niwashtue ndugu zangu tamaa mbele kwenye swala la bei.

Kila mtu anapenda kudumu katika biashara yake,ukiona mtu kadumu ktika biashara yake mwaka wa 1 2 3 na kuendelea yupo pale pale,Frem ile ile,kibanda kile kile wanakuja wengine wanamkuta wanamuacha,yeye bado yupo sio kila mtu ni mchawi/mshirikina Uchawi wa biashara yako ni BEI.

Acha tamaa kitu kama umekinunua 500 sio lazima uuze 1000 unaweza ukanunua kitu 500 ukamuuzia mteja 600 bado sh 100 n kubwa ktk biashara.

Usipofanya wewe,atakuja mpinzani wako ambae kwake yeye 100 ni nyingi sana, kitu ulichokua ukiuza 600 mwenzako atauza 550, kitu ulichokua ukiuza 1000 mwenzako atauza 600, Atakapo kuja mpinzani wako wa namna hiyo atakuchukulia wateja almost wote.

Atakuacha na wateja wale wanaokujaga kuku kopa TU,ila wateja wanaotoa cash huwa wanaenda penye unafuu wa bei,Kuwa makini sana na bei ya bidhaa zako.

Kuna wafanyabiashara wao target yao ktk faida ni sh 500 tu, wakati wewe target yako umejiwekea sh 2000 kwa bidhaa, acha tamaa ni heri shilingi 50 ya kila siku kuliko shilingi 2000 ya mara 1 kwa wiki.

Usikae na bidhaa muda mrefu shusha bei ukimbizane na soko,vitu vipya vinatoka kila siku Acha kuganda na bidhaa za miezi miaka imepita wewe bado uko nazo tu.

Usikubali mpinzani akakuyumbisha,kuwa makini sana ktka upangaji wa bei ya vitu unavyouza, hakikisha umepunguza bei chini hata akitokea mpinzani wako Akupite kwa vingine ila sio BEI.

yawezekana yeye ana mtaji amepanga frem,kaipamba,kairemba lakini siku zote wateja hufata huduma na wala sio uzuri wa jengo (japo kuna biashara muonekano huchangia kuleta wateja) lakini hizi zingine wateja hawajali wao wanachojali ni Huduma na Bei rafiki.

Kwa hiyo kama unaweza anza leo,anza sasa shusha bei uwe wa tofauti na wengine jiwekee mazingira mazuri ya kusurvive ktk biashara yako.

Umeshawahi kwenda duka lolote customer care yao mbovuuu,ukiuliza unajibiwa hovyooo lakini wateja hawakauki? unahisi ni uchawi au wameloga? Jibu ni HAPANA uchawi ni bei, utaenda wapi upate bei yao,utaingia duka gani ukutane na punguzo wanalotooa,hakuna.

Acha kuhangaika na waganga na ushirikina,hakuna mteja anae enda sehemu inayouza vtu vya gharama wakati kitu hcho hcho cha ubora huo huo anaweza kukipata kwa bei ya chini.

Changa karata zako vizuri,maswala ya kuuza vitu bei za juu ulimwengu huu uliojaa wafayabiashara kila robo hatua, sio kabisa ni kujichimbia kaburi lako mwenyewe ambalo siku 1 utadumbukia na watakufukia na kusahaulika ktk biashara.

Usiruhusu Mgeni akupige K.O tengeneza mazingira magumu kwa kila anaetaka kufanya/kuanzisha biashara kama yako eneo ulilopo.
 
Leo nami nimecomet bado kuandika nami uzi wangu! Niliwahi kufanya biashara ya hivo, ni kweli utaongeza idadi ya wateja tena wengine watapita huduma kadhaa kama za kwako na kukujia tu. Ila changamoto zake uwe na uhakika wa kuuza vitu vingi kwa siku
 
Kuna sehemu ukiuza vitu bei cheap sana wateja hawanunui kuhofia kama ni fake!,halafu hizo faida za 100 tsh ni kwa wale wenye mitaji kuanzia milioni 200 na kuendelea,sasa wewe unajitafuta ukuze mtaji na vifaida vya 500 itakuchukua karne mbili!kutoboa
Yaani mtaji wa milioni 10 halafu kodi ya pango iwe milioni kwa mwezi na ijiwekee vifaida uchwara vya 500tsh utaenjoy show!
Binafsi biashara zangu ni za double double tu sifanyi biashara kufurahisha wazalendo
 
Back
Top Bottom