Nampongeza sana Mh. Lowasa kwa namna ambavyo ameonyesha dhahiri kuwa yeye ni mtu wa Mungu, kwa wanaomjua Lowasa watakubaliana nami kuwa mara nyingi amekuwa mstari wa mbele kwenye mambo ya Mungu, na hii ndiyo maana wakati wa uongozi wake alikuwa mchapakazi hodari na msimamizi mzuri wa shughuli za serikali kitu kilichosabababisha apate maadui wengi kwani watanzania wengi hawajazoea utamaduni wa kusukumwa wengi hufanya kazi kwa mazoea bila kuzingatia taratibu zilizowekwa. Uchapakazi wa Lowasa ulifanya amfunike rais, yeye alikuwa ndiyo tegemeo la mwisho la watanzania wapenda maendeleo, ndiyo maana kama sio Lowasa wimbo wa ukosefu wa shule kwa vijana wanaofaulu kwenda kidato cha kwanza ungekuwa unaendelea kuimbwa kwa kupokezana. Leo hii watu wamesahau kuwa ni juhudi binafsi za Lowasa ndiyo maana hilo la shule za kata lilifanikiwa, alipoondoka ameondoka nalo kwani viongozi wengine hawakuwa na maona. Baadhi ya watu wachache hujaribu kumchafua Lowasa ili achafuke mbele za watu wakiwa na hofu kuwa huenda akagombea urais mwaka 2015 ukweli ni kuwa mpaka sasa kwenye chama cha CCM hakuna mtu anayeweza kumshinda Lowasa linapokuja suala la Utendaji na uwajibikaji. Nilishangaa sana kuona kuwa kampuni iliyosababisha mheshimiwa Lowasa ajiuzuru imenunuliwa na wamarekani khaaaaa!!! si tuliambiwa ni ya kitapeli hata serikali isiiguse mitambo hiyo? Mitambo hii tuliambiwa ni michakavu iweje leo ionekane mitambo hiyo niyamaana kwa nchi iliyopiga hatua katika medeni za viwango? Ndiyo maana nijuavyo mimi tatizo la Lowasa kuchukiwa sio ufisadi bali ni urais maana kwa vyovyote nia ya wenzetu ni kuhakikisha mwenzao anapata hivyo kila atakae inuka kama sio mwenzao lazima ataondoshwa.