BBC na uchochezi, itafutwe namna idhibitiwe

Hii nchi hii ipo cku mawe yataongea maana mnatamani kila mtu awasifie kwa lipi hasa au kwa kipi haswa au mlidhani kununua ndege ndio mtaandikwa mpaka kwenye cnn na mashirika yote ya habari duniani mkisifiwa?....huwezi kusonga mbele kama hujakosolewa TBC na gazeti la UHURU vinatosha kabisa kuwasifia msiforce kila mtu awasifie kwa lazima..
 
Unafikiri BBC ni sawa na mawio?
 
Unasikiliza na kuangalia habari za BBC, CNN, DW zanazohusu nchi zao? Ulishasikia zinasifia upupu? Soma jinsi BBC, Sky wanavyomchamba Teresa May je amefungia vyombo hivyo? Soma CNN na vyombo vingine wanavyomchamba Trump mpaka anasema fake news. Hizi ni independent organisation ingawa BBC inalipiwa na walipa kodi wa UK lakini hawaingiliwi na mtu siyo kama TBC.

Uliona Tido alipoingia akadhani yupo BBC kilichomtokea? Bado Tanzania ni makomnist au tuseme socialist country hivyo mtoa uzi utakufa bila kujitambua. Hata ukiobewa ni bure.
Watu wanajiuzuru kila siku vyeo sababu ya kuandikwa ukahaba, niambie mawaziri Tanzania wakipigwa picha na mahawala wakawekwa gazetini au kwenye TV, hivyo vyombo vitapona?
 
Umenena
 
Kweli, waliosema "Nionyeshe Rafiki/Marafiki zako Nami nitakueleza Wewe ni mtu wa aina gani hawakukosea." Tumeshakujua wewe ni mtu wa aina gani kutokana na marafiki ulionao. Haisumbui hata kidogo. But remember this "Tanzania si mali ya mtu binafsi. Ni ya Watanzania wote." Tuheshimiane kwani mawazo kinzani daima ndio hujenga Jamii na si kauli za ndio mzee. Inatia hasira kuona mtu analeta upuuzi wake hapa eti BBC wanaleta uchochozi. Substantiate huo uchochezi wa BBC
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…