Ritz, naona ama umenogewa na ngano za
Mohamed Said hadi zinaanza kutia kichefu chefu au wewe ni moja katika wanaomeza simulizi za barazani bila kuhoji. Kwako hadithi haina tofauti na ukweli.
Huu ni uongo ambao kama tu ungekuwa na kumbukumbu kidogo hungethubutu kuuandika humu JF kwani uliwahi kuletwa awali lakini ikagundulika ni simulizi tu kama za mgahawani. Mwalimu alikuwa ni Kiongozi wa TAA mkoani Tabora miaka mingi tu kabla ya huo mwaka 1952.
Kama kuna mtu Dar es Salaam alikuwa hamjui Mwalimu, basi huyo mtu hakujua harakati zozote zilizokuwa zikifanyika nchini Tanganyika nje ya Dar es Salaam. Katika mkutano wa kitaifa uliofanyika kabla jimboni Tabora uliohudhuriwa na viongozi wa kitaifa wa TAA Mwalimu alikutana na wawakilishi kutoka sehemu mbali mbali nchini na Dar akiwamo Dossa Aziz na wengineo. Abdulwahid Sykes wakati huo labda alikuwa akijulikana tu kama mtoto wa baba, Klyst Sykes, na hakuwa na wadhifa wowote ndani ya TAA.
Hii ilikuwa baada ya mapinduzi ya vijana kuutwaa uongozi wa TAA na Dr. Vedasto Kyaruzi kuchaguliwa kuwa Raisi wake wa kwanza na Abdulwahid Sykes katibu. Abdulwahid Sykes hakuwahi kuchaguliwa hata mara moja kuwa Raisi wa TAA, alikuja kukaimu tu kwa muda hiyo nafasi baada ya Raisi wake, Dr. Kyaruzi kuhamishiwa mikoani na wakoloni.
Ni wajumbe na viongozi wa TAA Dar es Salaam waliomuomba Mwalimu kujiunga na baraza hilo kwa sababu hakuwepo mtu aliyekuwa na ujasiri, elimu, uwezo na sifa ambaye angeweza kuiongoza TAA katika mabadiliko ya kuigeuza chama cha siasa.
Mwalimu alikuwa akifuatwa huko Pugu na kuna baadhi ya mikutano iliyofanyika huko huko wakimshawishi akubali kuwa kiongozi wao.
Hapana, wanasiasa wengi alishakutana nao kabla ya kwenda masomoni Uingereza, Dossa Aziz akiwa mojawao. Labda useme alikutana na viongozi wakazi wa mji ambao hawakuwahi kutoka nje ya Dar es Salaam kwa sababu mbali mbali; hapo itaeleweka.
Mwalimu alileta changamoto na fikra mpya ndani ya TAA na hapo ndipo sauti za kudai uhuru zikaanza kusikika kupitia magazeti kama Zuhura na kadhalika.
Miezi sita tu toka ajiunge na TAA Dar es Salaam alichaguliwa kuwa kiongozi wake mkuu akimbwaga Abdulwahid Sykes aliyekuwa akikaimu nafasi hiyo naye kujitosa kugombea.
Ritz, unapoambiwa jambo na wewe jipe fikra kidogo siyo unameza tu, hebu jiulize; huyu mtu ambaye hakuna aliyemfahamu anasafiri hadi Dar, anasema katoka Pugu, anakuta watu wamejipanga wanakiendesha TAA wakiwa na mipango lukuki, anatambulishwa na mtu moja na baada ya muda mfupi wanamkabidhi chama chao cha TAA walichokianzisha akiongoze! Ningekuwa wewe ningejiuliza, je hii iliwezekanaje?