The Finest
JF-Expert Member
- Jul 14, 2010
- 21,605
- 6,080
Wabongo bwana, eti siku hizi kama mtindo wa kuomba namba ya simu umeisha flani hivi...kila mtu utakayekutana nae anakuomba BBM Pin, eheeeee msinifanyie hivyo jamani sio kila mtu ana Blackberry...
Lol...kila ninayekutana nae ananiomba BBM Pin wakati mimi nina Nokia ya Tochi haya mambo haya khaaaaa...hahahaaaa kweli, hata mie sina msije mkaniomba. Pia huko darisalama pale mbalamwezi beach club waliandaa party, eti bbm party, ukiwa na blackberry basi unalipia nusu kiingilio. ukiwa huna basi unalipa fulu. Ngoja na sie wa nokia torch tuandae ya kwetu
Haujaombwa BBM Pin maana siku hizi hadi kuna party za BBM Pin...dahMhhh ndo wabongo walivyo
mambo ya kuombana email sijui no ya simu yameisha kwa sasa ni BBM pin
mie nimeamua kununua zile pin za kufungia nepi
anayeniomba nampa hiyo.
Geka kuna siku nilikutana na mdada mmoja katika kupiga naye stori mwishoni akaniambia "Naomba pin yako" nikasema ebooo Pin ndio nini....akaniambia BBM PIN nikasema tobaaa...Heh, technolojia na mambo yake, itakuja na skype. Heri ya sikukuu mkuu
Hahahaha!! Inawezekana kabisa....naomba BBM PIN yako....lolThe finest hujambo mkuu,
sikukuu ilikwendaje huko kwetu?
nimeona kama ni wewe unayekatakata mbuzi pale kijijini kwetu mkuu.
Hongera kama unatumia BB tochi! Ni among blakberry zilizo juu.Jamani hebu tufafunulieni jamani hiyo bbm pin ndo nini?me natumia tochi hapa
:lol: Kwahiyo next year namba ya simu haunipi tenaTF, mjini kubanana banaa, hebu changamka! Uzuri wa bbm chats inakuwa kama jf tu, hakuna details personal. Ngoja na mie nifanye buying a bb kuwa my new year resolution,lol
Geka kuna siku nilikutana na mdada mmoja katika kupiga naye stori mwishoni akaniambia "Naomba pin yako" nikasema ebooo Pin ndio nini....akaniambia BBM PIN nikasema tobaaa...
Hahahaha!! Haya banaaaHuyu angekutana na Kongosho ingekaa sawa sana, nadhani kutumia blakberry ndo mpango mzima kwa sasa. Likizo ya sikukuu ikiisha nitakutafuta kaka,
Huyu angekutana na Kongosho ingekaa sawa sana, nadhani kutumia blakberry ndo mpango mzima kwa sasa. Likizo ya sikukuu ikiisha nitakutafuta kaka,
Haujaombwa BBM Pin maana siku hizi hadi kuna party za BBM Pin...dah
usipoangalia hapa mjini wanakuasua kichwa.
Wanakuomba BBM pin huku wanakuletea kadi za michango
harusi
sendoff
kitchen part
ubarikio
graduation
ufunguzi wa nyumba(hapo mtu kajenga siku ya kuhamia party)
bride shower
baby shower
kibao kata