Bei ya ufuta mwaka huu ni majanga

stweka

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
422
144
Hali zenu wanajamvi?

Anaandika steka toka kusini, wadau zao la ufuta ni nguzo muhimu kwa uchumi wa mikoa ya kusini hasa mkoa wa Lindi, tulizoea kuuza zao hili kwa bei ya sh 2000-2500/ cha ajabu mwaka huu limeshuka kati ya sh 1500-1700/ kila mtu analaani mfumo na pia wanajaribu kuhamasishana wasiuze kwa hiyo bei ila watu wana dhiki zao hivyo hulazimika kuuza tu huku nyuso na mioyo yao ikiwa imekunja na leo ukijaribu kwenda kule na kale kawimbo ketu cha mbele kwa mbele utarudi jina, karibuni sana kusini mje kula ming'oko.
 
mbona umeandika kichochezi? sasa bei ya ufuta na wimbo wa mbele kwa mbele vina uhusiano gani kwani ccm ndio inanunua huo ufuta? kama umedoda huko kwa wakubwa wenye soko la dunia ulitaka hao mbele kwa mbele ndio wanunue?
 
Ulikuwa mwaka wa vyakula, sababu maeneo mengi nchini mvua zilikuwepo zakutosha hivyo wakulima walilima mazao mengi sana, kwa mfano mwaka jana huku kwetu mchele ulikuwa 1800-2200 ila kwa sasa mchele ni 800-1100 kwa kilo moja.
 
Hali zenu wanajamvi?

Anaandika steka toka kusini,wadau zao la ufuta ni nguzo muhimu kwa uchumi wa mikoa ya kusini hasa mkoa wa Lindi,tulizoea kuuza zao hili kwa bei ya sh 2000-2500/ cha ajabu mwaka huu limeshuka na watu huu za kati ya sh 1500-1700/ kila mtu analaani mfumo na pia wanajaribu kuhamasishana wasiuze kwa hiyo bei ila watu wanaziki zao hivyo hulazimika kuuza tu huku nyuso na mioyo yao ikiwa imekunja,na leo ukijaribu kwenda kule na kale kawimbo ketu cha mbele kwa mbele utarudi jina,karibuni sana kusini mje kula ming'oko.
Jaribu kuvumilia labda bei itapanda teh teh teh
 
mbona umeandika kichochezi? sasa bei ya ufuta na wimbo wa mbele kwa mbele vina uhusiano gani..kwani ccm ndio inanunua huo ufuta? kama umedoda huko kwa wakubwa wenye soko la dunia ulitaka hao mbele kwa mbele ndio wanunue?
Kweli kama hataki kuuza aukaange atengeneze kashata
 
Ulikuwa mwaka wa vyakula, sababu maeneo mengi nchini mvua zilikuwepo zakutosha hivyo wakulima walilima mazao mengi sana, kwa mfano mwaka jana huku kwetu mchele ulikuwa 1800-2200 ila kwa sasa mchele ni 800-1100 kwa kilo moja.
Samahani mkuu,
Huko kwenu bei ya mahindi ikoje na ni wapi huko?
 
Yaani kule dodoma kwa mfano mwaka jana kilo iliuzwa hadi 3500 ila kwasasa wakulima wanalia ovyo na bei ya ufuta.
 
samahan wanajamv naomba kujua bei ya ufuta,ulezi,mbaazi na mtama katika soko ka taifa na la kimataifa
 
Hali zenu wanajamvi?

Anaandika steka toka kusini, wadau zao la ufuta ni nguzo muhimu kwa uchumi wa mikoa ya kusini hasa mkoa wa Lindi, tulizoea kuuza zao hili kwa bei ya sh 2000-2500/ cha ajabu mwaka huu limeshuka kati ya sh 1500-1700/ kila mtu analaani mfumo na pia wanajaribu kuhamasishana wasiuze kwa hiyo bei ila watu wana dhiki zao hivyo hulazimika kuuza tu huku nyuso na mioyo yao ikiwa imekunja na leo ukijaribu kwenda kule na kale kawimbo ketu cha mbele kwa mbele utarudi jina, karibuni sana kusini mje kula ming'oko.
isee nilisikia bei elekezi ni sh.2200,lakini ufuta una tabia ya kushuka bei ule wa mwanzo,ule wa mwisho mwisho bei inapanda
 
Anayedhani kilimo kitatutoa katika lindi la umasikini anaota,yaani ukilima ni hasara tupu mwisho wa Sikh.Mchuuzi ndiye hufaidika
 
Back
Top Bottom