Shindu Namwaka
JF-Expert Member
- Sep 22, 2014
- 4,911
- 3,083
Ikiwa serikali imetoa tamko la sukari kushuka bei kufikia sh.1800 kwa gk1 bado bidhaa hiyo tunanunua sh.2200 kwa wateja wa reja reja wakati wateja wa jumla wakinunua sh.50000 hadi sh.49000 kwa kg25.
Ni wazi kuwa sukari sasa imezidi kupaa bei kila uchao, sehemu nyingi sasa bei ni elfu 3 kwa kilo, maamuzi ya Rais wetu mpendwa Magufuli naona aliya fanya haraka mno,wananchi wa chini sasa ndo wanaoumia zaidi.
Badala ya kupata unafuu ulikusudiwa sasa linaelekea kuwa janga. Najiuliza hapo ni sukari tu je angetangaza kupiga marufuku kuagiza na bidhaa zingine hali ingekuwaje? Kama sukari tu imeleta shida.