Bashiru Ally: Rebirth of Chachage? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bashiru Ally: Rebirth of Chachage?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tanganyika jeki, Dec 11, 2011.

 1. T

  Tanganyika jeki JF-Expert Member

  #1
  Dec 11, 2011
  Joined: Jun 12, 2011
  Messages: 243
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Huyu msomi toka chuo kikuu cha dsm yupo channel ten. Anasema wakulima si muda mrefu watafanya mapinduzi kwa sababu ya wakulima kusahauliwa na mpango dhaifu wa kilimo kwanza. Msomi huyu ananikumbusha chachage. Amefanana kwa mengi na marehemu chachage sethy chachage.
   
 2. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #2
  Dec 11, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,810
  Trophy Points: 280
  Ngoja tumpe muda. Akiwaweza kina Bhana na Mkandara kwa hoja na misimamo ya mahali ulipo ukweli, atastahili kufikiriwa kuvikwa taji hilo
   
 3. S

  Stephen Kagosi Member

  #3
  Dec 11, 2011
  Joined: Dec 10, 2011
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni kweli watafanya mapinduzi na kua wakulima maskini zaidi duniani *huyu msomi yuko sahihi kabisa
   
 4. T

  Tanganyika jeki JF-Expert Member

  #4
  Dec 11, 2011
  Joined: Jun 12, 2011
  Messages: 243
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mkuu msaada, nifafanulie hapo. Kwa nini wasema akiwaweza Bhana na Mkandara?
   
 5. payuka

  payuka JF-Expert Member

  #5
  Dec 11, 2011
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 832
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  huyu jamaa huwa napenda sana arguments zake, huwa zina make sense!
   
 6. T

  Tanganyika jeki JF-Expert Member

  #6
  Dec 11, 2011
  Joined: Jun 12, 2011
  Messages: 243
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Na hoja kubwa ni suala la ardhi. Km kuna jambo ambalo serikali inalifanyia mzaha ni suala hili. Ardhi kwa wakulima ni zaidi ya uchumi. Ni imani, uhai, familia. Ni kila kitu. Uwekezaji wa ardhi kwa sheria zilizopo zinasababisha uporaji wa ardhi wa wakulima. Mikoa ya pwani, arusha, morogoro, iringa na mbeya hali ni mbaya!
   
 7. M

  Mkandara Verified User

  #7
  Dec 11, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Acha Chachage pembeni, Mnajua kwamba hakuna Mwanasiasa hata mmoja Tanzania mwenye ilani inayotetea maslahi ya WAKULIMA ningawa ndilo kundi kubwa la wananchi na Kilimo ni uti wa mgongo wa Uchumi wetu?
   
 8. T

  Tanganyika jeki JF-Expert Member

  #8
  Dec 11, 2011
  Joined: Jun 12, 2011
  Messages: 243
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Ccm kuna wakati kilijinasibu chama cha wakulima. Wapi kilipoteleza? Bado chatumia alama za jembe na nyundo kwenye nembo yake. Swali ni nani mtetezi wa mkulima huyu aliyekamuliwa miaka yote hii 50 baada ya ccm kuporwa na mafisadi, mabeberu na mabepari?
   
 9. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #9
  Dec 11, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Mtetez wa wakulima
  wazir wa wakulima
   
 10. T

  Tanganyika jeki JF-Expert Member

  #10
  Dec 11, 2011
  Joined: Jun 12, 2011
  Messages: 243
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mtoto wa mkulima? Pinda?
   
 11. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #11
  Dec 11, 2011
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Hapana ... Chachage alikuwa anajishughulisha na mambo yote ya kijamii. Huyu jamaa huwa anazungumzia mambo ardhi tu.
   
 12. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #12
  Dec 11, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Bashiru Ally ni type ya kina Benson Bana. Hawezi kumfikia Chachage hata kwa 2%. Kwa taarifa yako huyu bwana ni mmoja ya wapiga debe wa CCM wazuri sana. Aliisha wahi kuwa Kampeni manager wa aliyekuwa mbunge wa CCM bukoba vijiji marehemu Sebastian Rukiza Kinyondo (RIP) ambaye alimpatia asante baada ya kuukwaa uwaziri wa kazi kwa kumwachia nyumba yake iliyo karibu na Mabibo Hostel aishi bila kulipa kodi.

