Nani yupo nyuma ya BBC Swahili?

Bossie mtoto

Member
Jul 6, 2020
85
12
Kama tunavyofahamu wote kuwa BBC Swahili ni chombo cha habari kinachoripoti habari za ulimwengu wa njia ya kiswahili ambayo ni lugha ya Taifa letu Tanzania.

Kwa muda mrefu sasa chombo hiki kimekuwa kikiripoti taarifa zinazotokea ndani ya nchi kwa njia inayoleta ukakasi kwa watanzania hasa wazalendo wa nchi yetu pendwa Tanzania.

Dunia nzima ilikumbwa na janga la homa ya mapafu COVID-19 ambayo imekuwa gumzo duniani kote ikipelekea maisha ya watu kubadilika na tabia mpya kuzaliwa.

Katika kupambana na janga hili lililotishia sana maisha ya watu, wizara ya Afya iliyochukua tahadhari zote kama zilivyoelekezwa na wataalamu mbalimbali wa afya ndani na nje ya nchi. Jitihada hizi kwa mara nyingi zilibezwa na kuhujumiwa kupitia chombo cha habari cha BBC Swahili kwa kuripoti habari zenye kutia hofu Watanzania na kukosoa utendaji kazi wa wizara ya afya hapa nchini.

HII INAPELEKEA KUHOJI NI NANI YUKO NYUMA YA BBC SWAHILI
Ni kweli kwamba hamna anayewapangia BBC Swahili waripoti nini, lakini pia wajue tuna ruhusa ya kuhoji wanachoripoti hasa kama kina maslahi na nchi yetu.

Kuna mambo mengi yaliyofanywa na Rais wa Tanzania mheshimiwa John Magufuli kwa kipindi cha miaka mitano ya muhula wake wa kwa za wa Urais; chombo hiki kimekinga mgongo kutoongelea mambo haya kabisa huku kikiwa mstari wa mbele kuwapa nafasi wale wanaoonesha nia ya kuikosoa na kupinga Serikali ya Tanzania pamoja na utawala wa rais Magufuli.

Wakati huu ambao vuguvugu la uchaguzi linaendelea kupanda na kila kona gumzo kuu ikiwa ni uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020, yameonekana matukio mengine ambayo sio ya kufumbia macho hasa kutokana na sintofahamu kwamba chombo cha habari cha BBC Swahili kinafanya vitu hivi kwa ajili ya kumnufaisha nani hasa!

Katika kipindi ambacho Tanzania imekuwa kwenye mapambano na janga la COVID-19, muhubiri mmoja hala nchini mwenye maelfu ya wafuasi ambaye ni mwanzilishi na msimamizi wa makanisa ya Ufufuo na Uzima duniani kote, Askofu Josephat Gwajima alikuwa mstari wa mbele akitoa elimu kwenye jamii kupitia vipindi vya ibada kanisani kwake.

Siku ya Jumapili tarehe 05.07.2020 BBC Swahili kupitia ukurasa wao wa Twitter walichapisha habari inayolenga kukanusha kile Askofu Gwajima alichosema kuhusu hatari ya mionzi ya 5G na jinsi unavyoathiri afya ya seli katika mwili wa binadamu.

Leo tena tarehe 10.07.2020 BBC Swahili imechapisha taarifa ya kuondolewa kwa ujumbe unaofanana na huo kwenye ukurasa wa Instagram wa Askofu Gwajima. Hii bila shaka ni kuijulisha dunia mafanikio ya jitihada zake za kutaka kile alichokiongea Askofu Gwajima kisisikike kwa watu duniani kote.

Ikumbukwe kuwa Askofu Gwajima ni mtia nia wa kiti cha Ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi CCM katika jimbo la Kawe- Dar es Salaam. Hii imezua sintofahamu kwa maelfu ya watu nje na ndani ya nchi wanaompenda na kumfuatilia Askofu Gwajima huku wakiamini ni mtu ambaye amejitoa sana katika kipindi kigumu cha janga la Corona hasa ukizingatia hofu iliyokuwa imetanda.

HII IMEPELEKEA KUHOJI TENA NANI ALIYE NYUMA YA BBC SWAHILI?

Je, kuna mtu ndani ya Tanzania ambaye anawaza kufanya hivyo kutomchafua Askofu Gwajima na kuondoa imani kubwa iliyo kwa wananchi juu yake?

Je, BBC mliwezaje kufahamu kuwa ujumbe umefutwa kwenye ukurasa wa Instagram? Hii inaleta maana kwamba jitihada zote za kuondoa ujumbe huo zimefanywa nanyi..nani hasa anawatuma au anawaomba kufanya hivyo.

Je, Vyama vya Upinzani ndio vinafanya jambo hili? Kwanini BBC Swahili mtumike kisiasa katika jambo hili?

Je, hamuoni wafuasi wenu wanafatilia taarifa kwenye kurasa zenu watapunguza mapenzi nanyi hasa ukizingatia kuwa wapo watu wengi ambao wasingependa kabisa Askofu Gwajima aonewe?

Je, hamuoni kuwa mnachofanya ni shambulio binafsi ambapo chombo cha kimataifa kama BBC Swahili kufanya hivyo ni kushusha hadhi yenu na kutia doa ubora wa taaifa zenu?

Ikumbukwe watu wenye uhusiano wa moja kwa moja na BBC Swahili wanajulikana na tungependa serikali iwachunguze na kuangalia mahusiano yake na jambo hili. Hatutakubali hujuma za aina yeyote kwenye nchi yetu.

Kuona mabaya tu ya nchi na ukatafumbia macho mazuri ya yanayofanyika kila siku ni ujumbe wa aina yake kuonesha uadui wa kimaslahi au kutumiwa na mtu au kundi lenye chuki binafsi.

USHAURI WANGU
Endeleeni kuripoti habari zenye kujenga na kuelimisha. Acheni taarifa zenye mashambulio binafsi kwa mtu. Hii kamwe haitawajenga, kumbuka BBC ni taasisi, hii chuki itaota mpaka ndani ya taasisi.

Mzalendo
Mwl James Katunga
 
Mnakoseaga sana kufikiri kuwa nchi inapigwa vita na mataifa makubwa duniani sijui ni kukosa exposure au nini ? Mnaelewa hayo mataifa yametuacha nyuma sana zaidi ya miaka 150 mbêle? Walipo wao leo sisi tutafika labda baada ya miaka 200. Halafu eti watuonee wivu... Huwa nashangaa sana
 
Achana na hao wabaguzi wa dini, wanajiona sio Watanzania tena. Mimi ningekuwa raisi nawapiga ban kuingia nchini.
 
Umetulia kuandika lakini nyama hazitoshi mkuu, hii ni mada ambayo ukikaa na watu wako wa karibu mnaichambua na kuimaliza, mwishowe unakuja kutambua you can change nothing , so better hold on to your business n nothing more
 
Mbona nyinyi mnaitumia TBC ccm ,mbona nyinyi mnawatumia polisi ccm watu awasemi ,ina maana mnataka kulazimisha Dunia nzima wawe na akili kama zenu za kusifu na kuabudu,imekula kwako hiyo ifungieni tu hiyo BBC.
 
Nimekuelewa vizuri sana mwalimu, watu wengi hawajui kwa nini Vyombo vya habari kama BBC huwa viko makini sana kuripoti na kuandika kuhusu nchi nyingine kuliko nchi zao. Ukweli ni kwamba njia pekee ya kuwagawa watu ni kuamua wampende nani na wamchukie nani. Ili kupenyeza maslahi yao. Na vyombo vyenye ustadi wa kufanya hivyo ndio kama BBC.
 
Back
Top Bottom