basi la NEWFORCE na konda wa kichina

basi la NEWFORCE na konda wa kichina

Kwa akili hizi mbona taifa litazidi kuangamia, sasa ww mchina kukagua tiketi imekukwaza nn? Ww ukipewa hiyo kazi utakubali? Au ndio utataka ya kukaa ofisini kama kawaida ya vijana wengi

wewe unadhani nimekwazwa?!, i thought there's a lesson to learn:
1. may be sisi hatuaminiki?!
2. najifunza jinsi wenzetu wasivyochagua kazi ama mazingira ya kazi.
3. unawenza ongeza fursa nyingi kadri ufikiriavyo......
 
Hii haiko sahihi, Kama kweli n mwekezaji, then hatakiwi kufanya anchokifanya huyo mchina, kwa sababu n kazi ambayo inaweza fanywa na mtanzania yeeyote, tatizo wachina wanapokuja taka kuwekeza, hawawekewi mipaka ya namna ya kuendesha hiyo biashara, ndo maana unaona mjini wanauza Maua barabarani , they should be doing the management count of the company, not low skilled jobs, hii inanyima fursa kwa vijana wetu
 
Mnaaminika vijana?????
Mnajituma mkipewa kazi?????
Heshima ya kazi ipo????

Biashara ya gari inachangamoto nyingi sana kwa hiyo ukimuachia tu mtu bora Mtanzania mwenzako itakula kwako!!!

Nimewahi kumkabidhi mtu gari ya biashara ya usafiri wa watu kama hiyo nikaja ambiwa gari hiyo ikifika iendako huwa ni bar ya mirungi bangi na vinginevyo!!!!!!!Gari ikawa inaua rotter mara kwa mara kumbe inajazwa mafuta ya magumashi...kuliko kuja kufungwa kwa murder bora mtu aajiri tu hao wanaojua maana ya kazi na chalenges za transport business

Ukweli kabisa kufanya kazi na baadhi ya vijana wa Kitanzania ni changamoto na pasua kichwa naandika haya nikiwa Mtanzania wa kuzaliwa tangu babu zangu

Tubadilike jamani kwa hawa wawekezaji kutoka nje hawana cha mtoto wa mjomba! !!!
 
Mkuu, ulichosema n sahihi, lakin kumbuka Huyu n mwekezaji, anakuja na pesa zake, anatafuta fursa, anapata na anawekeza,then kiutaratibu Kama mwekezaji anatakiwa afanye human capital investment kwa maana ya kuwafanyia training wabongo, ili waweze ku- run hiyo biashara, wakishapata training+objectives zao, watafanya kazi vizur tu na uaminifu mwingi

si kweli,Dar Kyela mchina anashuka uyole,ila anakaba kinoma kwenye mizigo,hata kilo 20 unalipia.
Sio wote mkuu, Dar - Kyela hashuki mtu.....safari mpaka mwisho.
 
huyo lazima atakuwa fundi. mabasi ya kichina huwa yana garantee na wanatengeneza wenyewe wachina. Lazima hilo gari lilikuwa na matatizo ya kiufundi
 
waache jamaa wasimamie mali zao,makampuni mengi ya mabasi yamefiriska kwa kuwaamini makondacta,iko wapi Sabco,wapi scandnavia,hood inachechemea,huwezi huamini makondakta wanamiliki mafuso na mali nyingi tu.
 
Hivi nyinyi watanzania mbona amwishi kulalamika. Mimi ni mtanzania ninaye ishi ngambo. Ina maana nisijijiri kisa mtanzania. Hii dunia ya Mungu, maisha kokote.
wewe unafanya kazi gani jombaa?
 
Nadhani huu ni ujasiri mkubwa kwa hawa ndugu zetu wa kichina kutufungua macho... unaweza kukuta huyo mchina ni graduate tena muhandis mzuri kwa vile hatuwez wote kuajiriwa bas kazi yoyote fanya..Hii inatupa changamoto kwa wavaa suti wetu wa vyuoni i mean wanasheria suti mwisho vyuoni mitahan kazi za sheria hakuna so msibweteke na degree zenu pigeni kazi km wachina la sivyo itakula kwen! Uganda madriver tax lukuki ni universty graduates so ata boda aka tukutuku kamata piga mzigo! bravo wachina
 
waafrica waliaribu sana biashara zangu kidogo nifilisike . nimeajili meneja mzungu. watu wa usafi wadada wa kichina.
na mambo yanaenda vizuri sana
 
Mkuu, ulichosema n sahihi, lakin kumbuka Huyu n mwekezaji, anakuja na pesa zake, anatafuta fursa, anapata na anawekeza,then kiutaratibu Kama mwekezaji anatakiwa afanye human capital investment kwa maana ya kuwafanyia training wabongo, ili waweze ku- run hiyo biashara, wakishapata training+objectives zao, watafanya kazi vizur tu na uaminifu mwingi

Mkuu serikali yenyewe haipeleki wafanyakazi wote kuongeza elimu! !!!!
Ukiajiriwa lazima ufanye kazi kwa miaka miwili na hiyo process waweza kata tamaa kama hukuambiwa kwa sasa pesa hakuna!!!!!