  Mimi huwa nikimuangalia simuamini na wala simuelewi dhamira yake ni nini hasa?, kuonekana academician?, kuonekana ni Independent person au kuonekana vipi hasa, maana matamko yake mengi hayaelezi uhalisia wa maisha ya leo zaidi ya blah blah za ujamaa. Sidhani kama hana dhamira ya kugombea nafasi ya uongozi hasa ubunge kupitia CCM, maana hiyo ni hobbie, aliishawahi kujaribu kuombea urais wa DARUSO mwaka 1998 akashindwa vibaya sana. Ila jamaa ukiwa humfahamu anaweza kukubadili nia kwa utaalamu wa kupangalia hoja. Nafikiri bado anapima upepo ili asiharibu kipaji.
   
 13. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #13
  Dec 11, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,859
  Likes Received: 4,544
  Trophy Points: 280
  Mkuu hivi let's just imagine wakulima wafanye mgomo nchi nzima! Sipati picha...nakumbuka nilikua maeneo ya Machame in 2008, mkulima mmoja akasema kwamba serikali daima imekua ikiwatupa na akasema anatamani siku moja wakulima wote TZ wagome (ila walime tu kwajili ya familia zao) ili serikali ishike adabu!! Nikasema duh! I can't even imagine that happening!!
   
 14. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #14
  Dec 11, 2011
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Si kweli, HAKUSHINDWA VIBAYA SANA. Alishindwa lakini si kihivyo.
   
 15. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #15
  Dec 11, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,859
  Likes Received: 4,544
  Trophy Points: 280
  Mtu yeyote anaejiita msomi au msomi yeyote kujifanya independent katika namna serikali hii ya CCM inavyoendesha na kuongoza nchi, hakika msomi huyo ni bonge la mnafiki.
  Msomi huwezi kuwa undependent wakati nchi inafanya sherehe za kipuuzi mwaka mzima kwa mabilioni ya pesa wakati wanafunzi kuanzia DSM hadi Msimbati hawana madawati ya kutosha...na shida nyingine kemkem!!
  Huo uindependent utatoka wapi katika hali hiyo? Hapo msomi lazima achukue side ya kuikosoa serikali; na kwa hali ya sasa ya serikali hii ya CCM, mtu anaeikosoa serikali anachukuliwa kama mpinzani (tena CHADEMA!!)
   
 16. u

  utantambua JF-Expert Member

  #16
  Dec 12, 2011
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,373
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  He got potential, ila mlimani pale kwa sasa namkubali zaidi Dr Ng'wanza Kamata anafikra za kupinga unyonyaji wa kitabaka sana, pia nawaheshimu Dr Lwaitama, Dr Makulilo, Professor Mmuya, na Professor Munishi, kutoka idara ya siasa.
   
 17. T

  Topical JF-Expert Member

  #17
  Dec 12, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nilitegemea tu ungesema hayo..tunajua ni kwanini??

  Never appreciate akishakuwa na majina kama yaleeee..
   
 18. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #18
  Dec 12, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Bashir kuwa sawa na Chachage ni utani usofaa.

  Anaficha misimamo yake. Pale Ihungo H/school akiwa HP hakupata kutetea maslahi ya wanafunzi. Iliaminika kuwa alikuwa TISS coz it was known to be married lakini uongozi wa shule hawakumgusa
   
 19. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #19
  Dec 12, 2011
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Ni kweli tupu, good leader and organiser, but likes to lead from behind. Alikua na ndoto za kugombea urais siku moja.
   
 20. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #20
  Dec 12, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na wewe kwa asimia zote kwa kuwa umekubali kuwa alishindwa na mimi ninaamua kukitoa kivumishi cha 'vibaya sana'

  hivyo intersection kati yetu inabakia kuwa 'ALISHINDWA'


   
Loading...