Sisi wananchi tilifurahi sana tuliposikia kuwa Serikali imetoa bei elekezi ya sukari kuwa Tshs.1,800 kwa kilo. Hapo awali bei ya sukari ilikuwa wastani wa Tshs. 2,200 na wananchi tuliizoea. Leo hii bei ya sukari imepaa mpaka wastani wa Tshs.2,400 - 2,500. Sisi wananchi tunajiuliza Serikali ilipotoa bei elekezi haikufanya utafiti?. Je wafanyabiashara wanaopandisha bei ya sukari nani ni mkubwa,Serikali au wafanyabiashara?. Ni afadhali tununue sukari kwa bei tulioizoea kuliko bei ya sasa. Sisi wananchi tunakosa iani na Serikali kuhusu bei ya sukari.