Bei ya mafuta yashuka kwa 54%

Habari za sasa hivi za CNN ni hizi "BREAKING NEWS: Oil dips below $50 a barrel on New York exchange for the first time since reaching record high of $147 in July"
Tatizo kubwa ninaloliona ni EWURA kutokuwa makini au kuna mikono michafu intembea pale ili kutuumiza. Na wala sio kodI, kwa sababu kodi inatozwa kulingana na mwingizaji alivyotoa taaria zake TRA wakati anaingiza mafuta au bidhaa yoyote. Kodi itakuwa kubwa kama bei ya mafuta itakuwa kubwa lakini jinsi mafuta yanavyopungua bei kodi pia inapungua. Ukiondoa "Kodi ya barabara" ambayo ni fixed, kodi ya kuingiza bidhaa "import duty" na kodi ya ongezeko la dhamani "VAT" inatozwa kwa asilimia ya bei ya mafuta wakati wa kuingia. NIjuavyo nchi hii haina matanki yanaweza kutunza mafuta hata kwa mwezi mmoja tu. Ndio maana meli ikichelewa kufika au kuingia bandarini waizaji wa mafuta huhaha.
Na kama kawaida haiwezekani mwingizaji wa mafuta akatoa taarifa TRa za bei yake ya mafuta kuwa kubwa ili aendelee kuuza mafuta akisingizia kodi kubwa. EWURA ingeangalia waingizaji wa mafuta wanatoa taarifa gani TRA na kuzifanyia kazi ingekuwa rahisi kuwabana. Lakini nina mashaka kuna mikono michafu intembea ingawa siamini kama na BP pia wanaweza kuhusika na uchafu huo.
 
CNN Breaking news: Oil dips below $50 a barrel on New York exchange for the first time since reaching record high of $147 in July.

Mara nyingi inaonekana kuwa wananchi wanakuwa watu wa kulalamikia serikali! wavivu wa kufikiri na wasioona mazuri yanayofanywa na serikali. Lakini jambo la msingi la kujiuliza ni kwanini kuwa na serikali? wakati watu walikuwepo kabla ya serikali kubuniwa? Kwanini watu wabebe mzigo wa kuigharamia serikali?

Serikali ipo, kwa manufaa ya watu na wala sio watu kwa manufaa ya serikali! sasa serikali inaposhindwa kusimamia majukumu yake ya msingi, ambayo ni kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma wanazozihitaji, unashindwa kujua kwanini kuwe na seriali, kama hospitali hakuna, usafiri hakuna, vyakula hakuna au bei juu, mafuta hayashikiki japo sokoni yankozalishwa yanafikia karibu sawa na bei ya bure!

Kama serikali inashindwa kutizama mambo haya kwa kisingizio cha soko huria, swali linarudi pale pale kuwa ya nini kuwa na serikali! Inaonekana kuwa kuna serikali kwa ajili ya mabwana, watawala pamoja na jamaa zao, ndio wanaomiliki njia kuu za uchumi, ndio waliochimba mifereji mirefu na mapana ya kuwaibia watanzania kile kidogo walionacho, ndio waliojizungushia majeshi na kila aina ya ulinzi ili kuhakikisha kuwa wao na jamaa zao wapo salama.

Labda sasa vianzishwe vyama vya walaji! Ndio, Ndio, tena sana. Watumiao mafuta waanzishe chama kutetea masilahi yao, umeme, maji nk, ikibidi na vyakula. Ndio kwanini tusifanye hivyo, wakati haya siyo majukumu ya serikali tena! Wao wanataka kodi tu! na kinachopatikana juu wananeemesha matumbo yao na jamaa zao. Kwani sio kweli?

Kama wakati mafuta yalipofikia takribani $150, hapa kwetu yalifikia 2000, leo yamekuwa $50! hapa hali ikoje?

Ndio, kwani bei zilipokuwa zikipanda wao walikuwa wanasubiri kumalizia pipa la mwisho walilonunua kwa bei ya zamani!

