Dkt. Bashiru Ally pole lakini maneno huumba

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,791
Hi vitu hufanya kazi nje ya uwezo na utashi wa kawaida wa binadamu....Na hii ndio maana tunaaswa sana tuwe na tafakuri kubwa tunapotamka mambo makubwa kwenye mazungumzo yetu

Bashiru msomi wa chuo kikuu cha Dsm wakati anateuliwa kushika wadhifa wa katibu mkuu wa CCM ... Kwa mdomo wake alitamka wazi kuwa nafasi hiyo ni kubwa sana kwake na hatarajii kushika nafasi nyingine kubwa na hata kama itatokea ATAIKATAA

Matendo ya Mungu si ya wanadamu.. Ikatokea nafasi ya katibu mkuu kiongozi ...nafasi kubwa zaidi kuliko ile ya ukatibu mkuu wa chama...!!!

Kwakuwa tumeumbwa kusahau na tumeumbiwa utashi wa kuwa dhaifu kuyakana maneno yetu hasa penye ulaji Bashiru alishindwa kutengua kauli yake ile.

Ni wazi kiroho kuwa kwakuwa alishakataa ile nafasi kubwa zaidi ya ukatibu mkuu basi kudra zimemfanya awe katibu mkuu kiongozi aliyehudumu muda mfupi zaidi.

Kama bado anajisikia kushika nafasi nyingine kubwa basi atengue kauli yake ile na mambo yatakuwa safi.

Midomo huumba... Tuwazayo na tutamkayo kwa asilimia 80 huwa...!!!! Tumakinike na kauli zetu.!

 
Back
Top Bottom