Kilo ya sukari Tsh. 3000 wakati sukari kutoka Zambia ni Tsh 2000 mnaizuia

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
11,975
48,843
Hii nchi ni ngumu sana kuielewa Sukari kutoka Zambia inauzwa 2000-2200 lakini cha kushangaza wanashindwa kuweka utaratibu wa Sukari kuingia.

Wanawakamata wateja ambao wameshanunua Sukari wakiwa ndani ya Tanzania.

Yaani unamkamata mtu kisa kabeba kilo moja ya Sukari kwenye basi? Hivi tuna serikali kweli hapa?

Sasa unajiuliza tunakwama wapi? Serikali ipo imeshindwa kutoa ruzuku kwenye viwanda vya ndani angalau sukari ipatikane kwa 1800?

Kama Sukari haitoshelezi mahitaji kwanini viwanda vya ndani visiagize vyenyewe Sukari na kuuza bei ya around 2000?

Inakuwaje Sukari kutoka nje inakuwa na bei ndogo halafu ya ndani inakuwa na bei kubwa tuna tatizo kama nchi inaonyesha hatuwezi biashara.

Haya ndio mambo sasa serikari inatakiwa kuyafanyia kazi.

Kama mambo yanayowahusu wananchi wa chini serikali haiwezi kuyafanyia kazi.

Basi hatuna serikali.
 
Hii nchi ni ngumu sana kuielewa Sukari kutoka Zambia inauzwa 2000-2200 lakini cha kushangaza wanashindwa kuweka utaratibu wa Sukari kuingia .

Wanawakamata wateja ambao wameshanunua Sukari wakiwa ndani ya Tanzania

Yaani unamkamata mtu kisa kabeba kilo moja ya Sukari kwenye basi? Hivi tuna serikali kweli hapa?

Sasa unajiuliza tunakwama wapi? Serikali ipo imeshindwa kutoa ruzuku kwenye viwanda vya ndani angalau sukari ipatikane kwa 1800?

Kama Sukari haitoshelezi mahitaji kwanini viwanda vya ndani visiagize vyenyewe Sukari na kuuza bei ya around 2000?

Inakuwaje Sukari kutoka nje inakuwa na bei ndogo halafu ya ndani inakuwa na bei kubwa tuna tatizo kama nchi inaonyesha hatuwezi biashara.

Haya ndio mambo sasa serikari inatakiwa kuyafanyia kazi

Kama mambo yanayowahusu wananchi wa chini serikali haiwezi kuyafanyia kazi ..

Basi hatuna serikali.
We acha tu mkuu
 
Protectionism inaumiza mamilioni ya wananchi at the expense ya kulinda maslahi ya wachache ambao ni wamiliki wa viwanda vya ndani na wale walioajiriwa, maana yake ni kwamba unaumiza watu milioni 55 ili ulinde maslahi ya wamiliki watano wa viwanda na wafanyakazi wasiofika mia tatu. Haiingii akilini sukari inaweza kupatikana kwa sh. 2000, wewe unalazimisha watu wanunue ile ya 3000 kisa inazalishwa ndani, ni kitu gani kinafanya hao wazalishaji wa ndani wasiboreshe strategy zao washindane kwenye soko?
 
Tatizo hao wamiliki wa hivyo viwanda ni wafadhili wa CCM wakati wa kampeni za uchaguzi.
 
Lazima ilinde viwanda vya ndani. Ikiruhusu tu, mtibwa sugar, kagera sugar, tppc nk azam. Vifungwe, walioajiliwa huko warudi makwao kisa kukufurahisha wewe mura, tata. Unafikiria tumbo rako mura
Kati ya viwanda na watanzania nani ni bora?.
 
Kama nchi zote zinazotuzunguka sukari ipo bei ya chini kwanini sukari yetu inakuwa bei juu, tatizo hivi viwanda wanahisa ni viongozi wanajifanya kuvilinda kumbe wanalinda maslahi yao.
 
Mngejua kitu kimoja.Hakuna nchi iliyoendelea kwa kuimport bila kuwa na viwanda vya ndani.
Pili tunaita mnyororo wa thamani. Kiwanda kinavyozalisha, kitalipia umeme, maji, land rent, kodi,
Wataajili wafanyakazi ambao watalipia paye, nssf, ppf
Watakodi makampuni ya ndani kwa ajili ya usambazaji wa bidhaa kwenda mikoani nk. Watafaidika makampuni ya usafirishaji na wafanya kazi wao na pia watanunua mafuta kwa ajili ya kusafirisha mizigo, matairi, spea, nk
Watakuwa na distributors ama wauzaji wakubwa na wadogo

Sasa ukiangalia huo mnyororo wa thamani unanufaisha wengi kwa kutoa ajira na mzunguko.
Ukimruhusu mura alete yeye Sukari ya bei rahisi atafaidika yeye na mke wake na watoto wake na ataajili cheap labor meneja wake atamlipa laki 2 bila mkataba.