SWALI LINABAKI SERIKALI YA NINI?

INAUDHI
 
.................tafadhali EWURA shusheni bei, ili na nauli zishuke. si zilipanda kwa sababu ya bei kubwa ya mafuta? shushenii watu twende x-mas kwa bei poa!!!
 
Wakuu ebu naomba mnipe hesabu za kitu hiki maanake tusiwe tunazungmza tuuu na kulaumu sana wakati hatujaangalia vitu vinavyosababisha mafuta kuwa bei ghali kiasi hicho..

Kwanza kabisa Barrel moja la mafuta ilipokuwa ghali ilikuwa Usd. 150 (147), na lina lita kitu kama 116.. Hapa tu utaona bei ya mafuta machafu ni hiyo $150 gawa kwa hizo lita 116 upate kwa lita au sio!.. Ni bei ya njugu kabisa..
Sasa ikiwa tumeuziwa kwa bei ya sh. 2000/= kwa lita bila shaka hii imetokana na gharama nyinginezo..Gharama ya usafiri na kafaida, usafishaji na ka faida, Kodi, storage(kafaida) kisha bado kuna gharama za wenye station za mafuta na kafaida kao..
Hizi gharama za matumizi zote haziwezi kupungua hata kama mafuta ni dollar 30 au 150, zinasimama pale pale ama kuongezeka...
Hivyo basi ukweli unaangukia kwamba gharama kubwa ya mafuta ipo nje ya bei ya barrel na kama sikosei mwaka 2003 barrel moja lilikuwa likiuzwa kitu kama Us dollar 30 tu na watu walilipa sh. 1200/= kwa lita ya mafuta safi, sasa jaribu kupanda na hiyo bei ufikie bei mafuta yalipokuwa juu, hiyo 150 utaona ni mara mara 5 (toka 30 hadi 150)..Je, hivi kweli mnataka kunambia bei ya mafuta mwezi October ilitakiwa iwe Sh.1200/= mara 5?..
Sidhani!..Ni kweli Bongo wafanya biashara wanatulima kishenzi lakini wakuu zangu sidhani kama mmetazama upande mwingine wa shilingi..
 
.....sijui kazi ya EWURA ni nini sasa kama wanashindwa kitu kidogo kama hiki? haiingii akilini bei ishuke kutoka 147 mpaka chini ya 50 lakini kwenye pump bei ni kama ile ya 147,maana constant nyingine zote(tax & fee,transportation etc) sijasikia zimepanda,hapa lazima kuwe na serious explaination kutoka kwa hawa wafanyabiashara,na EWURA lazima watoe maelezo tumechoka na hawa wababaishaji...na free market sio ripping off wananchi,ikijulikana kama kuna deal chafu wanacheza futa licence zao zote za kuuza mafuta na fukuza mgt ya EWURA,kuna honest people wengi tuu wanataka hiyo opportunity ya kuuza mafuta na kuitumikia serikali kusimamia maslahi ya wananchi,natafuta email ya mkurugenzi wa EWURA nimwandikie maana hii haikubaliki na!
 
Over 50% ni taxes, wauza mafuta watapunguzaje bei kama taxes ziko juu namna hii?

Kama ni hivyo hakuna sababu ya bei kutoshuka naana kodi inatozwa kulingana na bei yake inapoingizwa nchini. Kama bei ya lita inauzwa shs 500/- inafika nchini basi bei ya dukani itakuwa 500 + (50%)=750/- kwa lita kwa kuwa kodi iko kwenye asilimia. Na kama madai ya wengine hapo juu ni sahihi imekuwaje bei imeshuka hata hapa nchi (sio Dar) ingawa ni kwa kiasi kidogo sna kulinganisha na jinsi ilivyoshuka kwenye soko la dunia?