Muwekezaji yeyote huwa anataka manpower inayoweza kufanya kazi under minimal supervision na wakati huo aone faida kwa hiyo hilo la kuja kuanza kufundisha watu jinsi ya kufanya kazi sahau kwa sababu ni next to impossible na hakuna mfanyabiashara atayeweza kuanza kuwekeza huku akifundisha especially kwenye transport firm!!!!!

Labda hotelini ambapo kumuelekeza mtu kutandika kitanda haigharimu chochote!!!!
 
Hao wanasindikiza bus akimaliza kukagua anashuka, kwa Dar huwa wanashuka Kibaha.
Hili ni swali la msingi sana,wanaomshangaa mleta mada waje wajibu hili....huyu mwanamfalme aliyekamatwa na bimbwi atatumaliza...wachina sasa watakuja kuwa mpaka wazibua vyoo.
 
Wabongo wamezidi kuchagua kazi,halafu wezi sana,hata akipata training on how to run the business atakuibia tu,tumeona makampuni mengi ya mabus wahudumu tu wanajifanya miungu watu,hata tumbo likikuvuruga utajichafulia maana hawajui customer care,ndo maana makampun yanakufa taaratib scandinavia,Hood,Sabco, na sasa sumry inachechemea
 
Tanzania hakuna sheria za uhamiaji zinazosaidia kulinda wazawa (maarufu kama local content). Nchi kama mozambique, Angola, Ghana (just to mention a few) ni vigumu sana mgeni kufanya kazi.

Ifike wakati kuwe kuna justification katika kuruhusu wagenu kufanya kazi sehemu mbalimbali kuanzia makampuni makubwa mpaka biashara ndogo ndogo
 
Mnaaminika vijana?????
Mnajituma mkipewa kazi?????
Heshima ya kazi ipo????

Biashara ya gari inachangamoto nyingi sana kwa hiyo ukimuachia tu mtu bora Mtanzania mwenzako itakula kwako!!!

Nimewahi kumkabidhi mtu gari ya biashara ya usafiri wa watu kama hiyo nikaja ambiwa gari hiyo ikifika iendako huwa ni bar ya mirungi bangi na vinginevyo!!!!!!!Gari ikawa inaua rotter mara kwa mara kumbe inajazwa mafuta ya magumashi...kuliko kuja kufungwa kwa murder bora mtu aajiri tu hao wanaojua maana ya kazi na chalenges za transport business

Ukweli kabisa kufanya kazi na baadhi ya vijana wa Kitanzania ni changamoto na pasua kichwa naandika haya nikiwa Mtanzania wa kuzaliwa tangu babu zangu

Tubadilike jamani kwa hawa wawekezaji kutoka nje hawana cha mtoto wa mjomba! !!!

Yaani uko sahihi 100% nilijitutumua mzee nikanunua semi yangu nikampa jamaa nliekuwa namuamini mwaka mzima sijapata chochote mpaka nikauza kwa hasara,
Ukweli vijana wa kitanzania hawaaminiki,na ukifanya kosa la wakuwaamini ndio utajuta,watakutia mimba ambayo hutaisahau,hata hawa wachina wameshawasoma ndio maana wanafanya wenyewe,
 
Hapa Nina mpango wakuanzisha kampuni flani lakini ntaleta wafanyakazi wahindi,kwa sababu wanajua lengo la kuwa pale kazini,wanajituma na wanafanya kazi kwa uaminifu,wabongo wavivu,waongo,wezi,yaani wavurugaji tu sisi wabongo tubaki kubeba sembe na kuimba bongo fleva tu,kwa sababu ni wavivu na tunapenda starehe kuliko kazi
 
Acheni roho ya wivu. Kama haiwapendezei basi msuse kupanda hilo basi
 
Jee mtanzania anaweza kuwa kondakta wa ma bus china?
Si ndio hapo mkuu, kwani nchi hii inahitaji wachuuzi au wawekezaji 4 job creation; mbona hatujawahi kuwaona Wazungu wano uza maua, kanda mbili,mapazia i.e biashara ndogo ndogo je hao tuwahiteje "WAWAKEZAJI".
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom