CHADEMA wafanya Press Conference; yaliyojiri Singida- Ndago na yatokanayo

Tumaini Makene

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
2,642
6,071
UPDATES

Nimepata taarifa punde kutoka kwa Kamanda Shabaan kuwa Kamanda Waitara anashikiliwa na polisi. Ilikuwa nbi baada ya kuandikisha maelezo yake polisi. Kulikuwa na understanding kuwa baada ya maelezo yake angeondoka, kama kuna watu wengine ambao polisi wanawahitaji pia kwa ajili ya maelezo basi wangetafutwa kwa muda mwingine.

Taarifa zinasema amekamatwa baada ya gari moja linalodaiwa kuwa la Mkuu wa Wilaya kufika hapo. Inaonekana yametolewa maagizo. Kichaka kinachotumika ni 'maelekezo na maagizo kutoka juu'. Juu ndiyo nani au wapi ni kama hadithi inayomhusu ELUNGATA.


&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&


Wakuu Kamanda Mwita Mwikwabe Waitara amemaliza mkutano na waandishi wa habari punde mjini Singida na sasa hivi yuko kwa R.P.C akimaliza kuandikisha maelezo. Kwa wale wasiojua, Waitara ndiye mratibu wa operesheni ndogo ya ukaguzi wa uhai na ujenzi wa chama inayofanyika Mkoani Singida.

Operesheni hiyo ni maandalizi ya operesheni kubwa itakayofanyika baade mkoani Singida, kama moja ya mikoa mitano, Dodoma, Manyara, Morogoro na Iringa, ambayo itakuwa mikoa ya mwanzo katika operesheni inayopagangwa kufanyika kufuata kanda mbalimbali kama zilivyopitishwa na kuazimiwa na kikao cha Kamati Kuu hivi karibuni.

Shuguli nzima ya chama taifa inayoendelea mkoani Singida iko chini ya Waitara. Lakini baada ya kupanga kufanyika kwa mikutano ya hadhara katika maeneo mbalimbali unakofanyika ukaguzi na ujenzi wa chama, akaomba baadhi ya viongozi wa chama wahudhurie mikutano hiyo kuzungumza na wananchi.

Miongoni mwao walikuwa ni Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, John Mnyika, Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Ezekia Dibogo Wenje na Mjumbe wa Kamati Kuu, Mchungaji Peter Msigwa. Kutokana na udhuru na majukumu mengine, viongozi wengine hawakufika.

Press conference imefanyika kwa kufana. Wanahabari wameuliza maswali kadri walivyotaka kufahamu. Wamepewa majawabu.

Mpaka sasa inatambulika kuwa baadhi ya maofisa waandamizi wa polisi Singida waliokwenda na kundi la askari wengine kutoka mjini kuongeza ulinzi jana katika eneo la mkutano, wakiitikia wito wa kufanya hivyo kutoka kwa Waitara aliyemtaarifu R.P.C na OCD, juu ya lile kundi la wahuni lililoonekana kupangwa kufanya fujo, wana-understanding sahihi ya jinsi mkutano wa CHADEMA ulivyofanyika na kumalizika kwa amani.

Hapa chini nimeweka taarifa ya Kamanda Waitara kwa wanahabari leo Singida; Mbali ya kuwawekea hii taarifa, kupitia thread hii, propaganda nyepesi kama za akina Nape na wengine, zitajibiwa.

Hapa ni mahali pazuri pa kujadili hoja kwa hoja. Mtu makini hawezi kukimbia mijadala. Watu wa hovyo, wasiojua umuhimu wa kujadili kwa hoja ni kama yule mwanasiasa wa jana alivyokimbia mjadala kwa kuweka kikundi cha watu kudhibiti hoja kwa mawe. Ikashindikana. Watu hawa ni hatari. Bahati mbaya kwao na bahati nzuri kwa Watanzania, wanasiasa wa namna hii wako katika siku zao za mwisho.

