Basi la Shabiby lapata ajali Makunganya Morogoro likienda Dar

Bornvilla

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
924
271
Hakuna kifo hadi sasa lakini watu wameumia na hakuna huduma yoyote waliyopata.Polisi hawajafika na hata ambulance haijafika. Kuna watu wawili wamebanwa ndani ya basi msaada wa haraka unahitajika. Kwa wale wenye ndugu zao basi wajitahidi kuwatafuta kwa simu ili wajue hali zao.
Source:Radio Imani.
 
Shabiby ya kutoka wapi kwenda wapi?
Kuwa specific bana!...si wote tunaishi huko Kizimkazi!
 
sOURCE rADIO iMAN.........ATALETAJE HABARI KAMILI....SIIBAGUI RADIO NATAKA KUOONESHA UJINGA WA MCHANGIAJI WA KWANZA HAPO!
 
Mungu wangu!!Hizi ajali zitatumaliza watanzania aisee!!Imekuwaje?Imetokea wapi hiyo tena jamani?Duh!!
 
Kunradhi: Shabiby ilikuwa inatoka Dodoma kuelekea Dar es salaam. Na ajali imesababishwa na utelezi kutokana na hali mvuamvua.Baadhi ya majeruhi wamekili dereva hakuwa akiendesha kwa kasi.Ni katika kona hapo iliyumbayumba na kuanguka. Mungu awape tahfifu na kuwaponya abiria wote wa ajali hiyo na ajali zingine zinazozidi kuripotiwa na zile zisizoripotiwa.
 
yani hao majerui baada ya kunusurika, wameamua "kumkill" dereva?
 
Nipo eneo la makuda kihonda Morogoro ambapo kunàjali ya mabasi matatu Shabiby, Sumry na Alis na lory moja.

Kumekuwa na foleni kubwa sana kwani magari ya kutoka dodoma na yanayotoka dar hayapiti.

Kwamujibu wa mashuhuda kumekuwa na majeruhi kadhaa.
 
sOURCE rADIO iMAN.........ATALETAJE HABARI KAMILI....SIIBAGUI RADIO NATAKA KUOONESHA UJINGA WA MCHANGIAJI WA KWANZA HAPO!

Jamani udini hata kwenye ajali? Tujifiche kwanza katika masuala kama haya. Hata kichaa anaweza kukujulisha kuhusu msiba, hata mbwa anaweza kukujulisha kuhusu ajali ama msiba.
 
Back
Top Bottom