Basi la Happy Nation Lapata Ajali Hedaru Laua wawili

Mungu awapumzishe pale wanapostahili marehemu wote na awaponye walio majeruhi
 
Nimekutana nayo hiyo ajari nikitokea Arusha,nilipo jaribu kuulizia mashuhuda walidai kuwa hilo gari dogo(carina) lilikuwa linayumba(inasemekana dereva alisinzia)na dereva wa basi alijitahidi kumkwepa ikashindikana ki ukweli ni viungo vimegawanyika inasikitisha.RIP
Usingizi ni kitu kizuri unapokua kitandani tu.....mimi ni dereva wa muda mrefu nikiwa njiani usingizi ukinivamia huwa sinaga jeuri lazima nipaki pembeni nilale japo kwa nusu saa inatosha sana..We fikiria unatoka Dar kwenda Chuga saa 12 asubuhi usiku wake umekesha bar asubuhi unapiga supu na beer 2 kuweka kichwa vizuri...unaenda ukifika Korogwe unakula nusu kuku na Ugali unashushia na beer tatu....mama yangu nakuapia ukifika kile kipande cha Mombo mpaka Njia Panda lazima usinziee...narudia tena LAZIMA USINZIE wengi wetu huwa tunajikaza tu kisabuni ila ukweli ndio huo...R.I.P Makamanda Gone to soon
 
Haya mabasi ni majanga na mimi ni shuhuda.

Majuzi kati, nilipata lifti kwenda Dar kwenye gari dogo (GX 100) la jamaa yangu (tulikua wa4). Alikua anaendesha vizuri tu. Hakuzidi 100km. Mitaa hiyo hiyo ilipotokea ajali hii, kuna basi jeupe hivi la kizamani liliamua kujaa upande wetu. Ile linatufikia, likafanya kama ile kwenye muvi kutupiga 'bambi' na kurudi upande wake papo hapo. Kama si uhodari wa jamaa yangu kudhibiti gari, na spidi nzuri... Uwiiiiiiiii! Labda hiki ndicho kilichomtokea Ngowi na nduguye.

RIP fellows... You both went too young!!!

Mngemfukuza mkamblock then mnampa kichapo
 
Ushauri kwa wale madereva wa mijini ambao hupata safari za masafa marefu. Ukiwa na safari ndefu kamwe usithubutu kula chakula kingi kwani husababisha uzingizi. How?....unapo kula chakula kingi damu huteremka nyingi tumboni kwenda kuyeyusha chakula (kumeng'enya)hivyo sehemu nyingine huathiriwa kwa kuwa na upungufu huo wa damu. Kichwa huchukuwa sehemu kubwa sana ya damu iliyopo mwilini hivyo unapotokea upungufu wowote basi husababisha usingizi ili kuhifadhi damu kidogo iliyopo na ili ubongo uendelee kufanya kazi kama kawaida. jambo hili hufanyika kwa masaa takribani mawili hivi tokea ule chakula chako. Hivyo, nahisi hawa jamaa wali kula chakula pale Mombo au korongwe na digestion ilipoanza ku-take place dereva akaanza kusinzia na kupoteza mwelekeo.

Jingine, unapoendesha gari kwa masafa marefu hakikisha abiria aliyepo kiti cha mbele sambamba na dereva halali kwani kisaikolojia ina mfanya dereva naye kusikia usingizi. abiri ahuyo akisinzia simamisha gari na mwombe ahamie kiti cha nyuma. Hakikisha mtu anaye kaa hicho kiti ni mpiga stori sana .

ni hayo kwa leo
 
Huyo wa upande wa kushoto kama namfahamu vile? Ngoja nipige simu nipate uhakika
 
Mkuu MSALANI huyu dogo ndio kwanza anaanza maisha na kufaidi matunda ya ujana wake bahati mbaya hizi barabara zetu zinataka umakini sana.Jana nilikuwa natoka Tanga Kabuku na gari dogo kufika maili kumi kabla ya Korogwe nikakuta na Prado imeachiwa kisawa sawa ipo katikati ya barabara nilichokifanya nikuingia machakani bahati nzuri niliweza kucontrol gari vyema.Nilipofika Makanya nikapigiwa simu na jamaa zangu wa Kabuku nikaambiwa kuna prado imezama uvunguni mwa Scania nikajisemea bila shaka inaweza kuwa ile iliyonikosa kosa.Unajua hii barabara ya Dar Arusha siku hizi imejaa migahawa mizuri usipokuwa makini unaweza kunywa ukadhani unaendesha gari barabara za katikati ya mji ambako ni rahisi sana kuendesha gari hata kama umekunywa na usipate ajali lakini unapokuwa umekunywa na unaendesha gari barabara kuu (highway) kupata ajali ni jambo rahisi sana.

RIP Ngowi.

Pole sana Mkuu Ngongo. Safari ndefu inatahitaji umakini sana.
 
Mkuu wangu MSALANI si kama namsema vibaya marehemu hapana lakini marehemu Ngowi anawakilisha vijana wengi wa kipindi hiki cha sasa.Wakati sisi tunapata ajira ya kwanza tulikimbilia kununua viwanja na mashamba siku hizi vijana wengi hasa hizi taasisi za bank,mawasiliano (simu) and other kijana ajira ya kwanza anakimbilia kununua alteza mkopo unamtafuna,kumaintain gari mafuta na matengenezo kimbembe matokeo yake unakuta mtu kafanya kazi miaka 10 hana maendeleo yanayoendana na kipato chake.Fikiria kijana Ngowi kanunua gari bado anaishi na Baba na Mama wengine wana park magari kwenye nyumba za kupanga akitoka barabarani status ipo juu ukienda kwake kapanga au anakula kwa Baba na Mama niambie kijana wa jinsi hii baada ya miaka 10 atakuwa yupo wapi utakuta kamtia mtoto wa watu mimba kashindwa kuoa mwisho wa siku mtoto wake analelewa na Mama & Baba mkwe au na Mama na Baba yake mzazi.Haya ndio maisha ya vijana wengi wanapenda kuweka heshima bar.Ukichinguza marehemu alifuata nini Dar unaweza kuzimia kabisa kama si kufa,nimetoa hi mifano kwasababu nina ya wadogo zangu,majirani,marafiki ndugu jamaa hadith ni hizo hizo.

Kwetu tuna dogo wa mwisho mara kadhaa anakwenda Dar self drive kufuata birthday ya marafiki zake.Ebu pata picha 750 x 2 unaweza kuona jinsi kizazi cha sasa kilivyo hovyo,hapo kapanga baada ya sisi kumkomalia aondoke nyumbani kanuna kweli kweli.

Excellent! Mimi ninajirani yangu hapa hana gari lakini mpangaji wake ana magari mawili - Nissani la nguvu na Chaser
 
Mkuu Ngongo unaongea maneno ya busara sana. Ila kizazi hiki cha wala majani sidhani kama wanalielewa hili.
 
Last edited by a moderator:
Kwa harakaharaka inaonyesha dereva wa bus ali overtake bila tahadhari/waliovertake wengi naye slifuata mkumbo bila kuwa na clear visibility. Na hiki ndicho chanzo cha ajali nyingi ktk barabara zetu.
Tusubiri taarifa rasmi ya polisi juu ya chanzo cha ajali.
 
RIP Marehemu

Mzee wa hawa jamaa ni mtu wetu wa karibu sana

Poleni familia kwa kuwa uchungu mlionao hauelezeki. MUNGU awafariji
 
Ushauri kwa wale madereva wa mijini ambao hupata safari za masafa marefu. Ukiwa na safari ndefu kamwe usithubutu kula chakula kingi kwani husababisha uzingizi. How?....unapo kula chakula kingi damu huteremka nyingi tumboni kwenda kuyeyusha chakula (kumeng'enya)hivyo sehemu nyingine huathiriwa kwa kuwa na upungufu huo wa damu. Kichwa huchukuwa sehemu kubwa sana ya damu iliyopo mwilini hivyo unapotokea upungufu wowote basi husababisha usingizi ili kuhifadhi damu kidogo iliyopo na ili ubongo uendelee kufanya kazi kama kawaida. jambo hili hufanyika kwa masaa takribani mawili hivi tokea ule chakula chako. Hivyo, nahisi hawa jamaa wali kula chakula pale Mombo au korongwe na digestion ilipoanza ku-take place dereva akaanza kusinzia na kupoteza mwelekeo.

Jingine, unapoendesha gari kwa masafa marefu hakikisha abiria aliyepo kiti cha mbele sambamba na dereva halali kwani kisaikolojia ina mfanya dereva naye kusikia usingizi. abiri ahuyo akisinzia simamisha gari na mwombe ahamie kiti cha nyuma. Hakikisha mtu anaye kaa hicho kiti ni mpiga stori sana .

ni hayo kwa leo

Word

nilishawahi kusikia hili mahali!!!
 
Ha ha ha ha ha umenikumbusha sakata la ubomoaji wa nyumba za jiji maeneo ya Kaloleni ya juu,kaloleni ya chini,Kilombero na Fire.Kuna jamaa zangu wawili mmoja akiishi mitaa ya Kaloleni ya juu alikuwa na magari mawili siku macaterpiller yanapita watu wakamwambia akalale kwenye magari yake moja la watoto na lingine atumie na mke wake.Mwingiine mtu mzima kabisa tena anaingiza fedha za haja kama umewahi kwenda hopital ya Selian katengenza vitanda vyote vya chuma siku nyumba zinabomolewa akaenda kujiifadhi kwenye uwanja wa kanisa .