Lakini pia zipo taarifa kuwa aliyechukua mkanda wa video wa matukio yote ya jana, tangu mwanzo mpaka mwisho, anasakwa. Wanatamani kweli kuzitia mikononi mwao chip zinazoonesha matukio ya jana. Jinsi wahusika walivyokuwa wakitamba na kufanya fujo mbele ya polisi, bila kuchukuliwa hatua yoyote. Ilemela-type (tukio la akina Machemuli na Kiwia) so did I say here yesterday.

Wanatamani kweli kweli chip inayoonesha mkutano ulivyofanyika kwa amani kabisa, hoja zikashushwa, wananchi wakashangilia, wakamtaka Waitara kuhakikisha viongozi kama Mnyika na wengine wanarudi maeneo hayo kutoa elimu mara kwa mara. Hiyo ilikuwa ni baada ya lile kundi kuondolewa mkutanoni.

Wamechelewa. Kama ambavyo inatambulika kuwa wanasaka chip hizo, pia inatambulika walivyojipanga kufanya propaganda kwenye vyombo vya habari kesho kuwa viongozi wa CHADEMA walizomewa na hawakufanya mkutano. Wamechelewa sana.

Si wananchi w Ndago pekee, bali dunia nzima itawashangaa hasa wale watakaonasa kwenye mtego wa propaganda hizo.

Labda nimalizie maandishi haya mengi kwa sasa bila kuwachosha, kwa kuuliza, just rhetorically; hivi Nape Nnauye anaposema ugaidi, bila shaka anakuwa anamaanisha matukio yale ya Arumeru Mashariki, ambako mpaka sasa viongozi wake, wanashikiliwa kwa kumchinja, sorry, kumteka na kumchinja kiongozi wa CHADEMA?

Au anaamanisha jinsi viongozi wake wanavyoshikiliwa kwa kumfuata ofisini Mbunge Peter Msigwa na kutaka kumuua. Baada ya njama za kwenye mkutano wa jana yake Mjini Iringa kushindikana ambako pia walipanga kama walivyofanya jana huko Ndago?

The last one, but not least, is very interesting to note; Je Nape anamaanisha nini...Katibu Mkuu wake Wilson Mkama ambaye amenukuliwa akilalama kukosa kazi kwa kupokwa mamlaka, aliwahi kukurupuka na kufunua mpango wao wa kupeleka vikundi vyao vile vinavyofanyia kazi kwenye Msitu wa Mabwepande.

Katika hali ya kukata tamaa, akitumia nyaraka feki za kutengeza wao wenyewe, akalia ooh, CHADEMA wameleta magaidi. Lakini hivi karibuni alipoitwa kutoa ushahidi kwenye kesi ya Igunga, akasema CHADEMA haijawahi kuleta magaidi, alas!

Nway, je labda Nape anaposema ugaidi, atakuwa anamaanisha namna ambavyo viongozi wa CCM wanatuhumiwa kuwakata mapanga wabunge wa CHADEMA, Machemli na Kiwia, mbele ya polisi? Kisha hawataki kufanya uchunguzi makini, kuwakamata watuhumiwa ambao majina baadhi yametajwa na namba za magari yaliyowabeba zikiwekwa wazi hadharani

Au alimaanisha hivi...walimtimua Tambwe Hiza kwa sababu ile kazi ya kutofungamana na ukweli alikuwa haifanyi vizuri kama walivyotaka wao mabingwa. Sasa kikohozi kimempata mwenye pumu. Kuwa adui wa kudumu dhidi ya ukweli.


Hili ndilo tamko lililotolewa na Waitara leo;



CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI




Tamko Kuhusu Yaliyojiri Katika Mkutano wa Hadhara wa CHADEMA Uliofanyika Kata ya Ndago Siku ya Jumamosi Tarehe 14 Julai 2012

1. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kiliandaa mikutano ya hadhara katika Jimbo la Iramba Magharibi. Mikutano hiyo ilitolewa taarifa polisi na jeshi hilo lilitoa baraka zake kama utaratibu wa sheria unavyotaka kwa barua yake ya tarehe 12 Julai 2012 Kumb. Na. KIO/B1/1/VOL.V/268

2. Mkutano wa kwanza ulipangwa kufanyika katika Kata ya Ndago katika viwanja vilivyo karibu na kituo cha mabasi ambapo pia ni hatua chache karibu kabisa na Kituo cha Polisi Ndago. Mkutano huu ulipangwa kuanza saa nane mchana.

3. Msafara wa kitaifa unaofanya ziara ya ukaguzi wa chama, katika mkoa wa Singida chini ya uratibu wa Ofisa wa Sera na Utafiti Makao Makuu, Mwita Mwikwambe Waitara, (ikiwa ni maandalizi ya operesheni nyingine kubwa mkoani humo itakayofanyika baadae), uliwasili katika eneo la Mkutano majira ya saa tisa na nusu alasiri. Tulikuta wananchi wengi wakiwa wanatusubiri. Kabla ya Mkutano kuanza tulipewa taarifa kwamba kuna kikundi cha vijana kimeandaliwa kuvuruga mkutano wa CHADEMA kwa kufanya fujo, ikiwemo kurusha mawe ili mkutano huo usifanyike. Suala hilo lilielezwa mkutanoni mapema na Mheshimiwa Waitara, mbele ya askari polisi.

4.
Wakati tukijiandaa kuanza hotuba, vijana wapatao wanane walianza chokochoko kwa kutoa matusi na punde mawe yakaanza kurushwa kutoka sehemu mbalimbali. Wakati fujo zinaanzishwa na kile kikundi, Mheshimiwa Waitara alikuwa bado anazungumza na wananchi kuwaandaa kusikiliza wazungumzaji wengine. Vurumai hiyo ilizimwa na wananchi wenyewe wa Ndago waliokuwa na hamu ya kusikiliza ujumbe wa viongozi wa kitaifa wa CHADEMA.

5. Kwa kweli tunawashukuru wananchi wengi wa Ndago walioonesha ujasiri mkubwa kuweza kuwaondoa vijana wale eneo la mkutano, kisha mkutano ukaendelea, huku wananchi wakionesha kila hamasa ya kufurahia hoja kutoka kwa wazungumzaji, akiwemo Mheshimiwa John Mnyika, ambaye aliombwa ahudhurie ziara hiyo kwa nafasi yake ya Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA.

6. Mpaka tunamaliza mkutano huo ambao wananchi waliufurahia sana kwa namna ulivyohutubiwa kwa amani na utulivu huku wazungumzaji wakijenga hoja juu ya mstakabali wa jimbo na taifa lao kwa ujumla, mamia ya wananchi waliohudhuria walitaka tuendelea kuhutubia, lakini tulibanwa na ratiba ya kuwahi mkutano wa pili, eneo la Kinampanda.

7. Lakini kutokana na vurugu hizo zilizokuwa zikisababishwa na kikundi cha vijana ambao tayari ilishatolewa taarifa yao kwenye mkutano huo, lakini askari waliokuwepo hawakuthubutu kuchukua hatua, tulilazimika kuomba msaada kutoka kwa OCD na R.P.C, ambapo baadae wakati mkutano unakaribia kuisha tuliona gari la polisi kutoka Mjini Singida likiwa na askari waliojipanga rasmi kwa ajili ya kuzuia vurugu likifika pale eneo la mkutano, lakini wakati huo hali ilishatulia na hotuba zimetolewa vizuri.

