Pamoja na kutoa elimu ya haki za msingi bado inabidi CDM waje na Roadmap makini,
1-Wawaache wana Igunga wachague mtu wao hata kama ni DJ wa pale Sakao Bar alipofanyia kikao RA, wao waangalie je anakubalika kwenye jamii?
2-Wapate mtu anayejua kuupepeta kwa kisukuma na kiswahili kama Nyani Ngabu...Sorry.. (Kiingereza sio dili kule Igunga)
3-BAVICHA ijikite katika mambo yafuatayo,
- Waongelee kwa nini kuna Bei mbovu ya pamba inayosimamiwa na serikali ya CCM pamoja na mzani wa kuchakachua uliokubaliwa na serikali
- Shida ya maji kwa wakati wote ambapo kuna mabwawa makubwa mawili yanayozunguka Igunga, enzi za nyerere maji yalitolewa bwawa la Igogo yakapelekwa Igunga-Mbutu-Ibuta etc leo hii yanaishia Igunga tu na si maji salama,
- Daraja la mto Mbutu ni mtaji, wanainchi wengi wamekuwa wanashindwa kupata huduma za msingi kipindi cha mvua na CDM ikiweza kuja na suluhisho hilo basi kura za vijiji vyooote ng'ambo ya mto ni zao (Hili ni muhimu sana na RA alilitumia sana kuwadanganya watu wa Igunga)
- BAVICHA itahadhalishe na kuelimisha wana Igunga kuhusu wawekezaji uchwara wanoweza kuvamia Ardhi yao..nasikia wananyemelea,
- CDM watoe kipaumbele wa barabara ya Igunga - Itumba, Igunga - Nkinga, Igunga - Sakamaliwa, Igunga - Igurubi etc
- CDM wawaeleze wanainchi ni jinsi gani watasukuma gurudumu kupeleka Umeme vijiji vya ng'ambo ya mto mbutu,sakamaliwa, Ibuta, Hindishi, Ng'wanyagula, Bukama, Igurubi, Itumba, Makomero, Mwabakima etc
- BAVICHA wasisite kuelezea jinsi gani watafufua kilimo cha mpunga wa kumwagilia pale Mwanzugi
Mashule kukosa walimu, Nyumba zao Mbovu, Huduma ya Afya duni, vijiji vingi havina dispensary...(kwa leo inatosha na wengine wachangie)