Excellent! Mimi ninajirani yangu hapa hana gari lakini mpangaji wake ana magari mawili - Nissani la nguvu na Chaser
 
Ha ha ha ha ha umenikumbusha sakata la ubomoaji wa nyumba za jiji maeneo ya Kaloleni ya juu,kaloleni ya chini,Kilombero na Fire.Kuna jamaa zangu wawili mmoja akiishi mitaa ya Kaloleni ya juu alikuwa na magari mawili siku macaterpiller yanapita watu wakamwambia akalale kwenye magari yake moja la watoto na lingine atumie na mke wake.Mwingiine mtu mzima kabisa tena anaingiza fedha za haja kama umewahi kwenda hopital ya Selian katengenza vitanda vyote vya chuma siku nyumba zinabomolewa akaenda kujiifadhi kwenye uwanja wa kanisa .

Kweli mkuu kuna watu wameoa, kuzaa na kupata vijukuu wakiwa kwenye nyumba za shirika la nyumba NHC kama wapangaji huku wakiwa na utajiri mkubwa wa magari na biashara mbali mbali. Pita kwenye hizo nyumba za NHC uone walivyopaki migari ya nguvu lakini wengi wao hawana hata viwanja. Siku akitokea kiongozi "mwendawazimu" akasema wote waliokaa kwenye nyumba hizo kwa mika mitano na kuendelea mfululizo waondoke ili kuwapisha wengine itakuwa aibu tupu! Hao ndio wanaitwa LIfe Tenants - Yaani wapangaji wa kudumu. Mimi ningekuwa bosi wa NHC ningepitisha sheria kuwa upangaji uwe mwisho miaka 5 ili watu wengine wanaoanza maisha au kuingia mjini waweze kupata mahali pa kuishi ili kuzifanya nyumba hizo ziwe za kupokezana. Baada ya mika 5 kama mtu bado ni mjinga hawezi kuwa hata na kuchumba kamoja mjini ni bora arudi kijijini kwao.
 
Chonde chonde bandugu si kila mwendesha gari ana fit kwa masafa marefu.
Kuna mambo mengi ya kuzingatia,(hii imetangazwa lakini ajali za magari madogo ni nyingi sana sana) tunapoteza madogo wengi (nguvu kazi)
1.usiendeshe gari ukiwa umeshiba lazima utasinzia tu kama wewe si mtaalam wa masafa.
2.zingatia muda wa kulala
3.elewa sehem unayokwenda (ijue njia) same hedaru ni mkondo wa upepo magari huhama .
4.sali kwabla ya safari(wengi hupuuzia hii)
5.oga kabla ya safari au ukiwa safarini unaweza uka park kwa muda halafu ukaoga.
6.simama kila baada ya kilometer 150.
Na mengineyo mengi
 
Ushauri kwa wale madereva wa mijini ambao hupata safari za masafa marefu. Ukiwa na safari ndefu kamwe usithubutu kula chakula kingi kwani husababisha uzingizi. How?....unapo kula chakula kingi damu huteremka nyingi tumboni kwenda kuyeyusha chakula (kumeng'enya)hivyo sehemu nyingine huathiriwa kwa kuwa na upungufu huo wa damu. Kichwa huchukuwa sehemu kubwa sana ya damu iliyopo mwilini hivyo unapotokea upungufu wowote basi husababisha usingizi ili kuhifadhi damu kidogo iliyopo na ili ubongo uendelee kufanya kazi kama kawaida. jambo hili hufanyika kwa masaa takribani mawili hivi tokea ule chakula chako. Hivyo, nahisi hawa jamaa wali kula chakula pale Mombo au korongwe na digestion ilipoanza ku-take place dereva akaanza kusinzia na kupoteza mwelekeo.

Jingine, unapoendesha gari kwa masafa marefu hakikisha abiria aliyepo kiti cha mbele sambamba na dereva halali kwani kisaikolojia ina mfanya dereva naye kusikia usingizi. abiri ahuyo akisinzia simamisha gari na mwombe ahamie kiti cha nyuma. Hakikisha mtu anaye kaa hicho kiti ni mpiga stori sana .

ni hayo kwa leo

Labda jambo moja niongezee. Mirungi. Hii nayo inaumuhimu wake kwa kweli,hasa katika safari ndefu mfano dereva wa basi la abiria anatoka mwanza to dar,masaa zaidi ya 15 attention yake inahitajika mda wote. Sasa niambie hata kama anapigishwa stori mda wote,bila ya kutafuna mirungi lazima utafika mda Graf itashuka tu.
Na jinsi barabara zetu za highway zilivyo, one mistake..,kaburi linakuita.
 
ndugu zangu jamani..tulikuwa wote kwenye arusi ya mtoto wa amani ngowi...r.i.p ndugu zangu.mbele yetu nyuma yenu.
 
Yesu ni njia ya Kweli na uzima Tumtafute na kumwamini Yeye atuokoe na mauti ya milele
 
Back
Top Bottom