8. Kutokana na hali hiyo ya vurugu, zilitolewa taarifa Kituo cha Polisi cha Ndago, ambapo lilifunguliwa jalada NDG/RB/190/2012. Katika jalada hilo tulitaja baadhi ya majina ya watuhumiwa waliokuwa vinara wa kundi lililokuwa likifanya fujo kwenye mkutano mbele ya askari polisi. Majina hayo ni; 1. Daniel Sima, 2. Tito Nitwa, 3. Bakili Ayubu, 4. Yohana Makala Mpande, 5. Ernest Kadege, 6. Abel John, 7. Athuman Ntimbu, 8. Martin Manase, 9. James Ernest, 10. Simion Makacha, 11. Anton John, 12. Frank Yesaya

9. Kwa hakika askari polisi wa Ndago waliokuwepo mkutanoni mbali ya kutochukua hatua yoyote dhidi ya fujo tulizofanyiwa ikiwemo kupondwa mawe na kikundi kidogo cha wahuni, fujo zilipozidi askari wote walikimbia eneo la mkutano, akabaki OCS pekee ambaye naye alionekana dhahiri kutotaka kuchukua hatua stahili. Hakuonekana kufanya juhudi zozote za kuhakikisha amani inalindwa na ulinzi unaimarishwa katika eneo la mkutano na hatua zinachukuliwa dhidi ya watu walioonekana kudhamiria kufanya fujo. Mtu yeyote makini angeweza kuona kuwa askari wale walikuwepo pale mkutanoni ‘almuradi’ tu lakini kama vile walikuwa na maelekezo maalum ya kuhakikisha hawachukui hatua yoyote katika kuzuia mpango wowote wa kusababisha vurugu na kuvunja amani.

10. Baada ya kumaliza mkutano wa Ndago kwa amani, tulikwenda Kinampanda ambako tulifanya mkutano mwingine mzuri kwa amani kabisa, ambapo mbali ya wananchi kuwa wametusubiri kwa hamu kubwa na kutusikiliza kwa makini hoja zetu, polisi katika eneo hilo walitupatia ushirikiano mzuri tangu wakati tunafika mpaka tulipomaliza mkutano huo.

11. Jioni wakati tumerudi hotelini, tukasikia kuna taarifa zinasambazaa kuwa kuna mtu/watu wamekufa katika eneo la Ndago. Habari hizo zilikuwa zinakanganya kwa sababu zilikuwa zikitaja idadi tofauti tofauti. Lakini kwa vyovyote vile kama ni kweli kuna tukio la mtu kufariki, CHADEMA tunasikitika sana kwa tukio hilo la uhai wa mtu.

12. Tunalaani taarifa zinazozidi kusambazwa ambazo zinawataja polisi kuwa wanatuhusisha CHADEMA na tukio la mtu aliyefariki. Hii ni ajabu kubwa kwamba tumetoka kwenye mkutano ule kwa amani kabisa mpaka tumemaliza mkutano wa pili kwa amani na polisi wakiwepo sehemu zote mbili, kisha tunasingiziwa masuala ambayo wenyewe hatukuwa na habari nayo tangu mkutano wa kwanza ukiwa unaendelea mpaka mkutano wa mwisho ulipomalizika.

13. Kutokana na habari hiyo ya kifo cha mtu inavyoenezwa kwa kuihusisha CHADEMA, tumebaini kuwepo kwa mbinu na mikakati ya chama tawala pia vyombo vya dola vikihusika kutaka kuwatisha wananchi wa Singida, Watanzania wote wapenda mabadiliko na viongozi wa CHADEMA katika mkoa huu, wasifanye kazi ya kisiasa kwa kuwabambikizia tuhuma na kesi na pia kuwafanya waonekane ni watu wa vurugu.

14. Tunapenda kusema hapa kuwa njama hizo hazitafanikiwa. Zitashindwa kama zilivyoshindwa njama zingine zote ambazo zimekuwa zikifanywa na vyombo vya dola, viongozi wa serikali na chama tawala dhidi ya CHADEMA na vuguvugu la mabadiliko nchini.

15. Tunawataarifu wananchi kuwa ratiba ya kufanya Operesheni nyingine kubwa katika Mkoa wa Singida, ikiongozwa na Katibu Mkuu, Dkt. Willibrod Slaa, itafanyika baadae kama ilivyoazimiwa na kikao cha Kamati Kuu.


Imetolewa leo Singida, Julai 15, 2012 na;

Waitara Mwita Mwikwabe

Ofisa wa Sera na Utafiti CHADEMA Makao Makuu

UPDATES

Nimepata taarifa punde kutoka kwa Kamanda Shabaan kuwa Kamanda Waitara anashikiliwa na polisi. Ilikuwa nbi baada ya kuandikisha maelezo yake polisi. Kulikuwa na understanding kuwa baada ya maelezo yake angeondoka, kama kuna watu wengine ambao polisi wanawahitaji pia kwa ajili ya maelezo basi wangetafutwa kwa muda mwingine.

Taarifa zinasema amekamatwa baada ya gari moja linalodaiwa kuwa la Mkuu wa Wilaya kufika hapo. Inaonekana yametolewa maagizo. Kichaka kinachotumika ni 'maelekezo na maagizo kutoka juu'. Juu ndiyo nani au wapi ni kama hadithi inayomhusu ELUNGATA.
 
Huyu Mzinzi hafai hata kuwa mpiga debe wa daladala. 2015 hana kazi, aende akarambe miguu ya Vasco Da gama, a.k.a The Explorer
 
Watanzania tuendelee kuamini kuwa jeshi la polisi liko kulinda usalama wa raia? Kwa jinsi mambo yanavyokwenda upo uwezekano wa wananchi kutotaka kabisa kuwa karibu na askari polisi?
 
Nitarudi hapa baadaye, kwanza ngoja nielekee kwenye Sarakasi za Kova.


Saigon

Jamaa wataogeleamo sana. Ukisikia maji yamezidi unga ndiyo hii...plus kungfuu, judo, karatee, bahati mbaya wamechelewa kujua kuwa tuko level za Bruce Lee. Level za juu sana, wao ndo kwanza...wataogelea sana.
 
nilipoona Mwigulu kajaza tape za Mwl.Nyerere kwenye gari yake nikajua Iramba tumepata mbunge japo kapotea chama, mara ghafla akaanza kutumwagia pesa chafu mpaka makanisani, nikashindwa ku-link kati ya tape hizo na pesa chafu........sasa ameanzisha genge la kuua kabisa, pls Mwigulu nisaidie ku-link tape za Nyerere, Skafu ya Tz na haya mauaji unayochochea
 
Thanks wanajf kwa taarifa za ukweli na uhakika, hapa ndo nyumbani, nimeijua Tanzania vizuri through jf, nimeijua ccm na ukatiri wao through jf, in god we trust
 
Nepi hawezi kujibu chochote kuhusu hizi tuhuma , mwiguru pia ni mtuhumiwa inabidi atoe maelezo ya kilichotokea Ndago
 
Tunasema mara zote polis wanafanya kaz kwa ubaguzi na kwa kuipendelea ccm! Hawa ni mafisadi na wanatuibia kodi zetu! Nachelea kusema mwigulu ni janga!
 
Hawa Magamba wanajitaarishia wenyewe kesi hapo 2016 baada ya sisi walalahoi kuichukua hii nchi lazima hawa mafedhuli tuwaburuze kwenye sheria na kuwasweka ndani.

Mkuu Mzalendo

Hujakamilisha mapendekezo yako na ushahidi kwa ajili ya Ocampo List... Do it right now bro. Saidia mabadiliko hapo ulipo.
 
Tuna shukuru kwa taarifa hii...CCM wajiangalie sana na mambo yao,kwani kila mbinu chafu wanayofanya kwaajili ya kuichafua CDM ina kula kwao hiyo wanachauri CCM na Nape, kuwa makini sana maana tunawailia pozi.
 
Back
Top Bottom