Uchaguzi 2020 Uongo na Upotoshaji huu wa BBC London kuhusu Tanzania kipindi hiki cha kampeni una maana gani? Sio mbinu za mabeberu? Wapi weledi wa ki-BBC?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,443
113,452
Wanabodi,

Kati ya vyombo vyote vya habari duniani, chombo kikuu kabisa cha kuaminika, kwa sisi Anglophone Africa ni our colonial master, The British na shirika lao la habari la kibeberu la BBC London, na kwa Francophone Africa ni France na RFI na F24 TV. Sasa inapotokea chombo kama BBC London, Wakaripoti, kitu cha uongo, kwa upotoshaji kwa kukosa weledi, nani atakuwa mkweli?

Angalizo: Kutokana na umaarufu na heshima ya BBC, akitokea mwandishi tuu wa kawaida kama mimi kuikosoa BBC, wengi bado wataamini BBC is always right, na mimi ndie niko wrong, hawaamini kama BBC BBC inaweza kuwa biased kama kwenye story hii, kusema uongo, inaweza kupotosha, na inaweza kuripoti jambo fulani bila kufuata weledi wa kihabari.

Naomba kuwathibitishia kuwa japo ni kweli BBC ni weledi, lakini katika vita ya Kiuchumi na kutishiwa kwa Maslahi ya mabeberu, hata BBC huwa inaweka weledi pembeni, kutangaza uongo, upotoshaji kwa Maslahi ya mabeberu.

Huko nyuma mifano ipo ya BBC kusema uongo na kupotosha, imeshitakiwa mahakamani, imehukumiwa na kukutwa na hatia, imeomba radhi, na kulipishwa faini, hivyo katika upotoshaji wa jambo hili, BBC iombe radhi, vinginevyo sisi Tanzania tusikae kimya, tukanushe na kuinyoosha habari yenyewe.

Upotoshaji wenyewe ni huu
Uchaguzi 2020 - BBC Swahili wamesema kwenye makubaliano yetu na kampuni ya uchimbaji madini ya Barrick kwenye zile asilimia ni kama tumepigwa.



Nimeisikiliza BBC Swahili, kwanza makala yenyewe ni very biased kwa kujadili baadhi tuu ilani za baadhi ya vyama, na kuviacha vyama vingine. Huwezi kufanya analysis ya ilani za vyama, ukaiepuka ilani ya CCM ambayo ndicho chama tawala.

Pili BBC ni waongo, hakuna mkataba wala makubaliano ya 2017, wala 2019, bali mkataba ni mmoja tu, ule uliosainiwa Ikulu Jijini Dar es Salaam January 2020!. Yale ya 2017 yalikuwa ni mapendekezo tu na ya 2019 ni mapendekezo tuu, mkataba ni mmoja tuu wa January 2020!. How come BBC Swahili missed these facts?. BBC Swahili Iache Uongo!.

NB, uongo kama huu wa BBC pia uliwahi kuletwa mwanasiasa fulani, baada ya kuona makubaliano yamekuwa initialed, akaandika mkataba umesainiwa!, BBC nao wakaingia kichwa kichwa na kuamini mkataba umesainiwa!, wanaweza kuandika makala ndefu namna hiyo bila ku double-check na ku cross-check kuibalance makala yao na wahusika wa wizara husika? Huku ni kukosa weledi! Sasa kama BBC London inaweza kukosa weledi wa kiwango hiki, nani atakuwa mweledi?

Sio kwamba najidai, lakini kwenye mgogoro wa makinikia ya Acacia, hakuna mwana JF aliyeandika na kufuatilia kama mimi, na kwa jinsi nilivyomsikia Waziri Prof. Kabudi na Rais Magufuli, kuna maeneo ninaamini, ninayafahamu vizuri zaidi kuliko hata wahusika wenyewe wa kwetu, kwasababu issues nyingine ni issue ndogo tuu za lugha za watu, na watu wanaingizwa chaka, kama ilivyoelezwa kuwa tutagawana economic benefits pasu kwa pasu, tukaelezwa tutagawana faida, profits 50/50 kitu ambacho sii kweli.

Hata Mtaalamu wa Madini aliyehojiwa naye ni muongo tuu na mpotoshaji.
Kwenye hili la Mtaalamu, naomba kuheshimu mawazo ya yule Mtaalamu kwa kiasi kikubwa yuko right ila na yeye pia ni muongo baadhi ya maeneo na mpotoshaji.

Uongo mkubwa wa Mtaalamu ni ameshindwa kutofautisha Acacia, Barrick na Twiga. Baada ya Barrick kuinunua Acacia, ofisi zote za Acacia zilizokuwa London na South Africa, zilifungwa.

Accounts zote za Acacia zilizokuwa London na South Africa zilifungwa, Ofisi za Twiga ziko Tanzania tuu, na accounts za Twiga zina bank na City bank ya Tanzania.

Kwenye huu ubia, Barrick anamiliki 84%, na Tanzania anamiliki 16%, Barrick kama Barrick bado yuko huru kuwa na ofisi zake popote duniani na ku bank fedha zake na benki zozote!.

