Uchaguzi 2020 BBC Swahili wamesema kwenye makubaliano yetu na kampuni ya uchimbaji madini ya Barrick kwenye zile asilimia ni kama tumepigwa

Nahisi umechanganya ma file,
Umri wa hii Id nakushauri uachane nao, sawa MATAGA ?
Sawa
Screenshot_20200919-181807_Samsung Internet.jpg
 
B
Yes ni mazuri, tulikuwa tunamiliki nothing, sasa tunamiliki 16% stake!.
Tutagawana manufaa ya Kiuchumi 50/50.
That is good !.
P
Mayalla,wewe umesoma na kuelimika,kwa nini unajenga hoja nyepesi kama Kibajaji,Kasheku au Mlinga?Umewahi kuuona huo mkataba unaotupatia manufaa hayo?Je,wachimaji Dhahabu hapa Tanzania ni Barrick pekee?Hiyo mikataba inahusisha madini mengine kama Almasi,Tanzanite,Gas,Coal au Chuma?
Tusikariri majibu ya maswali magumu kutoka kwa waliotuingiza chaka.Vipi kuhusu makinikia na deni letu la kodi USD 190 Billion?
 
Hata mm nashangaa maana tuliambiwa na lisu kuwa tutashitakiwa MIGA matokeo yake hatujashitakiwa wala nn,pia tuliambiwa na Serikali kuwa makinikia hayataondoka na tutajenga smelter hapa hapa,lakini matokeo yake makinikia bado yanaondoka pia smelter haijengwa mpaka leo,Sasa sisi wakazi wa huku Katoro tuamini kuwa lissu alitudanganya na Serikali pia imetudanganya?au nyinyi wa huko mjini mnaonaje huko?
Akitokea wakukujibu initag mkuu
 
B

Mayalla,wewe umesoma na kuelimika,kwa nini unajenga hoja nyepesi kama Kibajaji,Kasheku au Mlinga?Umewahi kuuona huo mkataba unaotupatia manufaa hayo?Je,wachimaji Dhahabu hapa Tanzania ni Barrick pekee?Hiyo mikataba inahusisha madini mengine kama Almasi,Tanzanite,Gas,Coal au Chuma?
Tusikariri majibu ya maswali magumu kutoka kwa waliotuingiza chaka.Vipi kuhusu makinikia na deni letu la kodi USD 190 Billion?
Mayalla hana tofauti na Kabudi aliyesema ametolewa Jalalani pale University of Dar Es salaam
 
Wanaoteka na kuua watanzania wenzenu ili mpate madaraka si ndiyo nyinyi wenyewe ??

Msitufanye sisi watanzania kama wajinga
Je unawafahamu hao wanaoteka na kuua? Kama unawafahamu unashindwa Nini kutoa taarifa kunakohusika?! Huo ndio unafiki wenu kueneza kuwa Kuna watu wanaotekwa wakati ni porojo tu...wataje hao watekaji...
 
You are talking about sheria za kimataifa?! Unataka nilete humu ile video ya wazungu wa Lissu akiwemo Amsterdam na wenzake walichopanga dhidi ya Tanzania...wamepanga kuchochea maandamano na mauaji ili vurugu zitokee na kinachoitwa jumuiya ya kimataifa iitishe mkutano wa usuluhishi na Lissu...wazungu hao wanasema na kuropoka bila aibu kwamba ni lazima damu imwagike Tanzania...kuchomwa kwa ofisi za chadema ni miongoni mwa mikakati hiyo...
Hapo umemkamata maana ni mtu wa kukariri.
 
Wakuu mada nzuri, lakini mbona mmeanza kutukanana tena?sio vizuri jamani
Kuna jamaa amesema wengine tunafikiri kwa kutumia makalio baadala ya kichwa Mimi binafsi nimemwambia aanze kumwambia hivyo baba yake mzazi na jibu lake atupe mrejesho humu jf...
 
Je unawafahamu hao wanaoteka na kuua? Kama unawafahamu unashindwa Nini kutoa taarifa kunakohusika?! Huo ndio unafiki wenu kueneza kuwa Kuna watu wanaotekwa wakati ni porojo tu...wataje hao watekaji...
Nani anayeteka watu serikali iko kimya ?
 
Ni economic benefits not profits
Ni nini economic benefits? Tafadhali unaweza kutoa angalau mfano mmoja?
Kwa sababu sisi tusiofahamu misemo ya kiuchumi tunapopigwa changa la macho.
 