Vinginevyo waagizaji (kama ingekuwa ni serikali) kuna sehemu wanakopa ndo maana bei haishuki. Zaidi ya hapo kuna ufisadi, tupende tusipende na kama hakuna ufisadi kwa nini EWURA wamepiga kelele na kutoa ultimum kwa wenye vituo vya mafuta kushusha bei lakini imeshindikana? Justification gani walizotumia EWURA kuwataka waaagizaji mafuta washushe bei? SOMETHING MUST BE WRONG SOMEWHERE!
 
Why did they kill TPDC? I suspect it was an indicator of currently EPA scandal!
 
Mshiiri,
Yap, ndio swali kubwa mkuu wangu..Tatizo kubwa ni kwamba serikali yetu imeingia Ubepari kichwa kichwa kiasi kwamba hatukujipanga toka mwanzo..

Yawezekana kabisa kuwa hata mafuta safi yanaangizwa na watu binafsi toka nje..Tumeua TPDC hivyo mafuta yanakuja nchini tayari yamekwisha safishwa, na hakuna mmoja wetu anayejua tunayanunua kwa bei gani! unajua tena mdanganyika kwa ready made! na kama ni toka Mombasa haya Wasomali nao wamefunga border..Kifupi nchi yetu inakwenda kwa majaaliwa ya Mungu.
Wenzetu, mafuta ni chanzo muhimu sana cha maendeleo yao na wamejipanga kikamilifu kuhakikisha nchi hivyo wameweza kushika sehemu zote kiasi kwamba bei ya mafuta inapopanda wanajua
 
Mkandara
Its a nightmere to them now when nature is let to take its course then things such as these are not uncommon. EPA, Jails, and some occassion may amount to death of a certain group or killings from frustrated citizens; the bad side of it!

So leaders and authorities should intervene with citizens' interests they have forgotten for a very long time and to these interests only they must stick to save their as*es
 
Wakuu ebu naomba mnipe hesabu za kitu hiki maanake tusiwe tunazungmza tuuu na kulaumu sana wakati hatujaangalia vitu vinavyosababisha mafuta kuwa bei ghali kiasi hicho..

Kwanza kabisa Barrel moja la mafuta ilipokuwa ghali ilikuwa Usd. 150 (147), na lina lita kitu kama 116.. Hapa tu utaona bei ya mafuta machafu ni hiyo $150 gawa kwa hizo lita 116 upate kwa lita au sio!.. Ni bei ya njugu kabisa..
Sasa ikiwa tumeuziwa kwa bei ya sh. 2000/= kwa lita bila shaka hii imetokana na gharama nyinginezo..Gharama ya usafiri na kafaida, usafishaji na ka faida, Kodi, storage(kafaida) kisha bado kuna gharama za wenye station za mafuta na kafaida kao..
Hizi gharama za matumizi zote haziwezi kupungua hata kama mafuta ni dollar 30 au 150, zinasimama pale pale ama kuongezeka...

Hivyo basi ukweli unaangukia kwamba gharama kubwa ya mafuta ipo nje ya bei ya barrel na kama sikosei mwaka 2003 barrel moja lilikuwa likiuzwa kitu kama Us dollar 30 tu na watu walilipa sh. 1200/= kwa lita ya mafuta safi, sasa jaribu kupanda na hiyo bei ufikie bei mafuta yalipokuwa juu, hiyo 150 utaona ni mara mara 5 (toka 30 hadi 150)..Je, hivi kweli mnataka kunambia bei ya mafuta mwezi October ilitakiwa iwe Sh.1200/= mara 5?..
Sidhani!..Ni kweli Bongo wafanya biashara wanatulima kishenzi lakini wakuu zangu sidhani kama mmetazama upande mwingine wa shilingi..

Ndugu Mkandara,

Hebu pitia tena hiyo analysis yako uone kama ina-make sense. Kumbuka kuwa kwa bei kushuka sasa wanaweza wakaagiza mafuta mengi zaidi kwa kiasi kile kile cha fedha (actually mara tatu). Huko Marekani kwa mfano twaambiwa bei ya wastani ilikuwa inakaribia USD 1.00 kwa lita na sasa ni chini ya USD 0.25. (linganisha na Tshs. 2,000.00 hadi 1,600.00) - does it make sense ?

Pili the fact kwamba wakati ilipokuwa USD 0.20 kwa lita US na Tanzania wakawa wanauza Tshs. 1,200.00 inaonyesha state sponsored daylight robbery dhi di ya wananchi wake. Ndio mlolongo wa UFISADI huo na kujaribu kuutetea kwa namna yoyote ile ni kubariki na kukumbatia sera ya dhuluma ya CCM. Hebu pitia tena hizi hesabu ndugu yangu.
 
Mag3,
Mkuu nakuelewa unachozungumza isipokuwa tu unajaribu kufananisha Marekani na Tanzania wakati chumi za nchi hizi mbili ni tofauti kabisa..
Acha Mafuta nambie kitu chochote kinachoagizwa nje ambacho kinalingana bei na ile ya Marekani! hakuna lakini tazama bei ya vitu kama soda ya Cocacola (tunaagiza raw material) kisha inatengenezwa nyumbani unaweza kulinganisha na Ulaya.

Binafsi naamini kabisa kwetu sisi bei ya mafuta haitokani na bei ya pipa toka Arabuni kwa sababu za kijinga kabisa kuwa hatuna miundombinu yetu ktk Usafiri, viwanda ktk kusafisha na kadhalika zaidi ya kutegemea walanguzi wenye uchu wakati wenzetu wamejipanga kikamilifu ktk mahitaji muhimu kama mafuta na unaweza kupiga hesabu kirahisi..
Kwa hiyo kutokuwa developing country pia inaongeza gharama za matumizi kwani Tanzania hatuagizi Raw material kama wenzetu, sisi tunaagiza finished product yaani nchi nzima tupo ktk kundi la Wateja..

Ndio maana nikatumia ile hesabu ya kutoka Tsh.1200 mwaka 2003 na kujaribu kuzidisha mara tano, October 2008 tungekuwa tukinunua kwa T sh. zaidi ya 6,000 kwa lita, jambo ambalo halikutokea..Lakini kama ingekuwa Marekani hesabu zingekwenda hivyo! -kuna kitu hapa katikati ambcho kwa mtazamo wangu kinahusiana zaidi na sababu nje ya bei ya crude Oil.
Umezungumzia pia kupungua kwa bei kunamwezesha mnunuzi kununua mafuta mengi zaidi..Mkuu, biashara ya kibongo haiendi hivyo mbali na ukweli kwamba kiuchumi unaagiza mali (supply) kulingana na mahitaji (demand) kwa hiyo hata kama bei itakuwa chini bado utaagiza mafuta kulingana kiwango cha mahitaji ya matumizi..
Huwezi kununua mengi sana wakati hufahamu kama kesho bei itashuka zaidi kisha storage yenyewe matatizo tuna sehemu moja tu Tanzania nzima (Kurasini) kama sikosei..

Kuliwa tunaliwa sana ila tu nadhani zipo sababu nyingi ambazo zinasababisha Ubabaishaji nchini ikiwa ni pamoja na kuagiza kila kitu ready made, tukipuuza kabisa kujenga miundombinu.. infrastruture yetu mbovu ktk kila nyanja.
Ebu tazama energy, Kikwete aliahidi kuboresha nguvu za uzalishaji Umeme sijui kama leo hii kuna mradi hata mmoja ambao unafanyiwa kazi. Wakati uzalishaji wa umeme unapewa wafanyabiashara binafsi kina Lowassa, kisha usambazaji ndio serikali imeikabidhi Tanesco..Hapa lawama zote zitawafikia Tanesco ambao wamebanwa mbavu kishanzi na mashirika binafsi na huwezi kuweka regulations kwa msambazaji wakati hufahamu amenunua kiasi gani toka kwa mzalishaji na pengine katikati kuna mlanguzi..
 
Mag3,

Umezungumzia pia kupungua kwa bei kunamwezesha mnunuzi kununua mafuta mengi zaidi..Mkuu, biashara ya kibongo haiendi hivyo mbali na ukweli kwamba kiuchumi unaagiza mali (supply) kulingana na mahitaji (demand) kwa hiyo hata kama bei itakuwa chini bado utaagiza mafuta kulingana kiwango cha mahitaji ya matumizi..

Je hudhani kuwa mahitaji (demand) hutegemea bei. Bei ya mafuta ilipopanda Marekani wenye vituo vya mafuta ni wazi walilia sana kwa kukosa wateja.
 
Mag3,
Mkuu wenye stesheni za mafuta wao ni wafanya biashara kuna kupata na kukosa na yawezekana kabisa katika hesabu za kupanda bei ya mafuta kulipunguza demand, kwa hiyo ktk ongezeko la bei pia hufidia gharama za uendeshaji wakati demand ipo..
Lakini above all that bei ya mafuta ilipanda sana kutokana na demand kupanda kupita kiasi cha supply iliyokuwa ikitolewa na nchi za Opec..Pia kumbuka Nigeria, Iran na Venezuela walipunguza kabisa uzalishaji kutokana na mambo ya siasa.
Hivyo at a limited supply,mafuta yalikuwa dhahabu na kila wakipandisha bei bado yalizidi kuuzika... a very small number ya watu waliacha utumiaji wa mafuta na dunia haikuwa tayari kureplace mafuta..
Kama unakumbuka Marekani kabla ya bei kuwa juu sana waliwaomba Saudia kuongeza uzalishaji ili ku flood market ili kustable Oil price ilipokaribia 100 kwa pipa..
Haiwezekani bei kupanda tu hata kama demand haipo...Hata maji ya kunywa leo hii huko Congo na Somalia yanauzwa bei juu kuliko hata mafuta yote inatokana na demand, swala la wateja wachache halina uzito...
 
Hatimaye bei ya Petroli na Dizeli zimelingana huku Bara. Bei ya Petroli/Dizeli ni 1440/- kwa lita. Naamini kwa hali ilivyo kwenye soko la dunia kwa mafuta kushuka kwa zaidi ya 50% bado bei inaweza kufika hadi shs 1000/- kwa lita .

Kama huwa tunazingatia vigezo vya kupanda bei ya mafuta soko la duniani katika ku-justfy kupandisha bei hapa nchini inatupasa kutumia vigezo hivyo hivyo katika kushusha na si kupiga porojo kama tunavyofanya wengi wetu hapa JF kujaribu ku-justfy kwa nini bei ya mafuta nchini mwetu haishuki wakati wazalishaji wenyewe wameshusha!
 
Mkuu Ibrah,

Mimi mbona nanunua Tshs 1,600/= au Tshs 1,590/= per litre hapa Dar? Wapi huko mkuu, tupeane deal maana nahisi napigwa changa la Macho. Kituo gani hicho? Manake hata kile cha Mandela kati ya Buguruni na Tabata ambacho hujulikana kwa kuteremsha bei bado wamegomea Tshs 1,500/= per litre kwa petrol.

Halafu kuna vituo vinahisiwa kuchanganya mafuta, hili linanifanya nishindwe hata kujaza mafuta Big Bon, Camel na OilCom, unaweza kunipa dodoso ni vituo gani vinahisiwa kuchanganya mafuta?
 
Huku ni Arusha mkuu. Sasa ndo ushangae kuwa hapa Dar bei ni juu kuliko huko Bara na bandari iko hapoa Dar! Wiki 2 zilizopita nilikuwa huko Dar na nikashangazwa na bei ya mafuta kuwa juu kuliko mikoani. Wakati nlipokuwa huko bei ya Dizeli ilikuwa 1600/-wakati Morogoro ilikuwa 1,200/- ! Ndo maana nikasema kuna ufisadi mkubwa katika biashara ya mafuta na hasu huko Dar!

Suala la uchangaji wa mafuta ni gumu sana kulidhibiti EWURA wameshashindwa na walipovifungia baadhi ya vituo vilivyobaibika kuchanganya mafuta walishtakiwa na wakashindwa. BP na Orxy inasemekana kuwa ni Makampuni ambayo vituo vyake havichnagany Mafuta lakini mwezi wa June EWURA huku Arusha walibaini kuwa vituo maarufu vya Manjis BP na Clock Tower Orxy vinatuuzia mafuta machafu na EWURA wakatangaza magazetini kufungiwa kwa vituo hivyo (Manjis na Clock Tower) kuuza mafuta lakini cha ajabu vituo hivyo viliendelea kuuza mafuta kama kawa! Melo, nachokiona mimi ni mchezo mchafu na ufisadi tupu katika biashara ya mafuta hapa TZ na nashangaa ati serikali imeshindwa kudhibiti ubora na bei za mafuta. Hatuna pa kwenda mkuu labda ni pale Wakulu wa nchi wakiamua kutupa afueni na kutuaonea huruma, basi!
 
Oil falls below $67 a barrel on demand worries

Thursday, October 23, 2008

Oil prices plunged to their lowest in 16 months Wednesday as global economic worries led investors to predict a further drop in energy demand.

The continuing slide in prices is good news for drivers. The nationwide average gasoline price is now the lowest in nearly a year and is set to fall further.

The price of a barrel of light, sweet crude trading for delivery in December fell $5.43, or 7.5%, to $66.75, the lowest since June 2007. Oil prices are now down 54% from the record close of $145.29 on July 3.

MY TAKE: Hii ni kwa ajili ya nchi zilizoendelea pekee kwa kuwa nyumbani bei bado zile zile?, au ni uongozi wetu na siasa zisizoeleweka?.

Tuijadili..

Kinachopanga bei ya mafuta katika soko ni mahitaji. Bei imeshuka kwa sababu mahitaji yamepungua, ila kwa Tz sijui tupo katika sayari ya Mars maana bei ya mafuta iko pale pale japokuwa katika soko la dunia bei imeshuka. Si EWURA wala serikali nobody cares!
 
Huku ni Arusha mkuu. Sasa ndo ushangae kuwa hapa Dar bei ni juu kuliko huko Bara na bandari iko hapoa Dar! Wiki 2 zilizopita nilikuwa huko Dar na nikashangazwa na bei ya mafuta kuwa juu kuliko mikoani. Wakati nlipokuwa huko bei ya Dizeli ilikuwa 1600/-wakati Morogoro ilikuwa 1,200/- ! Ndo maana nikasema kuna ufisadi mkubwa katika biashara ya mafuta na hasu huko Dar!

...Hatuna pa kwenda mkuu labda ni pale Wakulu wa nchi wakiamua kutupa afueni na kutuaonea huruma, basi!
Makubwa haya, Arusha iwe bei pungufu kuliko Dar? Hii kwangu ni ajabu sana. Nini maanake?

BP nimekuwa nikiwatumia muda mrefu lakini kuanzia Februari mwaka huu nikajikuta nashindwa kuendelea nao kwani ukiwa na kasumba ya kununua mafuta sehemu moja tu kuna siku ukiwa mbali nao unajihisi kuwa na utumwa wa lazima kuwatafuta wao tu. Biashara hii ina wenyewe!
 
Hapo Dar ndo kwenye serikali na ufisadi umejikita hapo hapo, nini manaake? Nadhani kuna watu wame-engineer kamtandandao ka kushibisha matumbo yao kupitia biashara ya mafuta hapo Dar. Akili ya kawaida haiwezi kukubali kabisa kuwa Mafuta huku bara yawe bei ndogo kuliko Dar; kizingizio utachosikia ni kuwa kuna kukwepa kodi na njia za panya lakini si kweli maana mbona mafuta yalipoanda bei duniani huku Arusha bei ilikuwa juu kuliko Dar? Akili mukichwa!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom