Bashe: Si Lowassa pekee aliyeonewa CCM

Bashe: Si Lowassa pekee aliyeonewa CCM

Mbunge wa Nzega, Hussein Bashe amesema anaamini Edward Lowassa hakuenguliwa kwa haki na CCM katika mchakato wa kumpata mgombea urais wa chama hicho, na kwamba waziri mkuu huyo wa zamani si pekee ambaye amekumbana na uonevu kama huo.

Bashe, ambaye ameingia bungeni kwa mara ya kwanza katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana akipeperusha bendera ya CCM, pia amesema kashfa zote zinazoikumba Serikali hutengenezewa suluhisho kwa malengo fulani na si kutafuta muafaka wa haki.

Kiongozi huyo wa zamani wa Umoja wa Vijana wa CCM alisema hayo katika mahojiano maalumu na Mwananchi yaliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi.

Bashe, ambaye alikuwa kambi ya Lowassa wakati wa mchakato wa kumpata mgombea urais wa CCM, alisema ingawa hana uhusiano tena wa kisiasa na kada huyo, anaona tukio lake kuwa ni historia ya kutotendea haki wanachama wengi wa CCM. “Si Lowassa pekee, wako wengi,” alisema Bashe katika mahojiano hayo.

Chanzo: Mwananchi
Hii ni zaidi ya kula nyama ya mtu!
 
Unafik na uongo ni mwingi sana kwenye siasa.

Ni nani atakae kumuudhi "Don"?
 
Huyu Mkaka ni mfuasi na mpiga debe wa Lowasa namba moja. Kama hufahamu hilo fahamu. Na yuko hata huko CCM jina tuuu na wala si mwana CCM. Muwe mnachunguza vitu kabla ya kutoa yenu ya moyoni. Na kama watamuacja CCM atawatafuna kama mchwa maana ni moja kati ya wale wengi wa EL.
Hata kama watamtimua kina Bashe watazaliwa mamilioni kwa mamilioni, ukweli utasimama!
 
Mbunge wa Nzega, Hussein Bashe amesema anaamini Edward Lowassa hakuenguliwa kwa haki na CCM katika mchakato wa kumpata mgombea urais wa chama hicho, na kwamba waziri mkuu huyo wa zamani si pekee ambaye amekumbana na uonevu kama huo.

Bashe, ambaye ameingia bungeni kwa mara ya kwanza katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana akipeperusha bendera ya CCM, pia amesema kashfa zote zinazoikumba Serikali hutengenezewa suluhisho kwa malengo fulani na si kutafuta muafaka wa haki.

Kiongozi huyo wa zamani wa Umoja wa Vijana wa CCM alisema hayo katika mahojiano maalumu na Mwananchi yaliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi.

Bashe, ambaye alikuwa kambi ya Lowassa wakati wa mchakato wa kumpata mgombea urais wa CCM, alisema ingawa hana uhusiano tena wa kisiasa na kada huyo, anaona tukio lake kuwa ni historia ya kutotendea haki wanachama wengi wa CCM. “Si Lowassa pekee, wako wengi,” alisema Bashe katika mahojiano hayo.

Chanzo: Mwananchi
Huyu kijana anataka kuharibu mstakabali wake kwenye ccm ya magufuli. kujua kwingi kutamponza. kama anaamini upigaji dili ndio mpango bora kuiletea nchi maendeleo amfuate lowassa chadema. wananchi wanachukia upigaji dili...ni balaa kwa maendeleo ya nchi.
 
Kama kweli alikuwa anampenda Lowasa mbona hakumfata alipohama? Majitu mengine bwana
 
Kama ndiyo hivyo basi walionewa wengi akina Pinda,Bilala,Mahiga,Mwigulu .
Pia yeye alipoenda chadema aligombea peke yake yeye huko chadema hakuonea wenzake?
 
Mungu ana njia nyingi za kuepusha mambo, hapa alipanga "aonewe" ili Tz iende sawa.

Lowassa hakuonewa hata kidogo. Alikichukiza chama chake na hata Mungu wa mbinguni. Kitendo cha kuanza kampeni mapema kuanza kuwapa watu pesa halafu kuwaambia waje kujifanya wanakuomba ugombee urais kilikuwa ni maudhi kwa CCM. Halafu Januari 2015 alitoa shilingi 500,000 kwa kila mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM na shilingi 1,000,000 kwa kila mjumbe wa NEC ya CCM. Yeye alidai ni zawadi ya mwaka mpya lakini CCM waliona ni rushwa. Mambo mengine yote ya nyuma waweza kusahau. Lakini hayo mawili yalitosha kabisa kumtosa. Kumuudhi Mungu ni kule kuwarubuni watumishi wa Mungu wachungaji na mashehe na kuwapa pesa ili nao waende kwake kumwomba agombee urais. Mungu hawezi kufurahia mtu tajiri ambaye anatumia ufukara wa watumishi wake kufanikisha malengo yake ya kisiasa. Halafu kitendo cha Lowassa ambaye ni Mkristo kuingia msikitini na kuvalishwa kama Ustaadh ili tu apate kura za Waislam ni kumdhihaki Mungu kwa sababu leo huwezi kuwa Mwislam na Mkristo wakati huo huo. Ushenzi huu Mungu asingeruhusu ufanikiwe. Lowassa kapigwa chini na Mungu mwenyewe pamoja na CCM yake kwa makosa yake mwenyewe.
 
Jaji Ramadhani, Pinda, Bilall, Mwigulu, Makongoro, Wasira, Sumaye, etc. Wote ambao hawakufika 5 bora tuseme walionewa!!
Ndio tunashangaa kama PM na Makamu wa Rais walikatwa, nini EL ambaye hakuwa na wadhifa wowote!!
 
Bashe akasome definition ya political party....

Akiielewa atapunguza

4a084c1aa90d3f934c0e227a88ee6ee9.jpg

Ulimi wa bashe ni nyoka
 
Bwana Bashe, CCM ni shimo, nakushauri nenda nao kwa unafiki, angalia uko wapi, kwa wanafiki nawe kuwa mnafiki. Watakufukuza uanachama na utapoteza ubunge.
Nenda nao kinafiki for your survival! Sidhani kuwa CCM wote wanafurahia haya, hata wazee wetu wa taifa hili wako kimya, Unafiki. Nawe kuwa mnafiki UNLESS YOU MAKE A SACRIFICE LIKE LOWASA AND SUMAYE
 
Back
Top Bottom