Nilisikiliza taarifa yote ya habari...na mchambuzi huyu wa Chadema...very stupid indeed...BBC wamefanya hivyo makusudi kwa kumleta anayejiita mchambuzi kutoka Chadema..ni mkakati wa kampeni za Chadema
BBC ni Shirika la Utangazaji la Serikali ya Uingereza linatangaza taarifa yoyote ya kweli na uhakika yenye ushahidi tosha tofauti na TBC ya Serikali pia inayotangaza uongo tupu wa Serikali na Chama. Huyu mjinga wa CCM mtafuta uteuzi anayedai anamfahamu mchambuzi wa CHADEMA aliyehojiwa na BBC kama ana ushahidi si apeleke taarifa kwa wahusika waanze kushughulika? Humu jf wengi walihoji ukweli wa majigambo ya Magufuli na uhalali wa takwimu za mgao wa manufaa ya uchimbaji wa madini.
 
Nimemsikiliza Zuhura Yanus, BBC ni waongo, hakuna mkataba wala makubaliano ya 2017, mkataba ni mmoja tuu, ule uliosainiwa Ikulu 2019!.
Yale ya 2017 yalikuwa ni mapendekezo tuu.
BBC Swahili Iache Uongo!.

NB, uongo kama huu wa BBC pia uliwahi kuletwa na ZZK, baada ya kuona makubaliano yamekuwa initialed, akaandika mkataba umesainiwa.
Tulisaidia kufafanua
Japo Kazi ya Upinzani ni Kupinga, Lakini Sio Kupinga Kila Kitu, Kwenye Maslahi Ya Taifa, Tutangulize Utaifa, Tuwe Wamoja, Wakweli na Tusipotoshe.
P
P.
Hebu acha propaganda pembeni kidogo Kisha urudi kwenye uhalisia wa Jambo hili!
Inawezekanaje kibiashara, wewe uweke mtaji wa 16% na mgeni aweke 84% Kisha kwenye faida muende nusu kwa nusu?
Jibu kitaalamu zaidi yaani Kama mchumi ili utusaidie na wengine!
 
Hata mm nashangaa maana tuliambiwa na lisu kuwa tutashitakiwa MIGA matokeo yake hatujashitakiwa wala nn,pia tuliambiwa na Serikali kuwa makinikia hayataondoka na tutajenga smelter hapa hapa,lakini matokeo yake makinikia bado yanaondoka pia smelter haijengwa mpaka leo,Sasa sisi wakazi wa huku Katoro tuamini kuwa lissu alitudanganya na Serikali pia imetudanganya?au nyinyi wa huko mjini mnaonaje huko?

..inabidi uelewe barrick ni nani, na accacia ni nani ili usiweze kudanganyika ktk issue hii.

..barrick ndio walioanzisha kampuni ya accacia. walianza kwa kuimiliki 100% lakini baadae wakauza nadhani 35%++ ya hisa zao.

..wakati mgogoro huu unatokea barrick walikuwa ni majority share holders wa accacia, huku shares zilizobaki zikimilikiwa na watu wengine.

Nini kilitokea?

..serikali ilitoa ripoti za uchunguzi kwamba accacia wameiba madini na kukwepa kodi kiwango cha usd 191 billion.

..baada ya ripoti hiyo kutoka accacia waliipinga kupitia wasemaji wao mbalimbali. wakati huohuo ceo wa barrick alikuja hapa nchini na kukutana na Jpm ikulu.

..kwa upande mmoja serikali ikawa inasema accacia ni wezi. Na upande wa pili ikawa inasema barrick ni watu wazuri na tunafanya mazungumzo nao.

Tundu Lissu alisema nini?

..alisema kwamba ripoti zile haziaminiki. Na alisema tafiti za huko nyuma, zilizofanywa na makampuni mbalimbali, pamoja na SERIKALI yenyewe, zinaonyesha kwamba ripoti za Prof.Mruma na Prof.Ossoro zina walakini.

..vilevile Tundu Lissu alidai kwamba ripoti hizo na jinsi zilivyoandaliwa haziwezi kutusaidia ikiwa tutaamua kuwapeleka accacia mahakamani, au ikiwa accacia watatushitaki. Na alikwenda mbali na kusema ikiwa accacia watatushitaki watatushinda.

Je, tulishitakiwa?

..NDIO, tulishitakiwa.

..accacia walifungua kesi dhidi ya serikali ktk mahakama ya kimataifa wakipinga madai ya kudaiwa kodi ya usd 191 billion.

..kesi ya accacia dhidi ya serikali ya Tz ilisitishwa baada ya barrick kufika bei na kuwanunua minority share holder. hivyo basi accacia ikarudi kuwa mikononi mwa barrick 100%.

Matokeo ya kufutwa kesi ni nini?

..kesi ilipositishwa ndipo barrick sasa walipoweza kuendelea na ahadi ya kuilipa serikali " kishika uchumba " cha usd 300 million walichokuwa wameahidi mwaka 2017. serikali ya Tanzania nayo iliachana na madai yake ya usd 191 billion. Pia tulikubaliana kuanzisha kampuni ya ubia inayoitwa Twiga. Makinikia yalianza kusafirishwa tena kwenda ng'ambo.

