Bashiru Ally ni type ya kina Benson Bana. Hawezi kumfikia Chachage hata kwa 2%. Kwa taarifa yako huyu bwana ni mmoja ya wapiga debe wa CCM wazuri sana. Aliisha wahi kuwa Kampeni manager wa aliyekuwa mbunge wa CCM bukoba vijiji marehemu Sebastian Rukiza Kinyondo (RIP) ambaye alimpatia asante baada ya kuukwaa uwaziri wa kazi kwa kumwachia nyumba yake iliyo karibu na Mabibo Hostel aishi bila kulipa kodi.
Mimi huwa nikimuangalia simuamini na wala simuelewi dhamira yake ni nini hasa?, kuonekana academician?, kuonekana ni Independent person au kuonekana vipi hasa, maana matamko yake mengi hayaelezi uhalisia wa maisha ya leo zaidi ya blah blah za ujamaa. Sidhani kama hana dhamira ya kugombea nafasi ya uongozi hasa ubunge kupitia CCM, maana hiyo ni hobbie, aliishawahi kujaribu kuombea urais wa DARUSO mwaka 1998 akashindwa vibaya sana. Ila jamaa ukiwa humfahamu anaweza kukubadili nia kwa utaalamu wa kupangalia hoja. Nafikiri bado anapima upepo ili asiharibu kipaji.