Wito kwa serikali yetu
Naiomba serikali yetu ikanushe uongo huu wa BBC London kuihusu Tanzania haswa kipindi hiki cha kampeni. Dr. Abbas, hili usilinyamazie. Tukinyamaza, dunia itawaamini BBC wataonekana ni wa kweli.

Waelezeni BBC London na dunia ielewe kuwa hakuna makubaliano mawili kati ya serikali yetu na Barrick, makubaliano ni mamoja tuu, mkataba ni mmoja tuu, ambapo, japo tumepigwa fulani, lakini Tanzania ndio wafaidika wakubwa wa mkataba huo!.
Ofisi za Twiga ziko Mwanza Tanzania, na Accounts za Twiga ziko City Bank ya Tanzania!.

Namalizia kwa hili swali, Je, uongo na upotoshaji huu wa BBC London, kuhusu Tanzania kipindi hiki cha kampeni, kwa kuiepuka ilani ya CCM, kujadili ilani za Chadema na ACT tuu ni wa kawaida tuu kwenye media, au una maana gani?

Tukitafuta kitu kinachoitwa the motive behind, haiwezi kuwa ni mbinu za mabeberu? Wapi weledi wa Ki-BBC?

Paskali
Kwa wanaopenda kujielimisha kuhusu Hili karibu mitaa hizi
Kuzuia mchanga wa dhahabu, Magufuli anastahili pongezi. Tusiishie kwenye madini tu, na gesi je?
Kupata Maendeleo ya Kweli, Tanzania Inahitaji Systems Not Dramas, Ze Comedy na One Man Shows!

Serikali yazidisha kibano kwa Acacia, NEMC yasimamisha shughuli za mgodi, Acacia yasalimu amri kwa kusitisha kesi zote, yasubiria PUSU ya Barrick

Maendeleo ya kweli Tanzania yataletwa na Elimu na Ukweli. Tusidanganye, Tusidanganywe, Tusidanganyike!

Wataalamu Hawa Wachunguzwe!,Jee Kuna Posibility Walihongwa Kutoa Ripoti Kuwa "Tanzania Hatuwezi?!".

A Compromised Possibility: Iweje Ripoti ya Kamati ya 2 iibukie Acacia-London kabla ya kwa Magufuli?

Acacia Yaikana Barrick Mchana Kweupe!. Yatoa Press Release na Kumruka Barrick Kuwa Haijui Chochote Kuhusu Makubaliano Yoyote na Tanzania

Dola Milioni 300 zetu za kishika uchumba cha Acacia, danadana zinaendelea. Je, tutalipwa kweli au tunatapeliwa?!. Rais Magufuli anaweza kutapeliwa?

Hongera Serikali yetu, kuwatosa Acacia kwa kutowatambua huu ndio uanaume!. acacia kula jeuri yake, faces hostile take over, soon itakuwa kwishney!.

Leo ndio leo, ni deadline ya Barrick kutangaza kifo cha Acacia kwa neno moja tuu "PUSU" (Put Up or Shut Up). ni kubali ufe, kataa ufe!, no option!.

Je, wajua kuwa mazungumzo yetu na Barrick ni mazungumzo tu? Mwenye uamuzi wa mwisho ni Acacia!, Kwanini hakushirikishwa?!. Je, Tutalipwa?.

Japo Kazi ya Upinzani ni Kupinga, Lakini Sio Kupinga Kila Kitu, Kwenye Maslahi Ya Taifa, Tutangulize Utaifa, Tuwe Wamoja, Wakweli na Tusipotoshe.
 
BBC swahili hamna kitu Walipofika kueleza sera ya madini ya Chadema walitoroka kueleza kile kipengele cha kusema Chadema ikishika madaraka ikikopa taaissi za kimataifa itaweka rehani ardhi yenye madini kama dhamana!

Hilo BBC wamelikwepa baada ya kuuona moto wetu CCM kukataa wakaona ni kaa la moto la kuua Chadema hawakuongelea

CCM chama tawala sera zote za vyama tunazo tena kichwani
 
Wewe ktk uandishi wako unazingatia ethics za taaluma yako ya uandishi? mbona ni wazi umekuwa mwandishi anaetamguliza maslahi ya tumbo lake ktk kila habari unayoiandika? Una credibility gani ya kuwanyooshea kidole BBC? Acha waripoti kwa maslahi yao kama wewe unavyoandika kwa maslahi ya tumbo lako!
 
KWA NINI SIKU IZI BAROZI ZA ULAYA BAADA YA KUONA VYAMA FLANI VINAFANYA KAMPENI KWENYE MISURURU YA WATU, HAZITOI NYO JUU YA KUENEA NA UWEPO WA KORONA TANZANIA, KAMA KIPINDI KILEE? AU NAO WANAKUBALI KORONA IMEISHA??
Nchi zilichogundua ni kuwa serikali ni wakweli kwenye issue ya Corona kuwa Lisu na chadema ni waongo na hiyo ina impact kubwa sana kuwa they are not reliable and trustworthy.

Imemjengea credit Magufuli na kumbomoa Lisu kwenye international community
 
Back
Top Bottom