Usd 191 billion vs Usd 300 million.

..ukichukua 191 billion ukagawanya na 300 million unapata 636.666.

..maana yake ni kwamba barrick wakiamua kulipa 300 million kila mwaka itawachukua miaka 637 kumaliza deni la usd 191 billion.

..pia ukiibiwa 191 billion halafu ukakubali na kuridhika kulipwa 300 million, basi wewe huna tofauti na mtu aliyeibiwa shilingi 637 halafu ukakubali kulipwa shilingi 1.

Yatokanayo.

..Tundu Lissu aliitwa msaliti na kumiminiwa risasi 16 ili afe.

..Inasemekana alipigwa risasi kama adhabu kwa kuongea na Deo Mwanyika, Mtanzania mtendaji wa ngazi ya juu ktk accacia na barrick.

..Deo Mwanyika na wenzake walifunguliwa kesi na serikali wakidaiwa kuisaida accacia kukwepa kodi.

..Deo Mwanyika na wenzake walilipishwa faini ya mabilioni ya shilingi baada ya majadiliano na Dpp.

..Wiki chache baada ya kutoka kizuizini Deo Mwanyika alichaguliwa na kupitishwa na Kamati Kuu ya CCM kugombea ubunge wa Njombe mjini.

cc Abdul Mganyizi
 
Wakuu Jana niliangalia BBC Swahili, wamesema kwenye makubaliano yetu na kampuni ya uchimbaji madini ya Barrick kwenye zile asilimia ni kama tumepigwa, hivi hiki chombo cha habari cha mabeberu kinatutafutia nini?


Magufuli ni mwongo kiasi kwamba hata shetani anamuogopa
 
Kwenye Swala la mikataba hasa madini bila kutoa damu! Bado Mabeberu yataendele kuitwa hivyohivyo!

Hiyo ndiyo inapaswa iwe vita sasa! Zingine hizi za kuoneana Sisi Kwa Sisi, Tatalaaniwa bule

Swala la mikataba ya madini nadhani ipo shida kubwa kuliko tunavyosikia,
Kama ni vita tafadhari zianze upya
Shida ya magufuli ilikuwa kiki za kisiasa kuliko maslahi ya nchi.Magu ni mwongo,ni mwongo hadi anajidanganya mwenyewe
 
Nikiweka hapa itakuwa issue kubwa mno...binafsi nimeiangalia ile video nikashangaa na kuogopa namna wazungu wale walivyoandaa mipango...yaani bila hata aibu wanataka watu wafe Tanzania ili iwe vurugu kubwa ...
Ukiona zee zima linakuwa liongo,jua ama ni mchawi au taahira.
 
Shida ni moja huu mchakato ni wa siri sana, and haijulikani kama jamaa walitupiga au sisi tuliwaonea.....

Kilichopo ni kuwa kuna allegations tu na ndizo BBC wanatumia..... So far no any confirmed details from the true source.
 
Kwa hyo mkuu kabudi ametuingiza chaka kuwa tutapata 50/50 ya mgawanyo?alafu mbona vyombo vya habari vya ndani havihoji ili jambo kuwa mkataba umesainiwa ikulu,hii imekaaje kiongozi wangu?

Kuna watu wamepewa vyeo akiwemo Gavana wa Bot kwa kumdanganya Jiwe kuwa mkataba waliokubaliana na Barrick ulikuwa kwa manufaa ya nchi kumbe waliingiza nchi CHAKA!!
Haiwezekani kwenye corporate culture ambapo wenye hisa 16% wakagawana Sawa Sawa faida na wale wenye hisa 84%!! Kujiaminisha hivyo ni utopolo; zaidi ya hayo wao wanakuwa wanaweka mapato kutoka kwenye uuzaji wa dhahabu nje ya nchi!!
Jiwe majigambo tu lakini hajui akisemacho.
 
Shida ya magufuli ilikuwa kiki za kisiasa kuliko maslahi ya nchi.Magu ni mwongo,ni mwongo hadi anajidanganya mwenyewe
Unfortunately, sio tu kuwa Jiwe ni muongo bali pia ni IGNORANT hivyo he is easily duped!
Hivyo watu kama Kabudi na Mpango take that advantage na kumlisha matango pori.
 
Unfortunately, sio tu kuwa Jiwe ni muongo bali pia ni IGNORANT hivyo he is easily duped!
Hivyo watu kama Kabudi na Mpango take that advantage na kumlisha matango pori.

..kabudi mambo yalishamfika shingoni akataka kujiuzulu.

..na kwenye timu ya majadiliano walikuwepo maprofesa walioandaa ripoti zinazodai accacia/barrick wametuibia.

..ripoti za uchunguzi zilikuwa na matatizo, ndiyo maana nguvu kubwa inatumika kunyamazisha yeyote yule anayejaribu kuhoji.
 
Back
Top Bottom