Tataaa muraaa mutani wangu huyo
 
Unaweza kuwa uko sahihi. Lakini Kama uzalishaji wa ndani hautoshekezi mahitaji halisi ya bidhaa husika, solution yake ni kuziba masikio kwa kuwa tu tunalinda ajira, kodi etc? Kwani kama Nchi ni bidhaa gani tunayojitosheleza kukidhi mahitaji wa ndani zaidi ya soft Drinks labda na Mahindi ya kupata ugali wa Dona tu...say more...
 
hapa umeongea ugoro mtupu,kwan huko nchi nyingne hakuna gharama za uzalishaj??????
Hili chama chakavu mbinu za kuongoza zmeshakwisha na pumzi imekata ukitaka kulijua hilo petrol inapita kwetu kwenda jiran na huko
Utaikuta inauzwa bei ya chin kuliko kwetu kwann???
Mngejua kitu kimoja.Hakuna nchi iliyoendelea kwa kuimport bila kuwa na viwanda vya ndani.
Pili tunaita mnyororo wa thamani. Kiwanda kinavyozalisha, kitalipia umeme, maji, land rent, kodi,
Wataajili wafanyakazi ambao watalipia paye, nssf, ppf
Watakodi makampuni ya ndani kwa ajili ya usambazaji wa bidhaa kwenda mikoani nk. Watafaidika makampuni ya usafirishaji na wafanya kazi wao na pia watanunua mafuta kwa ajili ya kusafirisha mizigo, matairi, spea, nk
Watakuwa na distributors ama wauzaji wakubwa na wadogo

Sasa ukiangalia huo mnyororo wa thamani unanufaisha wengi kwa kutoa ajira na mzunguko.
Ukimruhusu mura alete yeye Sukari ya bei rahisi atafaidika yeye na mke wake na watoto wake na ataajili cheap labor meneja wake atamlipa laki 2 bila mkataba.

Tataaa muraaa mutani wangu huyo
 
Mngejua kitu kimoja.Hakuna nchi iliyoendelea kwa kuimport bila kuwa na viwanda vya ndani.
Pili tunaita mnyororo wa thamani. Kiwanda kinavyozalisha, kitalipia umeme, maji, land rent, kodi,
Wataajili wafanyakazi ambao watalipia paye, nssf, ppf
Watakodi makampuni ya ndani kwa ajili ya usambazaji wa bidhaa kwenda mikoani nk. Watafaidika makampuni ya usafirishaji na wafanya kazi wao na pia watanunua mafuta kwa ajili ya kusafirisha mizigo, matairi, spea, nk
Watakuwa na distributors ama wauzaji wakubwa na wadogo

Sasa ukiangalia huo mnyororo wa thamani unanufaisha wengi kwa kutoa ajira na mzunguko.
Ukimruhusu mura alete yeye Sukari ya bei rahisi atafaidika yeye na mke wake na watoto wake na ataajili cheap labor meneja wake atamlipa laki 2 bila mkataba.

Tataaa muraaa mutani wangu huyo

Umeongea point ile nje ya hoja ya msingi.

Kwanini sukari ya ndani inauzwa bei kubwa? Mbona wenzetu ni bei ndogo.. sisi tunafeli wapi hadi gharama za uendeshaji ni ghali??

Bidhaa zetu za ndani hazina uwezo ku-compete.

Sio bidhaa tuu. Nikupe mfano mmoja. Kuna icubator zile kubwa za kutotolesha mayai, nilinunua januari kkoo sh 780,000.
March nkaenda nairobi nikakuta kwa ile 780,000 ningepata incubator km zile zile mbili zaidi. Imagine:

Wote hazitengenezi, tuna import. Lkn kwann kwetu ghali???
 
Nina uzoefu na viwanda vya sukari Tanzania, bei wanayotuuzia sukari yao ni wizi na utapeli mtupu, wanataka super profit.

Wameiweka bodi ya sukari na wizara mfukoni, kila mwaka wanawapa story za kutaka kupanua uwezo wao wa kuzalisha kwahiyo bei iongezeke.

Dawa ni kuruhusu sukari ya nje hata kwa mwaka mmoja, warashusha hizo bei zao wenyewe.
 
Sukari toka Zambia kilo 2000-2200

Sasa hivi kitenge kinatoka Nje kinapita bandari ya Dar moja kwa moja mpaka Lusaka, halafu kinatolewa Lusaka mpaka Tunduma tena kinatoka Tunduma mpaka Mikoa ya Iringa, Dodoma, Arusha na bado kinalipa vizuri kuliko mfanyabiashara alielipia Bandari ya Dar.

Mafuta yanatoka nje yanapita Bandari ya Dar yanaenda mpaka Zambia ajabu yanauzwa kwa tofauti ya shilingi 700 na Tanzania.

Tunduma magari yote yanajaza mafuta upande wa Zambia kuanzia mabasi makubwa kwa madogo malori Hadi Gari binafsi utaona msululu wa kutosha kujaza mafuta upande wa Zambia.

Sijui tunafeli wapi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom