FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,506
- 123,776
Ritz, naona ama umenogewa na ngano za Mohamed Said hadi zinaanza kutia kichefu chefu au wewe ni moja katika wanaomeza simulizi za barazani bila kuhoji. Kwako hadithi haina tofauti na ukweli.
Huu ni uongo ambao kama tu ungekuwa na kumbukumbu kidogo hungethubutu kuuandika humu JF kwani uliwahi kuletwa awali lakini ikagundulika ni simulizi tu kama za mgahawani. Mwalimu alikuwa ni Kiongozi wa TAA mkoani Tabora miaka mingi tu kabla ya huo mwaka 1952.
Kama kuna mtu Dar es Salaam alikuwa hamjui Mwalimu, basi huyo mtu hakujua harakati zozote zilizokuwa zikifanyika nchini Tanganyika nje ya Dar es Salaam. Katika mkutano wa kitaifa uliofanyika kabla jimboni Tabora uliohudhuriwa na viongozi wa kitaifa wa TAA Mwalimu alikutana na wawakilishi kutoka sehemu mbali mbali nchini na Dar akiwamo Dossa Aziz na wengineo. Abdulwahid Sykes wakati huo labda alikuwa akijulikana tu kama mtoto wa baba, Klyst Sykes, na hakuwa na wadhifa wowote ndani ya TAA.
Hii ilikuwa baada ya mapinduzi ya vijana kuutwaa uongozi wa TAA na Dr. Vedasto Kyaruzi kuchaguliwa kuwa Raisi wake wa kwanza na Abdulwahid Sykes katibu. Abdulwahid Sykes hakuwahi kuchaguliwa hata mara moja kuwa Raisi wa TAA, alikuja kukaimu tu kwa muda hiyo nafasi baada ya Raisi wake, Dr. Kyaruzi kuhamishiwa mikoani na wakoloni.
Ni wajumbe na viongozi wa TAA Dar es Salaam waliomuomba Mwalimu kujiunga na baraza hilo kwa sababu hakuwepo mtu aliyekuwa na ujasiri, elimu, uwezo na sifa ambaye angeweza kuiongoza TAA katika mabadiliko ya kuigeuza chama cha siasa.
Mwalimu alikuwa akifuatwa huko Pugu na kuna baadhi ya mikutano iliyofanyika huko huko wakimshawishi akubali kuwa kiongozi wao.
Hapana, wanasiasa wengi alishakutana nao kabla ya kwenda masomoni Uingereza, Dossa Aziz akiwa mojawao. Labda useme alikutana na viongozi wakazi wa mji ambao hawakuwahi kutoka nje ya Dar es Salaam kwa sababu mbali mbali; hapo itaeleweka.
Mwalimu alileta changamoto na fikra mpya ndani ya TAA na hapo ndipo sauti za kudai uhuru zikaanza kusikika kupitia magazeti kama Zuhura na kadhalika.
Miezi sita tu toka ajiunge na TAA Dar es Salaam alichaguliwa kuwa kiongozi wake mkuu akimbwaga Abdulwahid Sykes aliyekuwa akikaimu nafasi hiyo naye kujitosa kugombea.
Ritz, unapoambiwa jambo na wewe jipe fikra kidogo siyo unameza tu, hebu jiulize; huyu mtu ambaye hakuna aliyemfahamu anasafiri hadi Dar, anasema katoka Pugu, anakuta watu wamejipanga wanakiendesha TAA wakiwa na mipango lukuki, anatambulishwa na mtu moja na baada ya muda mfupi wanamkabidhi chama chao cha TAA walichokianzisha akiongoze! Ningekuwa wewe ningejiuliza, je hii iliwezekanaje?
Nilielewa maneno mengine yote ila hiko ambalo mpaka sasa sielewi maana yake na ndiyo maana sijaligusia katika majibu yangu. Unaona tabu kutuelewesha lina maana ipi hilo neno?
Si kweli, hakuna chuo cha Kiislam Morogoro, kuna chuo cha Waislam Morogoro. Kumbuka hilo, ni Muslim University of Morogoro na si "Islamic" University of Morogoro. Hata kifupi chake ni MUM na si IUM.
Hivi hizo shule huwa mnaenda kusomea ujinga?
Naomba nisaidie hili swali langu dogo; Mau Mau walipigana na Wajerumani?
Mkuu Mohamed Said anaweza kuwa na hoja but anajikanganya Sana na article zake zipo too illogical na hazina ushahidi Wa kina.
All right professor, tuambie siku ambayo ulikanyaga darasa la shule ya sekondari.
Lusungo,
Ndugu yangu wala usipate tabu na makosa yangu kuwa "najikanganya."
Ikiwa unaliona kosa sahishisha wla usiwe na hofu.
Ikiwa wewe una ushahidi unaopingana na wangu ulete hapa barzani sote
tufaidike.
Mkuu ilikuwaje watu ambao wewe unadhani walikua initiators Wa vuguvugu la kudai Uhuru wakapinduliwa ktk historia na kubaki Nyerere?
Hebu jibu kwanza swali langu hapo juu halafu uje na yako, hiyo ndiyo raha ya mnakasha.
Lusungo,
Matatizo yaliyotokea baada ya uhuru nimeyaeleza kwa kirefu katika kitabu
cha Abdul Sykes.
Lusungo.Nani alianzisha TANU?
Okay lengo langu ilikua kuandika fukunyua....
Una lingine professor?
average minds discuss events,small minds discuss people....nakushauri tu ubaki kuwa muimba mapambio ya kumshabikia mohamed said.
Oooh, sasa ulikuwa unababaika nini? umelewa? "kufunyua" na "fukunyua" ni muhali. Au umeanza kujifunza kuandika Kiarabu?
Jee, Mau Mau walipigana na Wajerumani?
Ujinga unafundishwa MUM chuo cha kiislamu. Shika adabu yako!
Unayo habari kuwa hicho chuo hakipo ata kwenye Central admission System
(CAS) ya TCU?
unayo habari ata wanafunzi wake wamekuwa wa kuokoteza wale waliokosa pakwenda?
Unayo habari wahitimu wake hawaajiriki tokana na uwezo hafifu?
Chuo ata kuongeza meza za kusomea kimeshindwa wanatumia zile zile za Tanesco eti unasema kinakua! usiongee usivyovijua.
Bidada chunga ulimi wako usijifanye unayajua matusi, kwanza mwanamke wa kiislamu kushinda kwenye mijadala na wanaume ni bida'h .
Kufunyua na fukunyua muhali?
Fukunyua ndio msamiati hasa nilioulenga....
Kufunyua ni neno ambalo limekosa kiambishi 'Ku' ndio maana likakupa tabu...
Mfano kufu..nyua hapo Kati niliacha 'Ku' kwahiyo kufunyua na fukunyua si muhali bibiye inahitaji akili kubwa kung'amua haya...
Nani kasema MAU MAU ilipiganwa dhidi ya wajerumani?
Punjab Singh, unaelewa maana ya MOU?
Taasisi kama Aghakan haina MOU?
Zahanati za ARAFA zina MOU unasemaje?
Lusungo.
Msome Nyerere mwenyewe hapa chini.
Baada ya miezi 13, hapo 1954, tukaanzisha TANU. Jina hili lilipendekezwa na akina Abdul Sykes. Walikuwa wamelifikiria tangu zamani, walipokuwa askari vitani huko Burma (Vita vya Pili).
Nyerere mwenyewe kakiri kuwa jina la TANU lilikuwpo siku nyingi.
Jiulize fikra za kuanzisha chama kazileta Nyerere? Hapa ndiyo watu wanapinga kuwa hawa wengine mbona historia inawatupa mbali ndiyo maana Mohamed Said kawarudisha kwenye kitabu chake.